Kigoda cha Mwalimu: Prof. Shivji vs Mkapa

mkapa ana akili kuliko hata shivji na kamata(na siasa zao za ujamaa).yeye anatoa reasoning wabongo mtalalamika kumbe hata hamjasoma vision 2025.duh hii kali naanza kuona chadema inanguvu sana kwasababu ya ******
 
hatutapata best prezident kama mkapa tena except mwl nyerere ambaye hana wa kumfananisha naye jaman,WE LOVE YOU Mkapa
 
Hivi ni suala la kulinganisha Mkapa na wengine au kuangalia nini hasa alichofanya kiutendaji kilichotuwekea misingi mizuri ya uchumi na utawala? Hapa naona ni yale ya kwenye nchi ya vipofu, mwenye chongo ni mfalme! Kuongea sana si hoja. Mtu yeyote mwenye akili iliyounganika anaweza kupanga hoja zake na kuwakosha wasio na hulka ya kujisomea na kudadisi. Hata Hitler aliwakosha wajerumani kwa mtindo huo kabla mauti hayajawafikia.

Mkapa anaweza kudai kuwa alikuwa anatuletea majawabu kwa matatizo ya utendaji mbovu kwenye sekta ya umma. Lakini tujiulize, kuileta Net Group Solution ndio ilikuwa dawa ya kuhakikisha ukusanyaji bora wa madeni ya TANESCO kama alivyowahi kudai? Je, si amri ya Ikulu kuhakikisha kuwa hakuna "taasisi nyeti" itakayoweza kukwepa hilo? Manake si hospitali, jeshi hata taasisi za Serikali zilizopona. Walipoondoka tu, ikawa kama kawaida.

Halafu unapobinafsisha viwanda kwa ajili tu ya kuondokana na uongozi mbovu hapo haujafanya kitu. Tena mbaya zaidi ni kule kuacha zoezi zima lifanywe bila uoni (vision) wala mkakati wa maana na kisha litawaliwe na rushwa/ubadhirifu mkubwa kiasi cha yeye mwenyewe kujifanya mwekezaji (akiwa Ikulu) na kujimilikisha rasilimali moja muhimu ya Taifa. Anasemaje kuhusu kuruhusu wizi katika manunuzi makubwa ya kitaifa kama rada na ndege ya Serikali? Kuhusu uuzaji wa nyumba za serikali kwa sababu za kibinafsi?

Ni kweli hakuna binadamu mkamilifu, lakini kuna makosa mengine huwa si ya kawaida; yanadhamiria kuharibu misingi muhimu ya uchumi na mshikamano wa kitaifa. Wachina sio wajinga wanapohukumu kifo kwa makosa ya rushwa na uhujumu uchumi. Wanaelewa vizuri kwamba makosa ya aina hiyo ni ya msingi (fundamental) na huishia kubomoa nchi. Na hapo huwezi kuleta habari ya kulinganisha na "mazuri" au na "fulani". Badala ya kuleta jeuri, Mkapa anatakiwa kutambua kwamba yeye ni muendelezo wa utawala wa CCM unaozidi kuliangamiza taifa hili na asitegemee kwamba wananchi watamuona tofauti na vilaza wengine waliomo humo. Atafute namna nyingine ya kutoka; si hivyo!
 
hata mm namkubali sana mkapa alijitahidi sana kuhusu uchumi na hata thamani ya shilingi ilionekana siyo sasa hali ni ngumu sana cha kushangaza kikwete safari haziishi pesa yote inaishia safari za nje wanajf hilo mnalionaje
 
Back
Top Bottom