Wamiliki wawili wa Ghorofa lililoporomoka na kuua watu 29 Kariakoo wamepelekwa Mahabusu, mmoja apata dhamana

Mtoa Taarifa

Senior Member
Sep 21, 2024
151
430
Wamiliki wawili wa jengo la ghorofa lililoporomoka Kariakoo, Dar es salaam wamepelekwa mahabusu baada ya kukosa dhamana huku mmoja wao ambaye ni Leondela Mdete (49) akipata dhamana katika kesi ya kuua bila kukusudia inayowakabili katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Waliokosa dhamana ni Zenabu Islam (61), Mkazi wa Kariakoo na Ashour Awadh Ashour (38), Mkazi wa llala ambapo kwa pamoja walipewa masharti ya kuwa na Wadhamini wawili kila mmoja wenye barua za utambulisho, kitambulisho cha Taifa na watatakiwa kusaini bondi ya shilingi milioni tano kwa kila mmoja.

Wafanyabiashara hao wamefikishwa Mahakamani hapo leo na kusomewa mashtaka yao mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Godfrey Mhini ambapo Wakili Mwandamizi wa Serikali Adolfu Lema akisaidiana na Neema Mwanga na Erick Kamala walidai kuwa Washitakiwa hao walitenda kosa hilo Novemba 16 mwaka huu Mtaa wa Mchikichi na Kongo, jijini Dar es salaam.

Ilidaiwa kwamba, Washitakiwa hao kwa pamoja walishindwa kutimiza majukumu yao na kusababisha vifo vya Watu 31 ambapo baada ya kuwasomea mashitaka hayo, Hakimu Mhini aliwaeleza Washitakiwa kwamba hawatakiwi kujibu lolote kwasababu Mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo huku upande wa Jamhuri ukidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika hivyo ukaiomba Mahakama ipange tarehe nyingine ya kutajwa, kesi imeahirishwa hadi December 12 mwaka huu.

Pia Soma: Wamiliki jengo lililoporomoka Kariakoo wafikishwa Mahakamani Kisutu
 
Back
Top Bottom