Jana Mgombea Ubunge Jimbo la Kigamboni amezindua kampeni zake,
Hapa chini ni sehemu ya Hotuba yake ya uzinduzi
::::::::::::::::::::
HOTUBA YA MGOMBEA UBUNGE JIMBO LA KIGAMBONI
AGENDA KUU
1. MIUNDOMBINU BARABARA:
Suala la Miundombinu ya Barabara nimelipa kipaumbele cha kwanza kabisa na nitalitilia mkazo kuhakikisha barabara zote za Wilaya na zile za mitaa zinajengwa kwa kiwango cha lami. Pesa ya kutimiza ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami ipo kupitia bajeti ya serikali kuu ambapo nitatumia kiti changu cha Bunge kujenga hoja na kuishinikiza serikali iweke bajeti ya ujenzi Kigamboni kama suala la dharula. Pia bajeti ya Halmashauri nitatumia nafasi yangu ya Ubunge kushinikiza iongezwe mara kumi katika eneo la ujenzi wa miundombinu ya Barabara za mitaa na Barabara kuu kutoka Feri hadi Pembamnazi, Kutoka Ndundwi Songani hadi feri. Na barabara zote za mitaa.
2. TOZO ZA DARAJA NA VIVUKO:
Tozo zote hizi ni haramu, nitahakikisha zinaondolewa, mfano suala la daraja serikali kujitetea kuwa ni deni la NSSF, NSSF ni nani hasa kama sio umma? Basi nikishinda nitashauri na kusimamia kuhakikisha deni la NSSF linabebwa na serikali kuu, na wakati huo Serikali itaongeza Ruzuku za uendeshaji Vivuko, Pesa hiyo itatoka kwenye ongezeko la mapato ya bandari baada ya ubinafsishaji ambapo kila nusu ya mwaka kumekuwepo na ongezeko la 1.8 trilioni ya mapato ya Bandari kupitia DP World. Hapo mwananchi atakuwa ametuliwa mzigo wa tozo ya daraja hilo.
Katiba ya Jamhuri ya Muungano Ibara ya 13.(2) inasema, “Ni marufuku kwa sheria yoyote iliyotungwa na mamlaka yoyote katika Jamhuri ya Muungano kuweka sharti lolote ambalo ni la ubaguzi ama wa dhahiri au kwa taathira yake”.
Ibara ya 13. (4) inasema, “Ni marufuku kwa mtu yeyote kubaguliwa na mtu au mamlaka yoyote inayotekeleza madaraka yake chini ya sheria yoyote au katika utekelezaji wa kazi au shughuli yoyote ya Mamlaka ya Nchi”.
Ibara ya 13.(5) inasema, “Kwa madhumuni ya ufafanuzi wa masharti ya ibara hii neno "kubagua" maana yake ni kutimiza haja, haki au mahitaji mengineyo kwa watu mbalimbali kwa kuzingatia utaifa wao, kabila, pahala walipotokea, maoni yao ya kisiasa, rangi, dini, jinsia au hali yao ya maisha kwa namna ambayo watu wa aina fulani wanafanywa au kuhesabiwa kuwa dhaifu au duni na kuwekewa vikwazo au masharti ya vipingamizi ambapo watu wa aina nyingine wanatendewa tofauti au wanapewa fursa au faida iliyoko nje ya masharti au sifa za lazima, isipokuwa kwamba neno "kubagua" halitafafanuliwa kwa namna ambayo itaizuia Serikali kuchukua hatua za makusudi zenye lengo la kurekebisha matatizo katika jamii”.
Nipeni kura nitaondoa mzigo huu kwa Wananchi na Wananchi wa Kigamboni wataishi sawa na wananchi wengine nchini ambako madaraja yapo na hayalipiwi.
3. MAJI……..Tatizo la maji Kigamboni ni sugu tangu nchi yetu ipate uhuru, Lakini kwamsiojua Kigamboni ndipo mahali pekee kwa jiji la Dar es Salaa palipo na mkondo mkuu wa maji ambapo Dawasco wamechimba visima vikubwa vinne vinavyohudumia jiji la Dar es Salaama yaani Posta, Mbezi na Masaki wanapata maji kutoka Visima vya Kigamboni lakini ajabu na kweli, Wanakigamboni hawapati maji hayo badala yake wanahangaika kutafuta maji kwakutumia Punda, na maguta. Mkinichagua 29 Octoba 2025 nitatenga siku 60 za kusuka mtandao wa maji na kuhakikisha kila nyumba inapata maji safi na salama, kubwa zaidi ni kwamba Watu wataunganishiwa maji bila kulipia gharama za uunganishaji maji serikali itagharamia uunganishaji wa maji hayo kwa kila mwananchi, na badala yake wananchi watalipia matumizi yao ya maji kadiri wanavyotumia tu.
4. AJIRA:
Kuna ishu ya ajira kwa vijana, Mimi mbunge wenu agenda hii ni moja ya agenda ya 3 kati ya agenda kuu zangu 5. Kigamboni ni sehemu ya uwekezaji kwa Mahoteli, Viwanda eneo la Kisarawe II na Mwasonga, Hivyo mimi kama Mbunge nitasimamia halmashauri iweke sheria ndogondogo za uwekezaji kwamba mwekezaji yoyote anayekuja kuanzisha kiwanda au hoteli basi 80% ya Wafanyakazi wake lazima wawe wakazi wa kigamboni.
Pia kwa wale wanaojiajiri hasa Wavuvi, wachimba vifusi/wagonga kokoto, Wajasiliamali wa kada zote bila kujali itikadi zao Watakopeshwa Mkopo Halmashauri bila kuweka kigezo cha dhamana ya kuwa kwenye vikundi au kuwa na mali isiyohamishika.
Mimi Mbunge wenu natambua serikali inamtambua kila mwananchi wake kupitia Kitambulisho cha Taifa NIDA, Pili mimi Mbunge wenu natambua kwamba mafanikio ya mtu katika biashara yoyote hayapatikani kwa kuwa kwenye vikundi bali utajiri ni wa mtu mmoja mmoja. Hivyo nitasimamia kuhakikisha mtu moja binafsi ndie anakopeshwa mikopo hii isiyo na riba, na atakopeshwa kwa kutumia dhamana ya kirambulisho chake cha NiDa au paspoti au Leseni yake ya udereva full stop. Tunaka watu wa kigamboni wawe matajiri sio wawe kausha damu!
Nitatilia mkazo uuanzishwaji wa Viwanda vya usindikaji mazao ya bahari, nitahakikisha Wagonga kokoto wanapewa mikopo isiyo na riba, Wafugaji, Mafundi ujenzi nk
5. TATIZO LA UMEME:
Sera ya Umeme ni kwamba, Mtazamo wa Chama chetu ni kuwa na vyazo zaidi vya umeme na hasa kuwa na vyanzo vya kisasa zaidi hasa umeme wa Nyuklia. Muhimu zaidi chauma tumedhamiria kuondoa gharama za kuunganishiwa Umeme badala yake wananchi wabakie kulipia gharama za matumizi kadiri wanavyotumia tu. Sera yetu nikuwa huduma za kijamii zote kutolewa bure.
Shirika la umeme litaboreshwa na kuwa huria ambapo yataruhusiwa makampuni mengine kufanya kazi ya uzalishaji, usambazaji na uuzaji wa umeme wa umeme kwa bei ya chini zaidi na kwa haraka zaidi. Leo gharama ya Unit 1 inafikia shilingi 350 kiwango ambacho ni kikubwa zaidi ukilinganisha na gharama za maisha yetu. Wakati huo umeme kwa sasa hatununui wa dizel bali ni umeme wetu wa maji kwa 100% kutoka bwawa la JNHP ambapo umeme wa maji kwa viwango vya dunia, gharama ya kuzalisha kwa Unit 1 inakadiliwa kuwa shilingi 60-100 tu.
6. AFYA:
Kuhusu sera ya Afya, Chaumma tunasmini na tutasimamia huduma za afya zote nchini zitakuwa free yaani Bure, hatutauza tena maiti mahospitalini, wala hatutauza tena vichanga vinavyozaliwa mahospitalini kama ilivyo leo. Chaumma tumeongeza kuwa hospitali, vituo vya Afya na zahanati zote nchini Mgonjwa akilazwa atapatiwa chakula hospitalini badala ya sasa ndugu kuhangaika kuwapelekea ndugu zao vyakula.
Pesa ya kutoa bure huduma za afya na elimu zipo za kutosha, chaumma tumejipanga vizuri katika hili
7. ARDHI:
Suala la upimaji na urasimishaji ardhi, Ni ukweli kwamba Kigamboni ndiko kwenye Ardhi kubwa ambayo haijaendelezwa kwa jiji la Dar, na hivyo kuifanya kigamboni kuwa ndio eneo lenye migogoro mingi sana ya ardhi.
Mimi Mbunge wenu nitashirikiana na Halmashauri ya Manispaa kigamboni kuhakikisha ardhi yote kigamboni inapimwa kwa viwango vya mipango miji stahiki, na kubwa zaidi nitahakikisha migogoro ya ardhi inaondolewa kigamboni.
Moja ya njia muhimu ya kuondoa migogoro ya ardhi kigamboni ni kuhakikisha serikali za mitaa zinapewa madaraka kamili ambapo viwanja au shamba ili liuzwe lazima mauziano hayo yathibitishwe na Mwenyekiti wa Mtaa, Mtendaji wa Mtaa na Wajumbe wasiopungua watatu kati ya wajumbe watano wanaounda baraza la uongozi la mtaa.
Bila watu hao hapo juu kutimia na kusaini nyaraka ya mauziano, basi uuzaji huo utakuwa batili. Hati hiyo ya mauziano ipelekwe Kata ikathibitishwe na mtendaji wa mtaa na afisa wa polisi kata.
Hapo tutakuwa tumedhibiti wizi wa ardhi na udanganyifu unaofanyika Kigamboni.
Pia Ardhi Kigamboni ndio nyenzo kuu ya Uwekekeza, Sheria ya utwaaji wa Ardhi ya Uwekezaji inasema mwekezaji lazima kwanza amlipe fidia mwenye ardhi ndipo atwae ardhi hiyo.
Msimamo wangu ni kwamba mwananchi wa Kigamboni asiishie kulipwa fidia tu bali awe sehemu ya umiliki wa mradi huo yaaani awe mbia katika uwekezaji huo kama vile kule kwenye sheria ya madini inavyosema.
Naomba nifafanue zaidi hili, Yaani mwekezaji akija Kigamboni akitaka kuwekeza Kiwanda au Hoteli au mradi wowote akaamua kulipa fidia Wananchi ili kupisha mradi huo, Wananchi wenye ardhi walipwe 90% ya fidia ya ardhi, kisha asilimia 10 inayobaki iwe ni hisa zake katika umiliki wa mradi huo, na mwananchi huyo ataendelea kupokea gawio la 10% ya faida kila mwezi kwa maisha yake yote duniani na vizazi vyake vyote vitarithi umiliki huo hadi mradi utakapofilisika au kufa kabisa kwakuthibirishwa na RITA. Hivi ndivyo ninavyotaka wanakigamboni wawe matajiri kupitia uwekezaji katika ardhi yao.
8. ELIMU:
Sera ya Elimu, Chaumma kitaifa tunaamini juu ya elimu bure kuanzia chekechea hadi chuo kikuu. Chaumma katika sera yetu tumeongeza kwamba mashuleni kitatolewa chakula (ubwabwa) kwa kila mtoto.
9. HAKI ZA BINADAMU: Haki za binadamu Kigamboni zinatuhusu, Mimi ni mhanga wa masaibu ya ukiukwaji wa haki za binadamu ambapo nimewahi kutekwa zaidi ya mar tano na nilifunguliwa kesi 8 mahakamani na kesi moja kuhukumiwa kifungo nakisha kulipa faini, Kesi zote hizo kosa kubwa ni kutoa maoni na kukosoa serikali. Kwahiyo nina mifano hai ya ukiukaji wa haki za binadamu. Leo watu wanatekwa na kuuawa, Rafiki zangu Ben Saanane, Mzee Kibao, Soka na Mdude wamepotezwa kwasababu tu ya kutoa mawazo yao hasi, Mimi Mbunge wenu mkinichagua nitatumia jukwaa la kibunge kuhakikisha serikali yenye wajibu wa kulinda usalama wa raia inawajibika na utekaji unakomeshwa.
10. MICHEZO: Kigamboni kuna vipaji vingi vya michezo ya aina yote, lakini bahati mbaya ccm haiwapendi inawadharau, hatuna viwanja vya michezo, na vile vidogo vilivyokuwepo ccm imeviuza kwa matajiri. Laana ya ajabu hii, Nipeni nafasi ni isuke kigamboni tuibue vipaji vya vijana wetu. Ahadi yangu kwenu mkinichagua nitahakikisha Kigamboni tunajenga uwanja wa kisasa wenye uwezo wa kubeba watu 30M na wenye kutumika kwa michezo yote. Mimi mbunge wetu nitatafuta wawekezaji wa ndani ama wa nje kujenga uwanja huo.
Yericko Nyerere
Mgombea Ubunge Kigamboni