Kigeugeu cha Jaji Werema: Ruksa kupinga malipo ya DOWANS!

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,468
911,174
Wednesday, 12 January 2011
Na
Hussein Issa

SIKU moja baada ya Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), kuwasilisha pingamizi Mahakama Kuu kutaka serikali isiilipe Kampuni ya Dowans, Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Jaji Frederick Werema, ameibuka na kusema ni ruksa. Jaji Werema aliliambia gazeti hili jana kuwa, haoni tatizo lolote kwa wanasheria hao kupinga malipo hayo mahakamani, kwani suala hilo halina madhara kwa serikali.

"Waende tu (kupinga mahakamani), kwani ni sehemu ya kazi yao na huwezi kuwazuia. Hii haina madhara yoyote kwa serikali.


Mimi nimeshaongea vya kutosha kuhusu suala la Dowans na kulifafanua sana," alisema. Jaji Werema alisema tayari amesoma hukumu hiyo na kutoa mapendekezo yake kwa wizara husika, hivyo kinachotakiwa sasa ni serikali kutekeleza mapendekezo yake sio kuendeleza mjadala. "Sikiliza. Mimi nimeshatoa maoni yangu kupitia wizara husika. Hayo maswali mnayoniuliza nikiyajibu nitakuwa sijawatendei haki wananchi," alisema Jaji Werema.

Juzi LHRC, kwa kushirikiana na wanaharakati wa haki za jinsia nchini, waliwasilisha pingamizi Mahakama Kuu kupinga malipo ya fidia ya Sh97 bilioni kwa Kampuni ya Dowans. Hata hivyo, ili malipo hayo yafanyike, kesi hiyo ilipaswa kusajiliwa Mahakama Kuu jambo ambalo sasa limeonekana kuingia doa baada ya wanaharakati hao kuweka pingamizi kuzuia mchakato huo.

LHRC walitoa tamko hilo walisisitiza kuwa, wanaungwa mkono na vyama mbalimbali visivyo vya kiserikali yakiwamo mashirika yanayotetea haki za binadamu, usawa wa jinsia na ukombozi wa wanawake (FemAct).

Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC, Francis Kiwanga, alisema wameamua kuweka pingamizi kutokana na mikataba ya awali ya Kampuni ya Dowans kupatikana kwa rushwa na kukiuka maslahi ya umma.

"Kituo kinafungua shauri Mahakama Kuu kupinga uhalali wa tuzo iliyotolewa kwa Dowans isisajiliwe na kuwa, tuzo ya kimataifa kwa sababu mikataba ya awali ilipatikana kwa rushwa na kukiuka maslahi ya umma," alisema Kiwanga. Kiwanga alimtataja Wakili wa Kujitegemea na Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Bagamoyo, Dk Sengondo Mvungi, kuwa ndiye wakili aliyeteuliwa kulisimamia shauri hilo.

"Ikiwa Bunge la Jamhuri ya Muungano kupitia Kamati Teule ya Bunge iliyoundwa Novemba 13, 2007 ilithibitisha kuwa Richmond ni kampuni hewa, inawezekanaje kuwa na mkataba wa kurithisha Dowans?" alihoji Kiwanga. Kiwanga alisema Wizara ya Nishati na Madini inatia shaka kuhusu mwenendo wa suala zima la Dowans na kutaka Tanesco kukataa kulipa deni hilo.

"Uhalali wa kisheria wa miliki ya Dowans kwa mali za Richmond haupo. Ni kwanini serikali haikutaifisha mali za Richmond tangu awali? Pili ikiwa Dowans haikurithi kwa halali mali ya Richmond, inawezekanaje Dowans kuwa na madai halali dhidi ya serikali ya Tanzania?" alihoji Kiwanga.

Kiwanga alielezea shaka kwa serikali kuwa na uharaka wa kulipa deni hilo bila hata kuchukua hatua zozote za kisheria. Alihoji, "Nini hasa maslahi ya Wizara ya Nishati na Madini hasa ikizingatiwa ndio iliyoshinikiza Tanesco kukubali kuhusishwa na kuhamishwa kwa mkataba wa Richmond kwenda Dowans?"
 
"Waende tu (kupinga mahakamani), kwani ni sehemu ya kazi yao na huwezi kuwazuia. Hii haina madhara yoyote kwa serikali.
Mimi nimeshaongea vya kutosha kuhusu suala la Dowans na kulifafanua sana," alisema. Jaji Werema alisema tayari amesoma hukumu hiyo na kutoa mapendekezo yake kwa wizara husika, hivyo kinachotakiwa sasa ni serikali kutekeleza mapendekezo yake sio kuendeleza mjadala. "Sikiliza. Mimi nimeshatoa maoni yangu kupitia wizara husika. Hayo maswali mnayoniuliza nikiyajibu nitakuwa sijawatendei haki wananchi," alisema Jaji Werema.

Hivi Jaji Werema haoni hata haya na kuanza kujirudi kwa kutetea masilahi ya taifa? Na tukamkumbuka kwa hilo?
 
Huyu ni kibaraka wa mafisadi hao wananchi anaowasemea sijui ni wa nchi gani? huyu ni punga wa kisiasa.
 
Hii ndio inatakiwa, Wa Tz tuchukuwe hatua za kulinda resources zetu wenyewe.
Tusipofanya sisi, hawa mafisi wataendelea kuchezea mali za watanzania kila kukicha.
Nawapongeza hawa wanaharakati kwa kuchukua hatua.
 
tarime,lakini ajabu hana hata chembe za tabia za watu wa huko!.
Huyu sio wa Tarime. Hata kama angekuwa wa Tarime haina tatizo. Tatizo ni pale mnapokimbilia kumjadili mtu, dini yake, kabila yake,....., badala ya HOJA alioisema au kuitolea ufafanuzi! Au "MiTanzania ndivyo tulivyo?"
 
KATIBA ibadilishwe watu wawajibike kisheria na si kumtumikia mtu kwa maslahi ya mafisadi
 
sijui walimtoa wapi huyu

Wareme alipendekezwa kwa Rais na mafisadi wakuu wawili Nimrodi Mkono na rafikie Rostam aziz,these two characters are enemies of state sababu wote wemetajirika kwa pesa za walipa kodi kwa kucheza na makaratasi
 
Werema ameanza kuweweseka baada ya kuona UPEPO WA KISIASA KUHUSIANA NA MALIPO YA DOWANS UNAANZA KUBADILIKA.

Werema anajua kabisa kuna WANASHERIA WALIOBOBEA KATIKA SHERIA KULIKO YEYE NA WANAJUA MAMBO VIZURI ZAIDI KULIKO YEYE.
Kwa sasa hivi KILA PEMBE YA TANZANIA WATU WANALALAMIKA KUHUSU ONGEZEKO LA GHARAMA ZA UMEME SAMBAMBA NA KUWALIPA DOWANS MABILIONI YA SHILINGI. Hii inajidhihirisha kuwa Watanzania ndiyo tunaolipia hizo Bilioni 97 kupitia Bill zetu za umeme.

Werema lazima ajue kwamba SHERIA NA HAKI VINAENDA PAMOJA. Ndiyo maana HATA MTU AKIKAMATWA ANAMCHINJA MTU KWA JAMBIA LAZIMA HAKI ITENDEKE KWA HUYO MTU KUWEKEWA WAKILI WA KUMTETEA. HAIWEZEKANI TU AKAHUKUMIWA KIFUNGO PALEPALE. KWA HIYO HILI SWALA LA DOWANS LAZIMA SHERIA NA HAKI ITENDEKE KWA WATANZANIA NA TUJIRIDHISHE KUWA KAMPUNI HEWA YA DOWANS ITALIPWAJE!

HATUWEZI KUKUBALI WAJANJA NA MAFISI WACHACHE WANAJICHOTEA MABILIONI YETU NA KUJILIPA KWA VISINGIZIO VYA KIPUUZI KAMA HIVI VYA DOWANS.
 
Back
Top Bottom