Kigogo wa CCM adaiwa kumnajisi mtoto wake

Paul Alex

JF-Expert Member
Joined
Jul 14, 2012
Posts
4,346
Reaction score
9,846
Kigogo mmoja wa CCM wilayani Rombo anadaiwa kumnajisi mtoto wake mwenye umri wa mwaka mmoja.

Mama mzazi wa mtoto huyo alidai kuwa tukio hilo lilitokea Novemba 17, usiku nyumbani kwao Mwanga walipokuwa wamelala na alishtuka baada ya kusikia sauti ya mtoto akilia kutokea chumba kingine.

"Nilipoamka nilikwenda kwenye kile chumba na kumkuta mwanangu akitokwa na damu sehemu zake za siri, nilimchukua na kumpeleka Kituo cha Afya cha Mwanga," alidai mama huyo.

Alidai kuwa daktari aliyemtibu alithibitisha kuwa alikuwa amenajisiwa.

Hata hivyo, alisema baada ya mumewe kufanya kitendo hicho, aliondoka na kwenda kwenye kituo chake cha kazi alichohamishiwa hivi karibuni cha wilayani Rombo.

"Daktari alipompima na kukuta kalawitiwa alimtibu na kumpa dawa za maumivu na kuniambia nikatoe taarifa polisi ili mume wangu akamatwe, lakini hadi sasa hajakamatwa," alidai na kuongeza:

"Tangu amefanya kitendo hiki hajawasiliana na mimi na tayari nilishafungua jalada polisi. Nadhani alidhamiria kufanya kitendo hiki, amemuumiza mtoto," alidai mama huyo.

Hata hivyo, Kamanda wa Polisi mkoani Kilimanjaro, Flugence Ngonyani alisema mtuhumiwa bado anatafutwa na polisi kisha afunguliwe mashtaka ya ubakaji.

"Ni kweli tukio hilo nimelisikia na utaratibu unaendelea ili akamatwe na kutoa maelezo dhidi ya tuhuma zinazomkabili. Pia, kama kuna mtu anajua alipo, atusaidie ili tuweze kumkamata na kumfikisha mahakamani," alisema Kamanda Ngonyani:

"Tunawaomba wananchi mtusaidie katika hili, kitendo alichokifanya huyu baba si cha kufumbiwa macho, lazima atafutwe na akamatwe."
 
Kweli ya shikitisha yani na Jamaa nasikia yupo kazini Mkuu nimeskia kwenye radio Leo asubuhi.
 
imani za kishirikina znachochea mambo haya.

akamatwe na sheria ichukue maamuzi (kama ni kweli).
 
Kweli ya shikitisha yani na Jamaa nasikia yupo kazini Mkuu nimeskia kwenye radio Leo asubuhi.

Ndio Tanzania kiongozi.
Wengi wamepelekwa Mwanza wakahakikishe kamanda Mawazo hazikwi.
Sijui wanataka wamle nyama?
 
Mkiambiwa yale ya babu seya hamuamini!!! ila hili mmelishupalia na huoni mtu akijiuliza inawezekana kweli mwanao wa kumzaa tena mwaka mmoja??? imani potofu ukiziamini basi utafanya lolote alisemalo mganga!!!
 
Hii ni zaidi ya hatari mtoto wa mwaka mmoja so sad
 
Na kweli ni kigogo, make hata kutajwa tu jina lake nchi itatikisika.
 
Mungu wangu mtoto wa mwaka mmoja huyu jamaa afungwe maisha muuaji
 
mtoto wa kike????
Mhhh..huyu baba noma,kaamua kula vyake mapeema
 
Dah! Hii taarifa imenifanya nihisi maumivu makali aseee mimi kama mama uyu kigogo wakunyongwa tu mana hakuna namna sasa laana za mungu zimshukie
 
Kigogo mmoja wa CCM wilayani Rombo anadaiwa kumnajisi mtoto wake mwenye umri wa mwaka mmoja.

Mama mzazi wa mtoto huyo alidai kuwa tukio hilo lilitokea Novemba 17, usiku nyumbani kwao Mwanga walipokuwa wamelala na alishtuka baada ya kusikia sauti ya mtoto akilia kutokea chumba kingine.

"Nilipoamka nilikwenda kwenye kile chumba na kumkuta mwanangu akitokwa na damu sehemu zake za siri, nilimchukua na kumpeleka Kituo cha Afya cha Mwanga," alidai mama huyo.

Alidai kuwa daktari aliyemtibu alithibitisha kuwa alikuwa amenajisiwa.

Hata hivyo, alisema baada ya mumewe kufanya kitendo hicho, aliondoka na kwenda kwenye kituo chake cha kazi alichohamishiwa hivi karibuni cha wilayani Rombo.

"Daktari alipompima na kukuta kalawitiwa alimtibu na kumpa dawa za maumivu na kuniambia nikatoe taarifa polisi ili mume wangu akamatwe, lakini hadi sasa hajakamatwa," alidai na kuongeza:

"Tangu amefanya kitendo hiki hajawasiliana na mimi na tayari nilishafungua jalada polisi. Nadhani alidhamiria kufanya kitendo hiki, amemuumiza mtoto," alidai mama huyo.

Hata hivyo, Kamanda wa Polisi mkoani Kilimanjaro, Flugence Ngonyani alisema mtuhumiwa bado anatafutwa na polisi kisha afunguliwe mashtaka ya ubakaji.

"Ni kweli tukio hilo nimelisikia na utaratibu unaendelea ili akamatwe na kutoa maelezo dhidi ya tuhuma zinazomkabili. Pia, kama kuna mtu anajua alipo, atusaidie ili tuweze kumkamata na kumfikisha mahakamani," alisema Kamanda Ngonyani:

"Tunawaomba wananchi mtusaidie katika hili, kitendo alichokifanya huyu baba si cha kufumbiwa macho, lazima atafutwe na akamatwe."

Kwa nini asitajwe jina?? Mbona watuhumiwa wengine wanatajwa majina??? Mwenye jina la huyo pimbi atuwekee hapa
.Jaribuni kutafuta jina la kigogo aliyehamia Rombo recently then mlipueni hapa bila fear wala favour
 
PENGINE YAWEZA KUWA NI MIGOGORO kwenye ndoa mwisho wa siku wanataka kukomoana
Kigogo mmoja wa CCM wilayani Rombo anadaiwa kumnajisi mtoto wake mwenye umri wa mwaka mmoja.

Mama mzazi wa mtoto huyo alidai kuwa tukio hilo lilitokea Novemba 17, usiku nyumbani kwao Mwanga walipokuwa wamelala na alishtuka baada ya kusikia sauti ya mtoto akilia kutokea chumba kingine.

"Nilipoamka nilikwenda kwenye kile chumba na kumkuta mwanangu akitokwa na damu sehemu zake za siri, nilimchukua na kumpeleka Kituo cha Afya cha Mwanga," alidai mama huyo.

Alidai kuwa daktari aliyemtibu alithibitisha kuwa alikuwa amenajisiwa.

Hata hivyo, alisema baada ya mumewe kufanya kitendo hicho, aliondoka na kwenda kwenye kituo chake cha kazi alichohamishiwa hivi karibuni cha wilayani Rombo.

"Daktari alipompima na kukuta kalawitiwa alimtibu na kumpa dawa za maumivu na kuniambia nikatoe taarifa polisi ili mume wangu akamatwe, lakini hadi sasa hajakamatwa," alidai na kuongeza:

"Tangu amefanya kitendo hiki hajawasiliana na mimi na tayari nilishafungua jalada polisi. Nadhani alidhamiria kufanya kitendo hiki, amemuumiza mtoto," alidai mama huyo.

Hata hivyo, Kamanda wa Polisi mkoani Kilimanjaro, Flugence Ngonyani alisema mtuhumiwa bado anatafutwa na polisi kisha afunguliwe mashtaka ya ubakaji.

"Ni kweli tukio hilo nimelisikia na utaratibu unaendelea ili akamatwe na kutoa maelezo dhidi ya tuhuma zinazomkabili. Pia, kama kuna mtu anajua alipo, atusaidie ili tuweze kumkamata na kumfikisha mahakamani," alisema Kamanda Ngonyani:

"Tunawaomba wananchi mtusaidie katika hili, kitendo alichokifanya huyu baba si cha kufumbiwa macho, lazima atafutwe na akamatwe."
 
Pole sana mtoto. Huyo baba kweli ni baba mzazi!!?? Asee Mungu atamuadhibu.
 
Back
Top Bottom