Kigogo wa Wema Sepetu 'CK' ahukumiwa miaka 5 jela kwa wizi wa Tsh 100m ofisi ya Waziri Mkuu

Rais2020

JF-Expert Member
Jul 14, 2016
3,248
5,532
Clement Mwankayi Kiondo (43) “CK” aliyekuwa anajulikana kama “Kigogo wa Wema” ambaye alikuwa Mhasibu wa Wakala wa Ndege za Serikali, pamoja na aliyekuwa Ofisa wa benki ya NBC, Emmanuel Kagondela (36) wamehukumiwa kwenda jela miaka mitano kila mmoja kwa kukutwa na hatia ya makosa matatu ya kula njama, kughushi na kujaribu kujipatia zaidi ya shilingi milioni 100 kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu.

Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es salaam, Huruma Shaidi alisema baada ya kupitia ushahidi huo bila kuacha shaka, Mahakama yake imewatia washitakiwa hatiani kwa makosa yote matatu waliyoshtakiwa nayo.

“Mahakama hii inawahukumu washitakiwa wote kwenda jela miaka mitatu kosa la pili na miaka miwili kwa kosa la tatu na yote mtaitumikia kwa pamoja,” alisema Hakimu Shaidi

Kwakuwa wanatumikia vifungo hivi kwa pamoja, washitakiwa hao watatumikia adhabu hii kwa miaka mitatu. Washitakiwa hao walifikishwa Mahakamani hapo kwa mara ya kwanza Juni 26 mwaka 2015 na kusomewa mashitaka hayo matatu. Katika kesi ya msingi, ilidaiwa kuwa siku na mahali pasipofahamika jijini Dar es salaam washitakiwa kwa pamoja walikula njama ya kutenda kosa la wizi.

Katika shtaka la pili, ilidaiwa kuwa Machi 2014 jijini Dar es salaam, mshitakiwa wa kwanza alighushi hundi namba 302002 yenye thamani ya shilingi 100,430,430.50 akionesha kwamba imetolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu kwenda Ofisa Mkuu wa Wakala wa Ndege za Serikali aliyetajwa kwa jina la Joseph huku akijua sio kweli.

Katika shtaka la tatu, ilidaiwa kuwa Machi 13,2014 katika benki ya NBC tawi la Viwandani lililopo Ilala jijini Dar es salaam, washitakiwa kwa pamoja waliofanya jaribio la wizi wa shilingi milioni 100.4

January 31,2017

Source: Swahili times.com
 
"Katika kesi ya msingi, ilidaiwa kuwa siku na mahali pasipofahamika jijini Dar es salaam washitakiwa kwa pamoja walikula njama ya kutenda kosa la wizi."

Hapo hatia inatokea wapi, kama siku na mahala hazifahamiki?
 
Picha ya hao wahalifu na Wema ili kunogesha habari!

WhatsApp Image 2017-02-01 at 12.09.01.jpeg
 
Jamaa anaiba pesa za umma na kwenda kuhonga wadada wa mjini Wema na Kajala. Wacha kwanza aende jela.

-----------------------

Aibu sana.Unakwenda jela for a hundred million, tena mhasibu ! Njaa gani hiyo.
 
Back
Top Bottom