Kigoma iko mbele kwa saa moja!

Kigoma iko mbele kwa saa moja!

Red Giant

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2012
Posts
15,650
Reaction score
20,993
Tanzania tunatumia masaa ya kwenye longitudo 45 mashariki ya greenwich. Mji wa Kigoma upo nyuzi 29 mashariki. Hapo pana tofauti ya nyuzi 16. Kwenye masaa, nyuzi 15 ni sawa na saa 1. Hivyo masaa wanayotumia Kigoma na masaa halisi kunatofauti ya saa moja.
Inabidi wana Kigoma muanze kutumia masaa yenu halisi.
 
Duh basi hiyo ni habari njema. So huku mfano Dar ikiwa ni saa 17:55 Kigoma itakuwa saa 18:55 ama 16:55?
 
kichwa cha habari hakiko sawa kama unavyokata iwe, Kigoma iko magharibi zaidi, kwa hiyo ilitakiwa iwe nyuma kwa saa moja si kuwa mbele kwa saa moja.
ilitakiwa iwe nyuma saa 1 kwa hiyo kwa sasa iko mbele.
 
Lakini mji wa Mtwara ndiyo mji ulio mashariki zaidi ya Tanzania. Ukiwa Mtwara saa 12:30 ya jioni ni usiku kabisa!
 
Masaa ya kigoma ni kwa matakwa ya kisiasa zaidi kuliko kijiografia
 
Hata ngara kwakwli saa moja asubuhi ya ngara ni usiku sana yofauti na saa moja ya dar..yani watoto wa shule uwa nawaonea huruma wanaamka usiku kwenda shule wakiwai namba saa moja.
!!
 
Duh basi hiyo ni habari njema. So huku mfano Dar ikiwa ni saa 17:55 Kigoma itakuwa saa 18:55 ama 16:55?

Mi siku moja nilikuwa mpanda, bwana nipo ndani naangalia chanel ten, mala naona taarifa ya habari ya saa moja jioni, nikadhani tv imebuma kwani nje jua bado linaonekana kabisa!! eti saa moja!! niliona maajabu tena kama ndio unatoka dar, kasheshe asubuhi saa kumi 12,utadhani ni saa kumi giza nene kweli.
 
tanzania tunatumia masaa ya kwenye longitudo 45 mashariki ya greenwich. mji wa kigoma upo nyuzi 29 mashariki. hapo pana tofauti ya nyuzi 16. kwenye masaa, nyuzi 15 ni sawa na saa 1. hivyo masaa wanayotumia kigoma na masaa halisi kunatofauti ya saa moja.
inabidi wana kigomamuanze kutumia masaa yenu halisi.

Haiwezekani kamwe kwa Kigoma kuwa saa moja mbele. Latitudes na longitudes za Kigoma zinaweza kuifanya Kigoma kuwa saa moja nyuma na sio mbele kama unavyosema Mh Red Giant .

Halafu time zones hazifuati longitudes na latitudes pekee. Geographical boundaries zinahusika pia na ndio maana muda (time) wa Kigoma ni sawa na muda (time) wa Tanzania kwa ujumla na si vinginevyo .
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom