Kigamboni: Askari Magereza wamuua Neema Dominic kwa risasi wakati wakimdhibiti raia aliyeachiwa huru na Mahakama

REST IN ETERNAL PEACE NEEMA DOMINIC;
bila shaka huyo askari aliyetenda uovu huo alikuwa anatafuta kupandishwa cheo na mshahara kulingana na amri ya mkuu wa kaya ya hivi majuzi!!

MUNGU ANAMUONA!!
 
kwaiyo ndio habari kwisha mambosasa hakuna sheria tena kwa huyo magereza aliyeuwa?
au tuunge mkono maneno ya lissu akimkoti jamaa kwamba askari akiua aongezwe mshahara
 
HAYA MAUAJI HATUJUI YATAISHA LINI ILA NIONAVYO MIMI HAWA POLISI WANAFANYA VITA YA KUSHITUKIZA NA SISI RAIA, IMEFIKIA HATUA NA SISI TUJIBU MASHAMBULIZI. HATUTAKI POLISI TENA BORA TURUDISHE JESHI LETU LA SUNGUSUNGU.
 
Mbuzi kafia kea muuza thupu... kifo kiombee kea jirani tu
Na hiyo mpaka Mropokaji aje kumwamuru Katibu mkuu aunde kamati ya uchunguzi itachukua muda.

Hapa ndo weredi wa jeshi la Polisi huwa haueleweki. Wanamfungulia mtu mashtaka, mahakama inamwachia huru then wanatumia sheria vibaya kukamata tena.

Kibaya zaidi utakuta kesi yenyewe ni ya kipuuzi tu.

Halafu Kuna mpuuzi mmoja alisema polisi wa Tanzania wanamafunzo ya kulenga shabaha, wakilenga hawakosei. Sasa ajitokeze tena kujibu na hili maana hawachelewi kusema kuwa huyo aliyeua hajulikani.
 
Leo askari wa magereza wameua msichana Neema Dominic , mkazi wa Tuamoyo aliyemaliza kidato cha nne mwaka juzi.

Kifo hicho kimetokana na Askari Magereza kumfyatulia risasi mfungwa aliyekuwa ameachiwa na Mahakama wakitaka kumkamata tena ndipo risasi walizomfyatulia zikampata Neema na kumuua papo hapo, nyingine zikimjeruhi mama yake mzazi.

_____
Maoni Yangu:

Hivi haya mauaji ya askari kwa RAIA mpaka lini?

========

Dar es Salaam. Neema Dominick mkazi wa Kigamboni Mtaa wa Tuamoyo jijini Dar es Salaam amefariki dunia baada ya kupigwa risasi katika eneo la paja na askari Magereza.

Baada ya risasi iliyomuua Neema kutokea upande wa pili pia ilimjeruhi mama yake mzazi, Rehema Ibrahimu katika eneo la paja.

Mauti hayo yalimpata Neema jana akiwa nyumbani kwao karibu na Mahakama ya Kigamboni wakati askari wa Magereza alipokuwa akijaribu kumzuia mtuhumiwa asitoroke mahakamani.

Akizungumzia tukio hilo, kaka wa marehemu, Juma Mwinjaku alisema kabla ya tukio hilo mtuhumiwa huyo alitoroka kwa mara ya kwanza askari wakafanikiwa kumdhibiti kabla ya kutoroka tena na kuamua kutumia risasi kumzuia.

“Mara zote alipotoroka alikuwa akitumia upande ambao nyumba yetu ipo jambo ambalo lilifanya hata walipotumia risasi kuwa rahisi kutufikia.”

“Lakini kwa nini watumie risasi kumzuia mtuhumiwa ilhali wanajua eneo lile liko karibu na makazi ya watu pamoja na shule? Kwa nini hawaangalii madhara yanayoweza kutokea kwa watu,” alihoji.

“Binti huyo alimaliza kidato cha nne mwaka juzi kuna wakati alikuwa akitaka kwenda jeshini akakosa nafasi hivyo alikuwa yupo nyumbani tu akisubiri utaratibu mwingine,” alisema

Kamanda wa polisi kanda maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa mtuhumiwa aliyekuwa akizuiwa kwa risasi alikuwa tayari ameachiliwa na Mahakama.

Chanzo: Mwananchi

Mheshimiwa Lisu akiyazungumza matukio haya ya mauwaji ya raia, Lumumba na serekali wanakuja juu, oh anatukana taifa mara anatukana serekali au anatukana vyombo vyetu vya usalama. Matukio kama haya ndio yanayotukanisha nchi yetu ki mataifa, na hasa pale yanapotokea na serekali haichukui hatua yeyote. R.I.P binti wa ki Tanzania Neema.
 
Leo askari wa magereza wameua msichana Neema Dominic , mkazi wa Tuamoyo aliyemaliza kidato cha nne mwaka juzi.

Kifo hicho kimetokana na Askari Magereza kumfyatulia risasi mfungwa aliyekuwa ameachiwa na Mahakama wakitaka kumkamata tena ndipo risasi walizomfyatulia zikampata Neema na kumuua papo hapo, nyingine zikimjeruhi mama yake mzazi.

_____
Maoni Yangu:

Hivi haya mauaji ya askari kwa RAIA mpaka lini?

========

Dar es Salaam. Neema Dominick mkazi wa Kigamboni Mtaa wa Tuamoyo jijini Dar es Salaam amefariki dunia baada ya kupigwa risasi katika eneo la paja na askari Magereza.

Baada ya risasi iliyomuua Neema kutokea upande wa pili pia ilimjeruhi mama yake mzazi, Rehema Ibrahimu katika eneo la paja.

Mauti hayo yalimpata Neema jana akiwa nyumbani kwao karibu na Mahakama ya Kigamboni wakati askari wa Magereza alipokuwa akijaribu kumzuia mtuhumiwa asitoroke mahakamani.

Akizungumzia tukio hilo, kaka wa marehemu, Juma Mwinjaku alisema kabla ya tukio hilo mtuhumiwa huyo alitoroka kwa mara ya kwanza askari wakafanikiwa kumdhibiti kabla ya kutoroka tena na kuamua kutumia risasi kumzuia.

“Mara zote alipotoroka alikuwa akitumia upande ambao nyumba yetu ipo jambo ambalo lilifanya hata walipotumia risasi kuwa rahisi kutufikia.”

“Lakini kwa nini watumie risasi kumzuia mtuhumiwa ilhali wanajua eneo lile liko karibu na makazi ya watu pamoja na shule? Kwa nini hawaangalii madhara yanayoweza kutokea kwa watu,” alihoji.

“Binti huyo alimaliza kidato cha nne mwaka juzi kuna wakati alikuwa akitaka kwenda jeshini akakosa nafasi hivyo alikuwa yupo nyumbani tu akisubiri utaratibu mwingine,” alisema

Kamanda wa polisi kanda maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa mtuhumiwa aliyekuwa akizuiwa kwa risasi alikuwa tayari ameachiliwa na Mahakama.

Chanzo: Mwananchi
Mpandishe cheo huyo askari katimiza kigezo muhimu kuua raia yule wa tengeru amehamishwa kituo ili apandishwe vizuri. Hongera manjagu.
 
Na hiyo mpaka Mropokaji aje kumwamuru Katibu mkuu aunde kamati ya uchunguzi itachukua muda.

Hapa ndo weredi wa jeshi la Polisi huwa haueleweki. Wanamfungulia mtu mashtaka, mahakama inamwachia huru then wanatumia sheria vibaya kukamata tena.

Kibaya zaidi utakuta kesi yenyewe ni ya kipuuzi tu.

Halafu Kuna mpuuzi mmoja alisema polisi wa Tanzania wanamafunzo ya kulenga shabaha, wakilenga hawakosei. Sasa ajitokeze tena kujibu na hili maana hawachelewi kusema kuwa huyo aliyeua hajulikani.
Tena ni wakigamboni na yeye
 
Na ndiyo mkuu wake eneo husika!_
Na hiyo mpaka Mropokaji aje kumwamuru Katibu mkuu aunde kamati ya uchunguzi itachukua muda.

Hapa ndo weredi wa jeshi la Polisi huwa haueleweki. Wanamfungulia mtu mashtaka, mahakama inamwachia huru then wanatumia sheria vibaya kukamata tena.

Kibaya zaidi utakuta kesi yenyewe ni ya kipuuzi tu.

Halafu Kuna mpuuzi mmoja alisema polisi wa Tanzania wanamafunzo ya kulenga shabaha, wakilenga hawakosei. Sasa ajitokeze tena kujibu na hili maana hawachelewi kusema kuwa huyo aliyeua hajulikani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huwa najiuluza kwanini upige rusasi wakati mazingira hayaruhusu.

Mtuhumiwa anaweza akatafutwa tu kwa namna nyingine.

Naamini ni kushindwa kufanya maamuzi sahihi na mtuhumiwa alijua kabisa hawawezi ku shoot upande huo lakini askari mwenye mafunzo ya silaha alishindwa kung'amua hilo.

So sad Punzika kwa amani Binti.
 
Huyo mtuhumiwa tayari anayokesi ya kujibu
kwanini amemsababishia asikari magereza
kumpiga risasi raia mwema.
 
Maaskari wenyewe waleeeevi, mikono inatetemeka tu watawezea wapi kulenga shabaha
 
hii taarifa umeitoa kinafiki sana . huyo neema alikuwa wapi wakati risasi inafyatuliwa? huyo neema alienda mahakamani kama nani kwa mtuhumiwa ama mshtaki ?
hivi huyu alieandika ni binadamu ,kama ni binadamu basi n i j......i...n...g..a...puuziiiiiiiiiiii
 
Back
Top Bottom