Kifurushi gani unatumia kwenye simu?

Kifurushi gani unatumia kwenye simu?

Heshima kwako, nimefikia hatua ya kuandika hapa ili kupata unafuu wa vifurushi vya internet baada ya Voda kunibadilikia siku kadhaa baada ya uchaguzi sasa wananifyeka MB kwa kasi ya ajabu, wenye kutumia mitandao mingne vipi huko kwenu?

Halotel Royal Bundles pia zikoje?

Msaada tafadhali.
Airtel ya 35000 wananipa 40 gb japo haimalizi mwezi ila ni fresh
 
😲 Umetisha
Kuna mtu humu alisema yeye kwa mwezi anatumia zaidi ya 200gb. Mimi siku yangu inaanza saa 11 kwa kudownload files zina 900mbs, technically zina 4gb ila niligundua formula ya kuzi convert kwenye format nyingine so zinapungua ukubwa.

Halafu lazima nifanye calls skype 1hr na zoom kama 1.5 hours kila day. bado kuja humu kupiga story halafu uwa natazma video 144p Youtube kama za 1.5hrs kuhusu topics mbalimbali ndiyo maana.
 
Kwa sisi ambao hatuna kipato cha uhakika, Halotel ni mkombozi
 
Airtime: Airtel mitandao yote 10,000 DK 1150 kwa mwezi, hata sizimalizi hakyanani.

Data: TTCL namba tano inanihusu na huwa zinakata kabla mwezi haujageuka.
Screenshot_20201123-230624.jpg
 
Ivi kwanini Voda Moro super Uni ni 2000tsh GB 1 kwa wiki lakini mikoa mwingine Kama tanga, Pwani, DSM ni 1500tsh kwa wiki.
Mi niko Dar lakini wananipa Supa UNI kwa 2000. Sijui wanavigezo vp kugawa hizi ofa.
Screenshot_20201123-234745.jpg
 
Jamani hivi kwa nini internet ya Vodacom ni so expensive?

Nilikuwa naitumia lakini nimeamua kuwakimbia. Yaani internet yao ni ghali wakati kwa uzoefu wangu sioni kama wako bora kuliko Airtel au Tigo.

Kama humu kuna mtu wa Vodacom atusaidie. Kwa nini vifurushi vyenu ni ghali mno? Kuna kitu gani cha ziada?
 
Back
Top Bottom