Informer
Platinum Member
- Jul 29, 2006
- 1,604
- 6,698
MKURUGENZI wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Fadhili Manongi amedaiwa kungangania ofisi, licha ya kukabidhiwa barua ya kustaafu kwa mujibu wa sheria
Taarifa za uhakika ambazo gazeti hili imezipata zinasema kwamba tayari Manongi ana barua ya kustaafu tangu Machi 31, mwaka huu lakini ameendelea kuwamo ofisini.
Akiwa ndani ya ofisi hiyo, Manongi kwa sasa anaratibu safari za kiofisi ambako kwa wiki hii alikuwa Mtwara kabla ya kwenda Gaborone, Botswana. Taarifa zinasema kwamba Gabarone anakwenda kushiriki mkutano wa Wakurugenzi wa Usafiri wa Anga kwa nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo kwa nchi za Kusini mwa Afrika.
Huyu mtu amestaafu, hata kwenye bodi aliulizwa na akajibu atafutwe Katibu Mkuu, Katibu Mkuu akajibu kuwa wamempa barua ya kustaafu na kwamba hana budi kukabidhi ofisi, lakini hajafanya hivyo, alisema mtoa habari.
Gazeti hili lilimtafuta Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dk. Shaaban Mwinjaka bila mafanikio kwa siku za Jumatatu hadi Jumatano mpaka gazeti hili linakwenda mitamboni.
Lakini lilimpa nafasi Manongi kuzungumzia uwepo wake ofisini ilihali ana barua ya kustaafu mkononi ambako alisema, Uwepo wangu ofisini unajulikana kwa wakubwa, muulize Waziri au Katibu Mkuu.