Kigogo wa CCM adaiwa kumnajisi mtoto wake

Kigogo wa CCM adaiwa kumnajisi mtoto wake

Wanaume bwana!! Mmmmmm!!! Sababu 1. alihisi/ na bado anaendelea kuhisi mtoto huyo si wake! Alafu km kulikuwa na mvutano baina yao ameamua kwa makusudi kufanya hivyo. ( mama itabidi afunguke vizuri)
2. sababu za kishirikina ( apnde cheo, apendwe na watu na wamteyemekee km Mh
Magufuli nk.. I can not swallow it. Ee Mungu Nakuomba ulinde malaika wako hata sisi wakubwa pia. Amina.
 
Kuna mambo mawili matatu yananitatiza hapa. 1: Kama hakuna kasiasa flan ndani, iweje muweze kukitaja Chama, Wilaya na mkoa mshindwe kumtaja muhusika? Mwandishi anaposema ati RPC ameomba ushirikiano ili amkamate, tumpelekee kila mwanamume anayetoka wilaya ya Mwanga?
2: Mna uhakika gani kuwa hakuna ugomvi ndani ya hiyo nyumba. Mama alisikia mtoto akililia chumba kingine. Hivi kweli, mwanamke gani ambaye ana mtoto wa mwaka 1, anayeweza kuwa tiyari kishaenda kumlaza chumba kingine hata ka ana mimba kuubwa tu. Nadhani huyu mama ndo wa kuchunguzwa zaidi kwani ndo mwenye tatizo. Hana malezi mema. Yaani ni kuku wa kisasa.
3. Kuhusu kutokamatwa, nadhani Polisi wameangalia mazingara wakaona uzushi ni mwingi kuliko uhalisia. Kumbukeni kile kisa cha mjini Moshi miaka ya nyuma kuhusu babu kumbaka mjukuu wa miezi 6. Kumbe ilikuwa mpango wa kumkimbiza nyumbani ili mama mdogo airidhi nyumba. Na kweli alifanikiwa.
Ni hayo machache ila sikatai kuwa kwa dunia la leo, yawezekana lakini Stage setting ya mchezo, waliruka hatua nyingi yaani wameacha maswali mengi kuliko
 
Ndio Tanzania kiongozi.
Wengi wamepelekwa Mwanza wakahakikishe kamanda Mawazo hazikwi.
Sijui wanataka wamle nyama?
aheri nyumbu wa malisho kuliko kua zombie. hata wanachopigania makamanda kwa sasa hawajui wanapelekeshwa tu na mbowe.
 
Wewe usimtaje jina, si unajua sheria za mitandao zitakuhusu enhee? Na sheria zipo kwa walio juu tu, ama hilo mnalisahau jamani? Yaweza kuwa ni Masuala ya kupanda cheo, labda kutoka kuwa naibu katibu na kuwa m/nykiti wa eneo alilohamishiwa wa chama chake. Angetuhumiwa kubaka mlalahoi yeyote jina tungetajiwa tu, maana sheria za mitandao nahisi hazigusi wa chini, ama haziwaangalii wa chini.

NOTE:
Mjiandae kusikia baada ya ushahidi kukamilika, Daktari kageuza matokeo, na hapa tumeona Daktari kakiri mtoto kubakwa, ama mama mtoto kanyamazishwa na pesa, yanatokea sana haya jamani, tusubirie muone.

Nimeumia sana kama mzazi.

Ahsante!
 
PENGINE YAWEZA KUWA NI MIGOGORO kwenye ndoa mwisho wa siku wanataka kukomoana

Kukomoana gani huko?Huyo mtoto anahusika vipi kwenye migogoro yao?Anyongwe tu mana hakuna namna
 
Mimi ni mwana ccm damu,lakini kwenye hili naviomba vyombo vya dola vimkamate huyo firauni haraka sana.
 
Kigogo mmoja wa CCM wilayani Rombo anadaiwa kumnajisi mtoto wake mwenye umri wa mwaka mmoja.

"Ni kweli tukio hilo nimelisikia na utaratibu unaendelea ili akamatwe na kutoa maelezo dhidi ya tuhuma zinazomkabili. Pia, kama kuna mtu anajua alipo, atusaidie ili tuweze kumkamata na kumfikisha mahakamani," alisema Kamanda Ngonyani:

"Tunawaomba wananchi mtusaidie katika hili, kitendo alichokifanya huyu baba si cha kufumbiwa macho, lazima atafutwe na akamatwe."
kubakwa, kulawitiwa, kunajisiwa kwa watoto siyo issue kwa polisi. Ingekuwa ni kuzuia mikutano ya UKAWA mpaka sasa ungekuta hata mfurukutwa wa ukawa yupo ndani
 
Police watatoka wapi wa kumkamata huyo shetani? Wako busy mwanza wanalinda mochwari bugando, office za cdm na pale mahakama kuu, labda wamkamate mgambo
 
Kwanini hatajwi jina?
Sasa Mwandishi na kamanda wa Polisi wanasema wanaomba msaada wa kumpata halafu hawasemi jina lake, sisi wananchi tutamjuaje?
 
Kigogo mmoja wa CCM wilayani Rombo anadaiwa kumnajisi mtoto wake mwenye umri wa mwaka mmoja.

Mama mzazi wa mtoto huyo alidai kuwa tukio hilo lilitokea Novemba 17, usiku nyumbani kwao Mwanga walipokuwa wamelala na alishtuka baada ya kusikia sauti ya mtoto akilia kutokea chumba kingine.

"Nilipoamka nilikwenda kwenye kile chumba na kumkuta mwanangu akitokwa na damu sehemu zake za siri, nilimchukua na kumpeleka Kituo cha Afya cha Mwanga," alidai mama huyo.

Alidai kuwa daktari aliyemtibu alithibitisha kuwa alikuwa amenajisiwa.

Hata hivyo, alisema baada ya mumewe kufanya kitendo hicho, aliondoka na kwenda kwenye kituo chake cha kazi alichohamishiwa hivi karibuni cha wilayani Rombo.

"Daktari alipompima na kukuta kalawitiwa alimtibu na kumpa dawa za maumivu na kuniambia nikatoe taarifa polisi ili mume wangu akamatwe, lakini hadi sasa hajakamatwa," alidai na kuongeza:

"Tangu amefanya kitendo hiki hajawasiliana na mimi na tayari nilishafungua jalada polisi. Nadhani alidhamiria kufanya kitendo hiki, amemuumiza mtoto," alidai mama huyo.

Hata hivyo, Kamanda wa Polisi mkoani Kilimanjaro, Flugence Ngonyani alisema mtuhumiwa bado anatafutwa na polisi kisha afunguliwe mashtaka ya ubakaji.

"Ni kweli tukio hilo nimelisikia na utaratibu unaendelea ili akamatwe na kutoa maelezo dhidi ya tuhuma zinazomkabili. Pia, kama kuna mtu anajua alipo, atusaidie ili tuweze kumkamata na kumfikisha mahakamani," alisema Kamanda Ngonyani:

"Tunawaomba wananchi mtusaidie katika hili, kitendo alichokifanya huyu baba si cha kufumbiwa macho, lazima atafutwe na akamatwe."

Nashindwa kuamini kwa sababu zifuatazo:
1. Kesi iko polisi hata jina la mtuhumiwa halitajwi. Halafu Kamanda wa Polisi anatoa wito wa wananchi kuisaidia polisi kumkamata mtuhumiwa. Au jina limefichwa kwa sababu za kuhifadhi utu wa mtoto??
2. Mtoto mwenye umri wa mwaka mmoja analala chumba tofauti na mama yake?? Au baba huyo alimbeba wakati mama kalala na kumpeleka chumba kingine.
 
Siku hizi wachagga wanachangamkia tenda ya nguvu za giza (uchawi) ili wapate njia za mkato. Huyu akamatwe na akatwe dushelele lake ili liwe fundisho kwa wachagga wengine.
 
mwenye picha yake haiweke hapa JF, jamii iweze kulisaidia jeshi la polisi ....
 
hahaha kigogo mmoja serikalini?? kigogo mmoja serikalini.

inamaana jina lake linafichwa kwa manufaa ya nani hasa? huu ni uzuzu na ujinga kamwaga ugari wanao mfaham wabidue bakuri ya mboga .haiwezekani afichwe fichwe na kazini aendelee kwenda wakati kafanya ufedhuri wake huku
 
Nashindwa kuamini kwa sababu zifuatazo:
1. Kesi iko polisi hata jina la mtuhumiwa halitajwi. Halafu Kamanda wa Polisi anatoa wito wa wananchi kuisaidia polisi kumkamata mtuhumiwa. Au jina limefichwa kwa sababu za kuhifadhi utu wa mtoto??
2. Mtoto mwenye umri wa mwaka mmoja analala chumba tofauti na mama yake?? Au baba huyo alimbeba wakati mama kalala na kumpeleka chumba kingine.

Swali lako la pili hata mm linaniumiza kichwa!!!
 
huyu hana kosa kabisa,wale wanaota kwenda mazikonj wanamakosa makali sana!
 
Back
Top Bottom