Kigogo wa Polisi Arusha adaiwa kukodi majambazi wamuue mumewe, wamkatakata kwa mapanga

Halafu polisi kama wanamlinda mtuhumiwa vile,hii habari kuvuja kwa media itakua imewasikitisha sana.
 
Mkaguzi Msaidizi wa jeshi la Polisi kituo cha Usariver, Demetrida Sweethbert Thadeo Mkazi wa Momela, wilayani Arumeru Mkoani Arusha, anahojiwa na polisi katika kituo hicho akituhumiwa kukodi majambazi waliomjeruhi kwa mapanga mumewe Daud Thomasi Ayo kutokana na ugomvi wa kifamilia.

Kwa mujibu wa taarifa za ndani za jeshi hilo na kuthibitishwa na Mumewe, tukio hilo lilitokea usiku wa desemba 24, 2023 nyumbani kwao Momela ambapo watu wasiojulikana walimvamia akiwa anaingia nyumbani kwake akijaribu kufungua geti ndipo watu wanne walijitokeza na kuanza kumkatakata kwa mapanga sehemu mbalimbali za mwili wake.

Inadaiwa kuwa siku chache kabla ya tukio hilo Lemetilda alionekana akiharibu mfumo wa kamera za nyumbani kwao (CCTV Camera)na mumewe alipomuuliza kwanini anazima kamera hakuweza kutoa majibu ya maana ila alisema anarekebisha.

Taarifa zinasema kuwa wanandoa hao ambao wamebahatika kuwa na watoto wawili akiwemo mchanga wa kunyonya, Mume amekuwa akimtuhumu kujihusisha na mahusiano yasiofaa na mara nyingi tangia amejifungua alikuwa hamnyonyeshi mtoto ipasavyo na wakati mwingine amekuwa akilala nje ya ndoa na kurejea asubuhi.

Ayo ambaye amelazwa katika hospitali ya ALMC jijini Arusha, alithibitisha kutendewa unyama huo na mkewe kutokana na ugomvi wa Mara kwa mara ndani ya familia na kwamba kati ya majambazi wanne waliomvamia siku hiyo mmoja aliyetajwa kwa jina moja la Agustino anashikiliwa katika kituo hicho cha polisi na upelelezi unaendelea.

Hata hivyo taarifa zimedai kuwa baada ya mtuhumiwa kuhojiwa na polisi ,alikiri kuhusika na tukio hilo na kueleza kuwa yeye na wenzake walitoka dar es salaam baada ya kuahidiwa na askari huyo ujira wa Tsh. milioni 3 na tayari walikabidhiwa kitita cha sh,500,000 kama malipo ya awali kwa ajili ya kumuua mumewe.

"Hawa vijana aliwakodi kutoka Dar ili wamuue mume wake na siku ya tukio huyo mkewe (Askari) alikuwemo ndani ila alizima CCTV CAMERA na mumewe alipokuja majira ya saa nne usiku vijana hao walimvamia baada ya kuteremka kwenye gari na kuanza kumkatakata na alipoanguka chini walijua amekufa na wote walitoweka" kilisema chanzo ndani ya jeshi hilo.

Daudi alipotakiwa kuongelea tukio hilo mara ya kwanza alikubali na kuajidi kutoa ushirikiano lakini baadaye alipoitwa kutoa maelezo kituo cha polisi aliomba asiongee na mwandishi wa habari kwa madai kwamba amekatazwa na polisi baada ya kuahidiwa, kumchukulia hatua za kinidhamu kwa mkewe.

Baadhi ya askari polisi kituoni hapo wamesikitishwa na tukio hilo wakidai kwamba mara kadhaa mumewe amekuwa akija kituoni hapo kwa mkuu wa kituo afande ODC, kulalamika kuhusu tabia na mwenendo wa mkewe.

Baba mzazi wa Daudi, Thomas Ayo alikiri kuwa ndoa ya wawili hao ina mgogoro wa mara kwa mara na amesikitishwa sana na tukio hilo na mwanaye alimwambia aliyehusika ni mkewe ila polisi wamemzuia asiongee kwa waandishi wa habari kwani jeshi hilo limemwahidi kumfukuza kazi mkewe.

Kamanda wa polisi Mkoa wa Arusha, Justin Masejo alipoulizwa alisema bado hajapata taarifa ila aliahidi kulifuatilia kwa wasaidizi wake na kulitolea ufafanuzi.

"Ndo nalisikia kwako ila ngoja nifuatilie nitakupa taarifa" Hata hivyo ndugu na jamaa wamelalamikia hatua ya askari huyo kutochukuliwa hatua ikiwemo kufukuzwa kazi kwani mara kwa mara amekuwa akikabiliwa na tuhuma nyingi ambazo jeshi hilo limezifumbia macho, ikiwemo kashfa ya usagaji..

Sent from my SM-A127F using JamiiForums mobile app
mumewe alipokuja majira ya saa nne usiku vijana hao walimvamia baada ya kuteremka kwenye gari na kuanza kumkatakata na alipoanguka chini walijua amekufa na wote walitoweka" kilisema chanzo ndani ya jeshi hilo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Du! Kumbe ni msagaji? Sasa mbona amezaa? Au ni double....msagaji na mgegedwaji?
 
Kuwe na ndoa za mikataba haya mambo ya kusema mtakuwa mwili mmoja mpk kifo kiwatenganishe ni ujinga tupu. Wakristo tubadilike hakuna sababu ya kulazimisha ndoa kama kuna mgogoro watu waachane mapema.

Wanandoa wengi hawapendani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuwe na ndoa za mikataba haya mambo ya kusema mtakuwa mwili mmoja mpk kifo kiwatenganishe ni ujinga tupu. Wakristo tubadilike hakuna sababu ya kulazimisha ndoa kama kuna mgogoro watu waachane mapema.
Kwa mara ya kwanza umeongea jambo muhimu sana sana!! Una akili nyingi mno. Kuanzia Leo Mimi ni CHAWA wako
 
Mwanaume alifanya uzembe kidogo, kitendo cha kumkuta mkewe anachezea CCTV kamera na wakati wana ugomvi mkubwa ndani, pale pale machale yalipaswa kumcheza.
Ukisoma katikati ya mistari utagundua kwamba mwanaume analishwa na Afande.

Mwanaume huwezi kuwa mnyenyekevu namna hiyo kama mwehu. Mwanaume unakwendaje kumshitaki mwanamke? Mwanamke akizingua unamzingua palepele
 
Back
Top Bottom