Hapo ndo ninaposhangaa mimi, mwathiri hajatajwa jina, katajwa mwathirika!!
Wanaume wengine bwana! ndio yale yale ya mambo ya SIMU!
[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: contentheading, width: 100%"]Kigogo wa CCM mbaroni kwa tuhuma za mauaji [/TD]
[TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"]
Send to a friend [/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: createdate"] Tuesday, 06 September 2011 20:26 [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD] 0diggsdigg
Mussa Mwangoka, Sumbawanga
JESHI la Polisi Mkoa wa Rukwa linamshikilia kiongozi mmoja mwandamizi wa CCM mkoani hapa, kwa tuhuma za mauaji ya mkewe kutokana na kile kilichoelezwa kuwa ni wivu wa mapenzi.
Kifo cha mwanamke huyo kinadaiwa kwamba kilitokana na kipigo kutoka kwa mumewe baada ya kumsababishia majeraha hivyo kuvuja damu nyingi na kufariki dunia baada ya kufikishwa hospitalini.
Kamanda wa polisi Mkoa wa Rukwa, Isuto Mantage alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba kiongozi huyo wa anashikiliwa na polisi na afikishwa mahakamani wakati wowote.
Alisema tukio hilo lilitokea jana asubuhi majira ya saa tatu katika Kitongoji cha Kantalamba.
Kwa mujibu wa majirani, ugomvi wa wanandoa hao ulianza pale kiongozi huyo alipobaini kuwa mkewe yupo kwenye moja ya baa mjini hapa. Walisema baada ya kubaini hilo aliamua kumfuata na kumtaka warejee nyumbani.
Wakiwa nyumbani, inadaiwa kwamba mzozo ulianza baada ya mumewe kudai kwamba mkewe anatembea na wanaume mwingine. Baada ya mvutano wa muda mrefu, inadaiwa kuwa mwanamume huyo alianza kumpiga ngumi, mateke na kumbana shingo.
Majirani waliposikia sauti walifika, lakini walimkuta mwanamke huyo ameishiwa nguvu na ameanguka chini.
Majirani hao wakizungumza kwa sharti la kutotajwa jina gazetini walisema ilionekana kana kwamba mwanamke huyo alipigwa na kitu kizito kichwani. Walimbeba na kumpeleka hospitali jirani ya Dk Atman na walipompima walibaini kuwa ana majeraha ya damu kuvujia ndani ya ubongo.
Akiwa kwenye hospitali hiyo ya Dk Atman inaelezwa kuwa hali yake ilizidi kuwa mbaya hivyo wakachukua uamuzi wa kumpeleka Hospitali ya Mkoa wakati huo akiwa amepoteza fahamu. Alilazwa katika wodi ya wagonjwa mahututi ambako alifariki alipokuwa akipatiwa matibabu.
Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mkoa, Dk Sadun Kabuma alisema walipomchunguza kwa makini walibaini kuwa damu inavuja ndani ya ubongo.
"Inawezekana alikuwa akikibamiza kichwa cha mwanamke huyo ukutani kwa nguvu hali iliyosababisha kuvuja kwa damu nyingi kwenye ubongo wake...... hata maiti anaendelea kuvuja damu puani," alisema Dk Kabuma.[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
Source:
Kigogo wa CCM mbaroni kwa tuhuma za mauaji