Kigoma mna kisimati, mmependwa nyie!

Kigoma mna kisimati, mmependwa nyie!

He is the worst, probably he doesn't wanna go below the lowest standards
 
Naona kila lililo jema linasemwa juu ya mkoa wa Kigoma. Msimwangushe make nyie walau nyota inawaka. Wenzenu alikokwenda huko ukitoa "kwetu" mambo hayakuwa mazuri hivi. Mnapewa na mnaongezewa, ni rumbesa ya kila mnachokiomba. Chukueni. Natizamia mikoa mingine pia isaidiwe na kusemwa kwa mipango kama haya ya Kigoma. Naamini nchi ni moja, na maendeleo hayana Kigoma wala "kwetu".
Naona ardhi kwa maekari wanapewa walime, nasikia unaongoza mwenyewe mazungumzo ya kujenga kiwanda cha sukari. Umehaidi kupanua barabara na kuijenga upya kigoma iwe ya kisasa. Ni mipango mizuri lakini hata mikoa mingine pia walitarajia ukaongee kwa lugha za kujenga zikiwa na mtizamo chanya. Uchanya unapimwa kwa maneno ijapo matendo maridhawa kuliko maneno

Maendeleo hayana vyama, maendeleo hayana kabila wala dini. Basi hima mzee, kwingineko nako ni Tanzania.
Sikio la kufa ni la kufa tu, wape kila kitu mpaka watoto wapatie lkn nakueleza kama huna akili ya kujiendeleza huna tu.
Magofu yatabaki huko kwa sababu hivyo vitu siyo asili yao.

Mambo yao waachie uchawi wenye kujua Maendeleo wakija wao watahamia misitu ya Congo
 
Walishawahi kupewa ahadi na JK ya kuubadili mkoa wa Kigoma kuwa kama Dubai, mkuu usishangae hizo ni mbwembwe za wanasiasa wanapokuwa majukwaani.
 
Huu ni ukweli mkuu kama huamini subiri muda utaongea.

Nyerere aliliona hili kwa jicho la kwanza kama siyo la square 1 ndiyo maana alianzia ktk mfumo wa elimu mpaka makazini
Eg:
Aliyekuwa anasoma Songea alipelekwa Dodoma, wa Dodoma alipelekwa Zanzibar, wa Zanzibar akatupwa Kilimanjaro, wa kili akatupwa Mbeya, wa mbeya akatupwa bukoba, wa bukoba akatupwa Dar, wa Dar akatupwa shinyanga hivyohivyo mpaka kwenda JKT up to makazini ikawa hivyohivyo.

Hii ilikuwa ni ktk kuhamasisha watu kujifunza na to share different culture from different tribes hapa Tanzania kitu kilicholeta mwamko wa kujifunza tamaduni za mwenzako ambazo zilileta changamoto za watu kujikwamua kutoka kwenye mazingira na tabia walizozizoea.

Leo hii hakuna, mtu kazaliwa pwani kusoma pwani wanafanya kazi Pwani hakuna anachojua zaidi ya Pwani.
Hili ni TATIZO
 
Sent from my Zero Kufuli Bichwa Nazi using JamiiForums
 
Back
Top Bottom