Horseshoe Arch
JF-Expert Member
- Aug 10, 2009
- 13,402
- 12,787
CCM mwaka huu agenda kuu ni Lowassa tu...
Muacheni Lowassa nyie waswahili,siasa ni popularity nyie waswahili.Lowassa njoo chadema wakikuwekea vikwanzo sharti ni moja tu.Kama haukuwa richmond basi alikuwa nani?.kutafuta wadhamini ni campaign vile vile.....si lazima uwaridhishe na waridhike....mnataka awe bubu,au wananchi wasiende kuona?.Nyie chukueni hao 450 na baki ni kuwa amefaulu vizuri sana.....katika siasa pia kuna kufaulu na kufaulu vizuri sana
Kigogo mmoja wa CCM ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM amesema kuwa mtangaza nia Edward Lowassa anapiga kampeni badala ya kutafuta wadhamini. Mjumbe huyo wa CC amenidokeza kuwa jambo hilo litamkwamisha vya kutosha Lowassa katika kujaribu kupenya katika mchujo wa kuelekea kupigiwa kura na Mkutano Mkuu.
"Unajua ndugu yangu, Lowassa anajiharibia mwenyewe. Kitendo cha kuandaa watu kwa maelfu na kuzungumza nao ni kampeni na si kutafuta wadhamini. Watu wanadai kuwa Lowassa anakusanya umati ili 'kuitisha' CC kuwa yeye anakubalika zaidi na hivyo hazuiliki kupitishwa kuwa mgombea wa CCM. Anaitisha CC? Really?" alisema Mumbe huyo wa CC huku akicheka.
"Wakati mwingine mbwembwe huponza. Wanatakiwa wadhamini 450 kila mkoa katika mikoa 15,kati ya hiyo 3 iwe ya Zanzibar. Hiyo niyo kanuni. Sasa watu 20,000 mkoa mmoja nwa kazi gani? Huku ni kupoteza muda na rasilimali. Sitta na Dr. Bilal ni mifano mizuri, wametafuta wadhamini na kukamilisha bila maonesho yasiyo na msingi. Mambo kama ya Lowassa asubiri wakati wa kampeni akipitishwa kugombea,si sasa" aliongeza kigogo huyo ambaye hakutangaza nia.
Mzee Tupatupa wa Lumumba Dar es Salaam
Wengine tulipitwa na hizi habari, ebu dadavua kidogo ilikuwaje? sasa anaitwa nani? Dunia in vitu hii!Wewe Mtoto wa Malecella Lowassa sio kama Baba yako aliyebadili dini ili apate uraisi!!!. Alafu ninawacwac huyu kigogo labda ni Mama yako wa Kambo-Anna au ni Mzeee nini weka bayana Dogo
Atapata, ebu piga hizi hesabu: Wake 4, kila mmoja watoto 3 jumla 12, Tayari kumi wanafika.uspate shida na wewe kajaribu kutafuta saini kwa style hiyohiyo kama utapata hata watu 10
Kanuni za CCM ni wadhamini 450 mikoa 15 tu ukizidisha hiyo ni tiketi ya kukatwa jina lako.Kwa mujibu wa kanuni zetu jina la Lowasssa halitajadiliwa kabisa kamati ya maadili inajindaa kukata majina yafuatayo.
1. Edward Lowassa Ngoyai Ndossy - Kaanza kampeni mapema kabla ya kipenga kupulizwa,Kashfa ya RICHMOD & Rushwa
2. Makongoro Nyerere - Aliwahi kujiunga na chama cha upinzani NCCR Mageuzi,kushambulia washandani wake.
3. Stephen Wasira - Aliwhi kujiunga na chama cha upinzani NCCR Mageuzi
4. Lazaro Nyalandu - Kashindwa kuzuia mauaji ya Tembo,hana uzoefu wa siasa za kimataifa.
5. Bi Malecela - Hana uzoefu na siasa za kimataifa & Anategemea zaidi jina la Baba yake badala ya kujiuza yeye mwenyewe
6. Mwigulu Nchemba - Bado mchanga sana hajakomaa,jazba.
7. January Makamba - Anategemea jina la Baba,bado mchanga sana kuongoza nchi kubwa kama Tanzania.
Nitaongeza wengine ambao hawatajadiliwa na kamati kuu majina yao yatachujwa na kamati ya Mzee Mangula.[/QUOTHapo namba 6 Mwigulu hawezi kujadiliwa kwa sababu
1.Alianza kampeni mapema kwa kutumia chopa akitumia vibaya wadhifa wake wa Naibu Katibu Mkuu na kupelekea kupigwa stop na Kinana.
2.Kwa kuwa CCM inataka pia kura za wapinzani haitaweza kumteua Mwigulu kutokana na vitendo vyake vya kigaidi dhidi ya wapinzani hasa CHADEMA kwa kulipua Bomu kwenye mkutano WA chadema huko Arusha,mauaji ya makada WA CHADEMA Igunga na USA River na kuwabambikizia kesi viongozi WA CHADEMA.Inasemekana vitendo hivi havikuwa na haraka za CCM Bali alijiamulia mwenyewe.
3.Anawadharau vijana WA CCM na kuwaona masalia waliofukuzwa kutoka CHADEMA ni bora zaidi.
Yaani ukitaka kuuza gazeti, au thread yako ichangiwe sana mitandaoni, ANZA NA LOWASSA...ndio utajua huyo bwana anapendwa sana...Sisikii mti yeyote...jamaa kwa sasa ndio muda wake...!!!
Kanuni za CCM ni wadhamini 450 mikoa 15 tu ukizidisha hiyo ni tiketi ya kukatwa jina lako.Kwa mujibu wa kanuni zetu jina la Lowasssa halitajadiliwa kabisa kamati ya maadili inajindaa kukata majina yafuatayo.
1. Edward Lowassa Ngoyai Ndossy - Kaanza kampeni mapema kabla ya kipenga kupulizwa,Kashfa ya RICHMOD & Rushwa
2. Makongoro Nyerere - Aliwahi kujiunga na chama cha upinzani NCCR Mageuzi,kushambulia washandani wake.
3. Stephen Wasira - Aliwhi kujiunga na chama cha upinzani NCCR Mageuzi
4. Lazaro Nyalandu - Kashindwa kuzuia mauaji ya Tembo,hana uzoefu wa siasa za kimataifa.
5. Bi Malecela - Hana uzoefu na siasa za kimataifa & Anategemea zaidi jina la Baba yake badala ya kujiuza yeye mwenyewe
6. Mwigulu Nchemba - Bado mchanga sana hajakomaa,jazba.
7. January Makamba - Anategemea jina la Baba,bado mchanga sana kuongoza nchi kubwa kama Tanzania.
Nitaongeza wengine ambao hawatajadiliwa na kamati kuu majina yao yatachujwa na kamati ya Mzee Mangula.
Mr Ngogo naona unaota ndoto za mchana, hapo juu majina uliyotaja si yote yatakayokatwa, tulia uone shughuli
mmeilea hii kansa , sasa inawatafuna. haitibiki tena. hakuna wa kumzuiani wala kukata jina lake. bora mjiunge naye tu, maana mmeshindwa kumng'oa.