PreGE2025 Kigoma: Matukio yanayojiri kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

PreGE2025 Kigoma: Matukio yanayojiri kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
4,783
Reaction score
14,975

WanaJF,​

Mada hii itakuwa na 'Updates' za Matukio kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Urais, Ubunge na Udiwani 2025 kama yanavyotujia kutoka kwenu kutoka mkoa wa Kigoma. Ukiwa na taarifa yoyote ambayo ni ya eneo hili tafadhali usisite kuweka.

Kigomaa.jpg

Kigoma ni mkoa uliopo magharibi mwa Tanzania, ukipakana na nchi za Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kwa upande wa magharibi na kaskazini. Mkoa huu unajulikana kwa ziwa la Tanganyika, ambalo ni moja ya maziwa marefu zaidi duniani.

MUHTASARI WA MAENEO YA UTAWALA, MKOA WA KIGOMA
Katika muhtasari wa maeneo ya utawala, mkoa huu una halmashauri ambazo zimegawanyika katika mamlaka za miji na wilaya.

Idadi ya Watu
Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022 yanaonesha kuwa idadi ya watu katika Mkoa wa Kigoma ni 2,470,967; wanaume 1,186,833 na wanawake 1,284,134, ikiwa na wilaya 5.

Idadi ya Majimbo ya Mkoa wa Kigoma
Mkoa wa Kigoma una majimbo Nane ya uchaguzi
  • Jimbo la Buyungu
  • Jimbo la Kasulu Mjini
  • Jimbo la Kasulu Vijijini
  • Jimbo la Kigoma Kaskazini
  • Jimbo la Kigoma Kusini
  • Jimbo la Kigoma Mjini
  • Jimbo la Buhigwe
  • Jimbo la Muhambwe
ILIVYOKUWA UCHAGUZI MKUU 2020

Katika uchaguzi mkuu wa 2020 mkoani Kigoma, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kilishinda kwa kiwango kikubwa katika ngazi zote.

Kwa mujibu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Hayati John Magufuli alipata kura nyingi katika mkoa huu kwenye nafasi ya urais, akipata zaidi ya asilimia 80 ya kura zilizopigwa.

Katika nafasi za ubunge, wagombea wa CCM walishinda viti vyote vya majimbo, huku ACT Wazalendo ikipoteza ngome jimbo la Kigoma mjini.

Aidha, kwenye udiwani, CCM ilijinyakulia kata takriban zote kutokana na upinzani kukumbwa na changamoto nyingi, zikiwemo wagombea wao kuenguliwa kutokana na matatizo ya kisheria au kutokidhi vigezo

Updates

January

February
March
APRIL
May
June
July
August

Septemba
Oktoba

Kamati Kuu CCM yatangaza rasmi majina ya watia nia Ubunge 2025​

  • MKOA WA KIGOMA
    Jimbo la Kakonko

    (1) Ndugu Aloyce John KAMAMBA
    (2) Ndugu CPA. Emmamuel Jeremiah GWEGWENYENZA
    (3) Ndugu Dkt. Kagoma Pius KAMANA
    (4) Ndugu Alan Thomas MVANO
    (5) Ndugu Rosemary Delfina RUHINDA
    (6) Ndugu Modest Joseph APOLINARY
    (7) Ndugu Msakila Mussa KABEMBE

    Jimbo la Muhambwe
    (1) Ndugu Florence George SAMIZI
    (2) Ndugu Jamal Abdallah TAMIM
    (3) Ndugu Dickson Kisondaka BIDEBELI
    (4) Ndugu Andason Njiginya KABUKO
    (5) Ndugu Jeraidina Paskal KABULULU
    (6) Ndugu Julias Paul THOMAS
    (7) Ndugu Nduhilibusa Francis MAPIGANO

    Jimbo la Kasulu Mjini
    (1) Ndugu Prof. Joyce Lazaro NDALICHAKO
    (2) Ndugu David Issaya DYOYA
    (3) Ndugu Fadhili Salumu NGEZI
    (4) Ndugu Magterh Bernard KILENZA
    (5) Ndugu Mteule Amon MKOMBO
    (6) Ndugu Patrick ZULIGIMBASHA

    Jimbo la Kasulu Vijijini
    (1) Ndugu Augustine Vuma HOLE
    (2) Ndugu Agripina Zaitum BUYOGERA
    (3) Ndugu Edibiliy Kazala KIMNYOMA
    (4) Ndugu Emmanuel Thomas MSASA
    (5) Ndugu Selemeni Marumbo WANDWI
    (6) Ndugu Shukurani Patrick MPAGANYE

    Jimbo la Buhigwe
    (1) Ndugu Ntakimanzi L. YUSUPH
    (2) Ndugu Elias M. KAYANDABILA
    (3) Ndugu Dr. Yusilida KABUJANJA
    (4) Prof. Pius YANDA
    (5) Ndugu Cassian C. MBAJIJE
    (6) Ndugu Eliadory Felix KAVEJURU

    Jimbo la Kigoma Kaskazini
    (1) Ndugu Peter J. SERUKAMBA
    (2) Ndugu Assa N. MAKANIKA
    (3) Ndugu Godfrey H. RUSIMBI
    (4) Ndugu Marcel N. TALLINEGA
    (5) Ndugu Shaaban A. MTUNDA
    (6) Ndugu Athumani S. BAKENE

    Jimbo la Kigoma Kusini
    (1) Ndugu Nuru Issa KASHAKARI
    (2) Ndugu Yasinta Zacharia KAFULILA
    (3) Ndugu Nashon Wiliam BDYANGUZE
    (4) Ndugu January Benson KIZITO
    (5) Ndugu Peter Hezron NYABAKARI
    (6) Ndugu Majaliwa Zubeir KAYANDABILA
    (7) Ndugu Dkt. Rajabu Abed RIJA

    Jimbo la Kigoma Mjini
    (1) Ndugu Baruani Abdallah MUHUZA
    (2) Ndugu Kirumba Shaaban NG’ENDA
    (3) Ndugu Ahmadi Yahya SOVU
    (4) Ndugu Clayton Revacatus CHIPONDA (Baba Levo)
    (5) Ndugu Maulid Mohamed KIKONDO
    (6) Ndugu Moses John BASILA
ZINGATIA: Mikoa yote ina mada yake ya 'Update' ili kuweka wepesi katika ufuatiliaji.
 
Back
Top Bottom