Wakulima wa miwa Kilombero wampongeza Bashe sheria mpya ya sukari

Rege

Senior Member
Jul 9, 2022
116
152
Wakulima wa miwa katika Bonde la Mto Kilombero mkoani Morogoro wamempongeza Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe kwa uamuzi wake wa kubadilisha sheria ya sukari mwaka 2024 kwamba itawaletea manufaa makubwa na wamekanusha taarifa zilizotolewa na Mbunge wa Kisesa Luhaga Mpina kuhusu kilimo cha miwa na biashara ya sukari na kwamba wao hawana malalamiko yoyote na Wabunge wala Serikali. .

Wakizungumza na waandishi wa habari wilayani Kilombero viongozi wa umoja wa vyama vya wakulima pamoja na baadhi ya wakulima wanaounda vyama 17 vya ushirika (AMCOS), wamekanusha taarifa hizo wakidai kuwa ni uzushi na upotoshaji unaofanywa kwa maslahi ya kisiasa na kwamba wao hawajaathiwa chochote na uingizaji wa sukari kutoka nje ya nchi.

“Hakujawahi kutokea bei ya miwa kushuka kwani tangu tuanze kuuza miwa msimu huu tumeuza kwa bei nzuri na kwamba hata hiyo sheria mpya ya sukari iliyopitishwa na Bunge hatuoni kama inatuathiri kwa chochote ni sheria nzuri tunampongeza wabunge wetu Assenga na Londo kwa kuunga mkono sheria hiyo hizo taarifa zingine mnazosikia ni za uongo" Bakari Mkangamo Mwenyekiti wa Wakulima wa Kilombero.

Aidha wakulima hao wamedai kuwa hakujawahi tutokea ucheleweshwaji wa malipo kwa wakulima kutoka kwenye kiwanda cha Kilombero na badala yake malipo yalichelewa kwa siku mbili tu kutokana na mifumo mipya iliyowekwa kiwandani hapo ambapo walitakiwa kulipwa tarehe 15 na badala yake walilipwa tarehe 17.

Wakulima hao wamesisitiza kwamba hakuna athari zozote zilizowapata kufuatia uamuzi wa serikali kutoa vibali vya kuagiza sukari nje kupunguza ongozeko la bei ya bidhaa hiyo ili kuleta ahueni kwa wananchi.

Vilevile wakulima hao wamesema kuwa vyama vyao vina ushirikiano mzuri na kiwanda cha sukari Kilombero na wanayo matumaini makubwa ya mageuzi ya zao hilo, kwa kuwa kiwanda hicho kinalenga kufanya upanuzi mkubwa utakaopelekea wakulima kuuza miwa kwa wingi zaidi.

Pia wamempongeza Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe kwa sheria nzuri ya sukari ya mwaka 2024 kwani itasaidia kuwawezesha wananchi kupata sukari kwa bei nafuu nafuu.
 
Hao ndio watu wenye shukrani. Wanajitambua, wameweka siasa pembeni, wameangalia maslahi yao na kuielewa nia nzuri ya serikali ya kuendeleza zao la miwa. Wapongezwe!
Hao wanaopiga propaganda mitandaoni watafeli tu.
 
Wakulima wa miwa katika Bonde la Mto Kilombero mkoani Morogoro wamempongeza Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe kwa uamuzi wake wa kubadilisha sheria ya sukari mwaka 2024 kwamba itawaletea manufaa makubwa na wamekanusha taarifa zilizotolewa na Mbunge wa Kisesa Luhaga Mpina kuhusu kilimo cha miwa na biashara ya sukari na kwamba wao hawana malalamiko yoyote na Wabunge wala Serikali. .

Wakizungumza na waandishi wa habari wilayani Kilombero viongozi wa umoja wa vyama vya wakulima pamoja na baadhi ya wakulima wanaounda vyama 17 vya ushirika (AMCOS), wamekanusha taarifa hizo wakidai kuwa ni uzushi na upotoshaji unaofanywa kwa maslahi ya kisiasa na kwamba wao hawajaathiwa chochote na uingizaji wa sukari kutoka nje ya nchi.

“Hakujawahi kutokea bei ya miwa kushuka kwani tangu tuanze kuuza miwa msimu huu tumeuza kwa bei nzuri na kwamba hata hiyo sheria mpya ya sukari iliyopitishwa na Bunge hatuoni kama inatuathiri kwa chochote ni sheria nzuri tunampongeza wabunge wetu Assenga na Londo kwa kuunga mkono sheria hiyo hizo taarifa zingine mnazosikia ni za uongo" Bakari Mkangamo Mwenyekiti wa Wakulima wa Kilombero.

Aidha wakulima hao wamedai kuwa hakujawahi tutokea ucheleweshwaji wa malipo kwa wakulima kutoka kwenye kiwanda cha Kilombero na badala yake malipo yalichelewa kwa siku mbili tu kutokana na mifumo mipya iliyowekwa kiwandani hapo ambapo walitakiwa kulipwa tarehe 15 na badala yake walilipwa tarehe 17.

Wakulima hao wamesisitiza kwamba hakuna athari zozote zilizowapata kufuatia uamuzi wa serikali kutoa vibali vya kuagiza sukari nje kupunguza ongozeko la bei ya bidhaa hiyo ili kuleta ahueni kwa wananchi.

Vilevile wakulima hao wamesema kuwa vyama vyao vina ushirikiano mzuri na kiwanda cha sukari Kilombero na wanayo matumaini makubwa ya mageuzi ya zao hilo, kwa kuwa kiwanda hicho kinalenga kufanya upanuzi mkubwa utakaopelekea wakulima kuuza miwa kwa wingi zaidi.

Pia wamempongeza Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe kwa sheria nzuri ya sukari ya mwaka 2024 kwani itasaidia kuwawezesha wananchi kupata sukari kwa bei nafuu nafuu.
Kesi zipo mahakamani..!!! Nyie pongezaneni, nyie kaneni, lakini mjue kesi zipo mahakamani..!!
 
Back
Top Bottom