Kigogo wa Bakwata kufikishwa mahakamani leo

Sumasuma

JF-Expert Member
Jun 23, 2011
342
110
Frederick Katulanda, Mwanza
TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (Takukuru) Mkoa wa Mwanza, leo inatarajia kumpandisha kizimbani kigogo wa Baraza la Waislamu Tanzania (Bakwata) mkoani Mwanza, kwa kosa la kuhujumu uchumi.

Habari zilizopatikana na kuthibitishwa na Kamanda wa Takukuru Mkoa wa Mwanza, Christopher Mariba, zimedai kuwa kufikishwa mahakamani kwa Kigogo huyo, kunatokana kutumia msamaha wa kodi wa Serikali kununua saruji kwa niaba ya wafanyabiashara kwa jina la Bakwata, hivyo kukwepa kodi zaidi ya Sh15 milioni kila mwezi mmoja.

Imeelezwa kufikishwa mahakamani kwa kigogo huyo kunatokana na hujuma hizo kuanza kufichuliwa na Gazeti la Mwananchi Jumapili, baada ya kutolewa mara ya kwanza Januari 25, 2009 Takukuru walifanya uchunguzi wao na kubaini kuwa kulikuwa na ukweli.

“Uchunguzi wetu umekamilika, kama Mungu akijalia kesho (leo) tutamfikisha mahakamani, sasa naomba mfike wenyewe mahakamani maana siwezi kuongea sana juu ya masuala haya,” alisema Mariba.

Pia, katika habari iliyoandikwa na Mwananchi Jumapili zilieleza katibu huyo akiwa na dhamana ya kuongoza Bakwata, alishirikiana na wafanyabiashara wa Mwanza kutumia jina la Bakwata kununua tani za saruji 2,298 kwa Sh31,589,34.

Kipindi cha wiki mbili wanadaiwa walinunua saruji kwa bei ya Sh16,500 kila mfuko, kisha kuiuza kwa bei ya Sh19,000 yenye kodi sawa na Sh43,651,913, hivyo kujinufaisha binafsi na kuikosesha Serikali mapato.

Ilielezwa kuwa kiasi hicho cha fedha kiliwekwa katika akaunti namba 015101004917 iliyopo tawi la NBC Mwanza kabla ya kuingizwa kwenye akaunti hiyo ilikuwa na salio la Sh474,045.45, lakini baada ya kuingia fedha hizo zilitolewa kwa vipindi tofauti zikionyesha kwenda kwa Cement Distributor kulipia ununuzi wa saruji.

Kulingana na kumbukumbu ya nyaraka mbalimbali kutoka ofisi ya Bakwata mkoani Mwanza ambazo gazeti hili imebahatika kuziona, Januari 3, mwaka huu akaunti hiyo ikiwa salio la Sh474,045.45, ilionyesha kupokea Sh8,680,000 na kiasi hicho kutolewa siku hiyo kwenda kwa Cement Distributor.

Kiasi kingine cha Sh11,085,163,00 kiliingia katika akaunti hiyo Januari 9, mwaka huu lakini pia kilitolewa siku hiyo pia kikielekea kununua saruji.

Fedha nyingine Sh11,824,176 ilingia katika akaunti hiyo na kutolewa siku hiyo, hivyo kuifanya akaunti hiyo katika wiki mbili kupokea Sh31,590,200 na kiasi hicho kutolewa na kuifanya akaunti hiyo kubakiwa na salio la Sh474,045.45.

Kesi hii itakuwa ya kwanza ya aina yake kwa viongozi wa dini kufikishwa mahakamani wakikabiliwa na tuhuma za kusababisha Serikali kukosa mapato.:A S 465:
 
Sasa nimejuwa kwanini BAKWATA haiwezi kujenga ma-shule wala ma-hospitali!!
 
anaonewa kwa kuwa amekataa kutoa rushwa.huyu jamaa namfaham anamsimamo sana.zengwe tu hili.
 
kwa hali hii mtu kama huyu akipewa jukumu la kusaini MoU na CCM itakuaje? Jamani viongozi wa dini tuwe na hofu ya Mungu, ingawa mnafanya uovu huu kwa siri lakini Mungu anaona kila kitu....
Haki itendeke kwa huyo Kigogo wa BAKWATA na watuhumiwa wengine
 
ha ha ha.. wanikumbusha mzee wa upako alitaka kuingiza tairi mia nne za magari hapa.. ati za kanisa.. dili likastukiwa.. hii misamaha ya kodi inakuwa abused na viongozi wa dini wenye uchu na uroho wa mali za dunia.. huku waki2danganya sie ati 2ciwekeze hapa duniani..
 
tunawajua wachungaji na maaskofu ni wauza madawa la kulevya.ndio maana wanajenga ma shule na ma hospitali.
shule zote na mahospital yanajengwa kwa fedha za wahumini ndo mana wanasema wakristu michango imezidi makanisani na pia fedha za wahisani zinasaidia kujenga pia hzo shule na watoto wenu tunawapokea na kuwapa elimu nzuri na malezi bora mashuleni, na bila kusahau hospitalini tunawahudumia na kuwapa tiba bora. uza na wewe madawa ya kulevya ukajenge hizo shule na hospital kama unaona wanafaidi.
 
Bila kuwasahau wale viongozi wa dini wanaouza madawa ya kulevya nao wafikishwe mahakamani kwani ata jk alidai anawafahamu, kulikoni numwone huyu tu huku hawa wengine wakiendelea kudunda mitaani?
kaka hata huyu akukamatwa tu na kufikishwa mahakamani bali uchunguzi ulifanyika kwanza so ukute wanafanya uchunguzi ndo wawapeleke hao watu mahakamani.
 
Bila kuwasahau wale viongozi wa dini wanaouza madawa ya kulevya nao wafikishwe mahakamani kwani ata jk alidai anawafahamu, kulikoni numwone huyu tu huku hawa wengine wakiendelea kudunda mitaani?
Kamwambie JK apeleke ushahidi wake kwenye kikosi kinachozuia madawa ya kulevya, kwa vile umesema anawafahamu, ili nao wafikishwe Mahakamani.
 
Mtu kama una ushahidi kuwa hizo fedha zilizokuwa zikiingizwa na kutolewa fasta fasta kwenye akaunti yake zilikuwa ni zake, si uende ukawe shahidi wake wa utetezi Mahakamani? Manake pengine huyo mtu anafanya biashara ya simenti siku nyingi japokuwa akaunti yake ilikuwa na salio lisilozidi laki 5 kwa muda mrefu. Halafu watu wengine wanasema eti kakamatwa kwakuwa ana msimamo mkali na eti alikataa kutoa rushwa, sasa rushwa aitoe kwa nani wakati yeye ndo playmaker?
 
shule zote na mahospital yanajengwa kwa fedha za wahumini ndo mana wanasema wakristu michango imezidi makanisani na pia fedha za wahisani zinasaidia kujenga pia hzo shule na watoto wenu tunawapokea na kuwapa elimu nzuri na malezi bora mashuleni, na bila kusahau hospitalini tunawahudumia na kuwapa tiba bora. uza na wewe madawa ya kulevya ukajenge hizo shule na hospital kama unaona wanafaidi.

MHHH kwa mwendo huu tanzania bila udini itawezekana kweli???maana naona mrembo umekomaa na unaonyesha jinsi gani ulivyo mdini,hapa dini ya mtu hatuangalii kama sheikh kama ustadh kama baba paroko atajua mwenyewe kama kavunja sheria na ashughulikiwe tu tena kikamilifu..
 
Back
Top Bottom