Kigogo wa Sukari: Magufuli ametunyoosha

Judi wa Kishua

JF-Expert Member
Apr 15, 2012
1,066
1,048
Mfanyabiashara mmoja mkubwa, ambaye hivi karibuni alikutwa na tani
nyingi za sukari katika ghala lake (jina lake linahifadhiwa) amekiri kuwa utawala wa Rais John Magufuli umewanyoosha kwa vile hataki mchezo kazini.

Akizungumza na gazeti hili ofisini kwake hivi karibuni, pamoja na kutoa ufafanuzi wa jinsi anavyoifanya biashara hiyo kwa mujibu wa utaratibu, lakini pia alisema wafanyabiashara
wamejikuta wakilazimika kufuata sheria na kuacha konakona kama ilivyokuwa siku za nyuma.

“Sukari iliyokutwa kwangu haikuwa na matatizo ndiyo maana hakuna hatua zilizochukuliwa kwa sababu ipo ‘clean’ (halali), lakini nikuambie ndugu yangu, Magufuli katunyoosha, katufanya
tuufyate, maana sasa hivi hakuna konakona, zamani ungeweza kusema ngoja nifanye ujanja, lakini hakuna,” alisema bila kutoa ufafanuzi zaidi
wa kauli hiyo, licha ya kuombwa kufanya hivyo.

Baada ya Rais Magufuli kupiga marufuku uagizaji wa sukari kutoka nje, akidai baadhi ya wafanyabiashara wasio waaminifu huagiza bidhaa hiyo ikikaribia kumalizika muda wake, uhaba mkubwa ulijitokeza, huku kukiwa na tetesi za bidhaa hiyo kufichwa makusudi ili kupandisha bei sokoni.

Kufuatia hali hiyo, rais aliagiza kukamatwa kwa wafanyabiashara wote watakaobainika kuificha sukari hiyo, hali iliyosababisha baadhi yao, wakiwemo Harun Zacharia, Haidary Mohamed,
Mohamed Enterprises na wengineo kukutwa nayo kwenye maghala yao na hivyo kuhojiwa na vyombo vya dola.

Chanzo : Global publishers
 
Wambane ataje hizo kona kona huenda ametumaliza na sukari chafu iliyokwisha muda wa matumizi.
 
Wafanya biashara wakinyooka wananchi wa kawaida ndio tunanyooka na kukauka kabisa, leo TZ imekuwa nchi ya foleni ya sukari?! Sikutegemea hii historia ingejirudia bila vita nilisikia ilikuwepo kwa sababu Iddi amini alituchokoza now?! kazi kweli
 
Kona kona ni nyingi awa wafanyabiashara wasio wazalendo wamefanya uovu mwingi sana huko nyuma. Acha Magu atunyooshee nchi.
kona zenyewe zitakuwa sukari feki, magendo, iliyoexpire, kupunja kipimo, iliyochanganywa na molasesi, ukwepaji wa kodi, kuficha, n.k
 
Story mbon kama imetungwa na kuandikwa na alietunga? Hakuna weledi hapo wala ukweli! Hao wafanyabiashara wana issues kibao na wameiba miaka zaidi 20 sasa wako vizuri! Watanzania ndio tunanyooshwa....wale matajiri hawana shida kabisa nakwambia
 
Njaa ni mbaya sana, yani mpaka sasa bado CCM ina ujasiri wa kuongelea sukari?
Hizi akili zinashabihiana na za Agness wa uchungu.
 
Mbona maelezo hayaoneshi walichofanywa? Kichwa cha habari ni kinyume cha habari yenyewe.
 
Back
Top Bottom