Kigogo wa CCM adaiwa kumnajisi mtoto wake

Kigogo wa CCM adaiwa kumnajisi mtoto wake

Duuuh leo ni siku ya habari za kifirauni tu.
Huku baba kamlawiti mwanae,kule kijana wa Kitz kaolewa na mzungu.

Luna mda hata naogopa kufungua mitandao ya kijaamii unjiuliza tz kuna tatzo gn mara maiti imekuwa dili kuliko waliomuua
 
Kigogo mmoja wa CCM wilayani Rombo anadaiwa kumnajisi mtoto wake mwenye umri wa mwaka mmoja.

Mama mzazi wa mtoto huyo alidai kuwa tukio hilo lilitokea Novemba 17, usiku nyumbani kwao Mwanga walipokuwa wamelala na alishtuka baada ya kusikia sauti ya mtoto akilia kutokea chumba kingine.

"Nilipoamka nilikwenda kwenye kile chumba na kumkuta mwanangu akitokwa na damu sehemu zake za siri, nilimchukua na kumpeleka Kituo cha Afya cha Mwanga," alidai mama huyo.

Alidai kuwa daktari aliyemtibu alithibitisha kuwa alikuwa amenajisiwa.

Hata hivyo, alisema baada ya mumewe kufanya kitendo hicho, aliondoka na kwenda kwenye kituo chake cha kazi alichohamishiwa hivi karibuni cha wilayani Rombo.

"Daktari alipompima na kukuta kalawitiwa alimtibu na kumpa dawa za maumivu na kuniambia nikatoe taarifa polisi ili mume wangu akamatwe, lakini hadi sasa hajakamatwa," alidai na kuongeza:

"Tangu amefanya kitendo hiki hajawasiliana na mimi na tayari nilishafungua jalada polisi. Nadhani alidhamiria kufanya kitendo hiki, amemuumiza mtoto," alidai mama huyo.

Hata hivyo, Kamanda wa Polisi mkoani Kilimanjaro, Flugence Ngonyani alisema mtuhumiwa bado anatafutwa na polisi kisha afunguliwe mashtaka ya ubakaji.

"Ni kweli tukio hilo nimelisikia na utaratibu unaendelea ili akamatwe na kutoa maelezo dhidi ya tuhuma zinazomkabili. Pia, kama kuna mtu anajua alipo, atusaidie ili tuweze kumkamata na kumfikisha mahakamani," alisema Kamanda Ngonyani:

"Tunawaomba wananchi mtusaidie katika hili, kitendo alichokifanya huyu baba si cha kufumbiwa macho, lazima atafutwe na akamatwe."
Nilijuatu utakuwa chaga
 
Nikisoma habari hiyo katikati ya mistari naona kuna mgogoro wa ndoa ambao ndio umefikia kutokea kwa tukio hilo.

Kitendo cha mtoto mdogo wa mwaka mmoja kulala mbali na mama yake kunaweza kuleta hisia za kuwepo tofauti kuhusiana na mtoto huyo. Inawezekana huyo kigogo anaona huyo mtoto sio wake, hivyo kuamua kwamba asilale chumbani kwake kama hatua ya kumkomesha mkewe, na hatua ya yeye kumnajisi huyo mtoto ni muendelezo wa kumkomesha mkewe.

Hayo mambo ya ushirikina yanaweza kuhusika ila bado hakuondoi uwezekano wa kwamba wazazi wa huyo mtoto wana migogoro. Ni vigumu kwa mzazi kumfanyia hivyo mtoto wake japo inawezekana, lakini kutegemeana na historia ya mhusika.
 
Hivi hawa watu wa rombo wana matizo ganii kila kukicha habarii mbaya haziishii....
 
watu wanalinda nafasi kwa ushirikina. Polisi wamfuate huku mkuu rombo alikohamishiwa.waache kuzuga eti wanamtafuta!
 
Dah! Hii taarifa imenifanya nihisi maumivu makali aseee mimi kama mama uyu kigogo wakunyongwa tu mana hakuna namna sasa laana za mungu zimshukie
Mkuu nahisi umesahau usemi kuwa "the law govern the poor, the rich rule the law".
 
Back
Top Bottom