Kifungo Mwenzi Mmoja Kwa Kubusiana Hadharani

Hawa watu wanastahili pongezi kwa kulinda na silka,maadili na adabu za tamaduni zao bila kujali wala kutazama mtu usoni. Kwa baadhi ya watu inaonekana kama kinyume nyume, nakumbika miaka ile ya 1990,palitokea tukio hapa Tanzania la Wazungu wawili kukamatwa kwa kosa la kumfanyisha ngono mwanamke wa Kitanzani na mbwa wao, baadae waliachiwa kwa kuwa hakukuwa na kosa kama lile katika vitabu vya sheria zetu na diplomasia nazo zikamaliza kesi kabisa, ni hivi karibuni tena huko mikoa ya kanda ya ziwa Watanzania wenyewe walifanya kitendo hicho hicho cha kumrubuni binti wa watu masikini na kumfanyisha mapenz na mbwa wa mzungu, cha kujiuliza hapa je ni vibaya kuwa na sheria zinazokubali kutambuwa hatia ama kosa la kimaadili japo halipo katika sheria za kizungu tulizorithishwa na wakoloni? sasa hawa wenzetu wa Dubai hawa kusubiri hayo yatokee wanayapinga kwa nguvu wanazoweza kulinda tamaduni zao ambzo wao wanaamini ni bora kuliko hizo za hao wanaowaona hawajuwi.
Chambelecho, ya E.Kezilahabi, "Dunia Uwanja wa Fujo", watu wanauwana kwa uchawi na ushirikina na athari zake zinakuwa kubwa kwa jamii na hali ya uvunjifu wa amani hutokezea kwa mambo haya, na utangamano wa jamii huwa mashakani kwa mambo haya haya lakini kwa kuwa sheria za kikoloni tulizoachiwa hazitambuwi, madhara yanayosababishwa na uchawi kuwa ni makosa na sisi kwa ulimbukeni wetu wa tai za rohoni na kalamu mifukoni,tumeyaacha mambo hayo yaendelee kuharibu jamii...leo akija mganga akisema "...atakayeshindana kugombea kiti cha uongozi na fulani,basi atakufa..." tushajisahau kuwa uhuru wa watu kuwa na fikra za kimaendeleo umetishiwa na sheria hatuna,tufanyaje, JANGA SUGU LA WAZAWA hili....hongereni wa Dubai...Mkataa utamaduni wake na akuwacha unajisiwe na watandawazi huyo ni mjinga
 
Back
Top Bottom