Kigogo wa CCM: Lowassa anafanya kampeni

Kigogo wa CCM: Lowassa anafanya kampeni

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Posts
6,140
Reaction score
18,004
Kigogo mmoja wa CCM ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM amesema kuwa mtangaza nia Edward Lowassa anapiga kampeni badala ya kutafuta wadhamini. Mjumbe huyo wa CC amenidokeza kuwa jambo hilo litamkwamisha vya kutosha Lowassa katika kujaribu kupenya katika mchujo wa kuelekea kupigiwa kura na Mkutano Mkuu.

"Unajua ndugu yangu, Lowassa anajiharibia mwenyewe. Kitendo cha kuandaa watu kwa maelfu na kuzungumza nao ni kampeni na si kutafuta wadhamini. Watu wanadai kuwa Lowassa anakusanya umati ili 'kuitisha' CC kuwa yeye anakubalika zaidi na hivyo hazuiliki kupitishwa kuwa mgombea wa CCM. Anaitisha CC? Really?" alisema Mumbe huyo wa CC huku akicheka.

"Wakati mwingine mbwembwe huponza. Wanatakiwa wadhamini 450 kila mkoa katika mikoa 15,kati ya hiyo 3 iwe ya Zanzibar. Hiyo niyo kanuni. Sasa watu 20,000 mkoa mmoja nwa kazi gani? Huku ni kupoteza muda na rasilimali. Sitta na Dr. Bilal ni mifano mizuri, wametafuta wadhamini na kukamilisha bila maonesho yasiyo na msingi. Mambo kama ya Lowassa asubiri wakati wa kampeni akipitishwa kugombea,si sasa" aliongeza kigogo huyo ambaye hakutangaza nia.

Mzee Tupatupa wa Lumumba Dar es Salaam
 
Muacheni Lowassa nyie waswahili,siasa ni popularity nyie waswahili.Lowassa njoo chadema wakikuwekea vikwanzo sharti ni moja tu.Kama haukuwa richmond basi alikuwa nani?.kutafuta wadhamini ni campaign vile vile.....si lazima uwaridhishe na waridhike....mnataka awe bubu,au wananchi wasiende kuona?.Nyie chukueni hao 450 na baki ni kuwa amefaulu vizuri sana.....katika siasa pia kuna kufaulu na kufaulu vizuri sana
 
Mbona na wengine wanawakusanya na hamuwasemi?, ccm mtauana kwa wivu mwaka huu
 
Wewe Mtoto wa Malecella Lowassa sio kama Baba yako aliyebadili dini ili apate uraisi!!!. Alafu ninawacwac huyu kigogo labda ni Mama yako wa Kambo-Anna au ni Mzeee nini weka bayana Dogo
 
Hana mahali pa kusemea? hapa tutamsaidia nn? alshasema uwez zuia mafuriko kwa mikono
 
Sijui wanachelewesha nn kulimwaga hilo gamba na jambazi sugu!!!!!!
 
Kipi ambacho siyo kampeni? Tafasiri ya neno "kampeni" ni ipi? Je, ni Mkusanyiko?, au kuhutubia, au vyote, au maneno yanayotamkwa na mhusika katika mkusanyiko huo wakati anahutubia?

Nani anayepima kuwa hii ni kampeni na ile siyo kampeni?

Tofauti ya lowassa na wenzake ni ipi?
 
Mzee Tupatupa mbona wote wanafanya ayafanyayo Lowassa..............Mwaka huu kuna watu wakufa kwa kihoro.

Siyo team Lowassa lakini naona CCM mnavurugana tu.Any way ndiyo nachukua jembe nikasafishe shamba............

Safari hii likizo yangu itakuwa kusubiri mavuno pale Tume ya Mkude Simba itakapofika pande hii yetu
 
Jamaa yupo vizuri kwa kweli hebu angalia vyombo vya habari anavyopewa coverage kuliko hata ya RAIS. Mfano mazishi ya Mufti angalia anavyopewa kipaumbele akina Membe wapo lkn picha ni moja tu tena ambayo haikutoka vizuri yeye hata za kusindikizwa zipo! CCM ikivuka salama hapa itakuwa poa kabisa
 
Nakubaliana na mleta mada, ni kweli kabisa kule sio kuomba wadhamini ni kampeni
 
Kanuni za CCM ni wadhamini 450 mikoa 15 tu ukizidisha hiyo ni tiketi ya kukatwa jina lako.Kwa mujibu wa kanuni zetu jina la Lowasssa halitajadiliwa kabisa kamati ya maadili inajindaa kukata majina yafuatayo.

1. Edward Lowassa Ngoyai Ndossy - Kaanza kampeni mapema kabla ya kipenga kupulizwa,Kashfa ya RICHMOD & Rushwa

2. Makongoro Nyerere - Aliwahi kujiunga na chama cha upinzani NCCR Mageuzi,kushambulia washandani wake.

3. Stephen Wasira - Aliwhi kujiunga na chama cha upinzani NCCR Mageuzi

4. Lazaro Nyalandu - Kashindwa kuzuia mauaji ya Tembo,hana uzoefu wa siasa za kimataifa.

5. Bi Malecela - Hana uzoefu na siasa za kimataifa & Anategemea zaidi jina la Baba yake badala ya kujiuza yeye mwenyewe

6. Mwigulu Nchemba - Bado mchanga sana hajakomaa,jazba.

7. January Makamba - Anategemea jina la Baba,bado mchanga sana kuongoza nchi kubwa kama Tanzania.

Nitaongeza wengine ambao hawatajadiliwa na kamati kuu majina yao yatachujwa na kamati ya Mzee Mangula.
 
Back
Top Bottom