Kifungo kilivyowakatisha masomo wanafunzi Mara

Ng'wanza Madaso

JF-Expert Member
Oct 21, 2008
2,268
333
Kifungo kilivyowakatisha masomo wanafunzi Mara



Mobini Sarya




NI miaka 47 sasa imepita tangu nchi hii ijikomboa kutoka makucha ya wakoloni, lakini hali ilivyo sasa ni kama wamerejea kwenye ukoloni kwa mtindo mwingine.

Nimenza na maelezo hayo kutokana na hali halisi ya uwekezaji wa kampuni ya Grumet Reserve Fund ya mkoani Mara, iliyowekeza vitegauchumi katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, lakini baadaye iliingia makubaliano mengine na viongozi wa serikali na kupatiwa eneo la uwindaji lililokuwa likitegemewa na wananchi.

Sasa kampuni hiyo imegeuka tatizo kwa wananchi wa eneo hilo hadi kufikia hatua ya kuwafanya watoto wa Wilaya ya Bunda kugeuka watumwa na kutoona umuhimu wa nchi yao inayoongozwa na utawara bora wa sheria.

Hiyo inatokana na ukweli kwamba wakati viongozi wa serikali za mitaa katika maeneo hayo wanaingia makubaliano na mwekezaji huyo, Grumet Reserve Fund haikujua kama ingepata madhara inayopata hivi sasa.

Siku chache baada ya gazeti hili kuripoti habari za kufungwa jela mwanafunzi Gonjoju Gilabi (13) kwa kosa la kunywesha mifugo maji katika Mto Rubana, Bunda, mwanafunzi mwingine wa Darasa la Sita, Kihagazo Nyakile (14), alihukumiwa kifungo cha miaka mitatu kwa kosa kama hilo lakini alikaa jela miezi miwili.

Nyakile aliyekuwa akisoma Shule ya Msingi ya Kunzugu katika wilaya hiyo, amefungwa miaka mitatu kwa kosa la kunywesha ng’ombe maji katika mto, wanaomilikiwa na baba yake. Mto huo unatenganisha eneo la mwekezaji wa Grumet Reserve Fund na wanakijiji.

Akisimulia tukio hilo kwa masikitiko, kaimu Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi ya Kunzugu, Deus Mogasa, anasema mwanafunzi huyo ameathirika kisaikolojia kutokana na kutupwa kwenye gereza la watu wazima la Butimba, mkoani Mwanza.

‘‘Kuna kijana mmoja hapa wa Darasa la Sita naye amekumbwa na mkasa kama huo, baada ya kukamatwa na kufungwa akiwa na mifugo ya baba yake katika mto ule,” anasema Mogasa akionyesha kwa kidole mto huo ambao uko jirani na shule hiyo.

Kwa mujibu wa mwalimu Mogasa, mwanafunzi huyo kwa kuwa alifanya kosa, alipaswa kupewa adhabu ndogo ya kumuonya na kumuasa si kumfunga.

‘‘Hii ilikuwa kumpa adhabu ndogo kama kumkanya tu, lakini sasa walipomfunga miaka mitatu ni matatizo makubwa kwa sababu haifundishi ila wanazidisha chuki kwa jamii,” anasema.

Mzazi wa mwanafunzi huyo, Nyakile Kihagazo, anasema mtoto wake alikamatwa Desemba 30, mwaka jana, alipokuwa amepeleka ndama wake mtoni.

Anasimulia kwamba siku hiyo askari wa mwekezaji wa kampuni hiyo walikuwa wamekamata watu wengine watatu katika eneo hilo, na mtoto wake alipofika na ndama hao baada ya kunywa maji wengine walivuka ng’ambo ya mto huo ikabidi avuke kuwarudisha ndipo akatiwa mbaroni kwa kosa la kuingia hifadhini.

‘‘Siku hiyo mwanangu alikwenda kuchunga ndama na alipofika kwenye mto huo unaotutenganisha na hifadhi, yeye akiwa nyuma na ndama mbele alipofika akakuta ndama wamevuka akaenda kuwarudisha, ndipo akakumbana na askari waliokuwa wamekamata wachungaji wengine watatu wakamuunganisha” anasema mzee Nyakile.

Baada ya kukamatwa walipelekwa na mifugo yao kwenye kambi ya Ndabaka ambako walitozwa sh milioni 2; mifugo ikaachiwa wale wachungaji wakapelekwa kesho yake mahakamani na kuhukumiwa siku hiyo hiyo akiwemo huyo mtoto.

‘‘Siku ya kesi ilipofika mshitakiwa namba moja alikuwa mwanangu kwa kuwa alikuwa mtoto aliposomewa shitaka akakubali kosa akafungwa miaka mitatu, baadaye nikakata rufaa Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza akaachiwa kwa dhamana wakati kesi inaendelea,” anasema Nyakire.

Mwanafunzi Gonjoju Gilabi (13) wa Shule ya Msingi Mariwanda, amefungwa miaka mitatu jela kwa kosa la kuingiza ng’ombe wa mzazi wake katika mto Rubana.

Wakizungumza na Tanzania Daima, kijijini Mariwanda, Kata ya Hunyari, walimu wa shule hiyo wamesema Gilabi alikuwa miongoni mwa wanafunzi 10 bora waliotarajiwa kujiunga Kidato cha Kwanza mwaka huu.

Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, David Balijera, anasema Gilabi aliyekuwa na uwezo mkubwa darasani, ameharibiwa maisha kwa kosa ambalo kimsingi lilipaswa kulipiwa faini ya shilingi 50,000.

“Kwa kweli hata mimi mwalimu wake nimesikitishwa na hii hukumu, kwani huyo mtoto nilikuwa namtegemea kuiwakilisha shule yangu katika shule za watoto wenye vipaji kutokana na uwezo wake,”anasema Baljera kwa masikitiko.

Gilabi alikuwa miongoni mwa wanafunzi watano bora waliokuwa wanaongoza darasani, hivyo shule yake ilimtegea kuchaguliwa katika shule za watoto wenye vipaji.

“Hata kama Gilabi asingechaguliwa katika shule zenye vipaji maalumu, bado angekwenda sekondari kutokana na ukweli kwamba shule hii ndiyo imekuwa ya kwanza kiwilaya, kufaulisha wanafunzi 61 kwenda sekondari mwaka huu,” anasema Baljera.

Mwalimu huyo anasema taarifa za kufungwa mwanafunzi huyo kwa kosa ambalo lingemalizwa kwa kulipwa fidia zilimsikitisha hadi ikabidi awasiliane na wakuu wa idara akiwemo Ofisa Elimu wa wilaya kama watamsaidia mwanafunzi aweze kufanya mtihani.

Anasema baada ya kuwasiliana na Ofisa Elimu wa Wilaya alimwambiwa amjazie fomu zote za mtihani ili akibahatika kutoka jela siku moja kabla aweze kuruhusiwa kufanya mtihani, jambo alilotekeleza kwa kumjazia fomu ya TSM 9.

Mkuu wa Wilaya ya Bunda, Chiku Galawa, alipoulizwa kuhusiana na ukiukwaji huo wa haki za watoto kushindwa kuendelea na masomo, alisema hana taarifa hiyo.

‘‘Sina habari hizo...wewe ndio kwanza unaniambia...inawezekana alipokamatwa alishindwa kujieleza kwamba yeye ni mwanafunzi ndiyo maana hakimu akamhukumu kama mtu wa kawaida, sasa nitaanza kulifuatilia suala hilo,” anasema Luten Galawa.

Mwenyekiti wa kijiji hicho, Samson Kisung’unda, anasema jitihada za kuhakikisha mwanafunzi huyo anaachiwa zilifikishwa hadi kwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Shamsa Mwangunga, aliyeahidi kulisimamia lakini hakuna lolote lililofanyika hadi sasa.

Kisung’unda anasema katika hotuba aliyomsomea Mwangunga, alimjulisha juu ya matesa ya wananchi wanayopata katika eneo hilo ikiwemo kufungwa kwa wanafunzi kwa kosa ambalo lisingemfanya akaenda jela.

‘‘Baada ya maelezo hayo, waziri akanitaka nimthibitishie nikamwomba Mwalimu Mkuu amweleze ukweli huo.”

Baadhi ya walimu waliozungumza na Tanzania Daima wamesema suala la kufungwa kwa mwanafunzi huyo, limetokana na uelewa mdogo wa wananchi eneo hilo kushindwa kudai haki zao kwa sababu mwanafunzi hakuwa anamiliki mifugo.

Kaimu Ofisa Mtendaji wa kijiji hicho ambaye pia ni Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Mariwanda A, Damian Wegina, anasema amekuwa akishuhudia wanakijiji wakifikishwa ofisini kwake kwa ajili ya kulipishwa faini na askari wa mwekezaji bila kuhoji haki zao.

Mwanafunzi huyo aliyekuwa afanye mtihani wake Oktoba mwaka jana kwa kutumia namba PS0/9011137/013, alikamatwa na askari wa kampuni hiyo.

Kwa sasa anahitaji msaada wa kisheria pamoja na huruma ya Rais Jakaya Kikwete kuweza kutumia msamaha wa wafungwa kumtoa gerezani aweze kuendelea na masomo yake.

Mzazi wa mwanafunzi huyo, Matobora Meshinya (59), akizungumza kwa huzuni ameomba mashirika ya kutetea haki za watoto pamoja na vituo vya misaada ya sheria kujitokeza kumtoa mwanae gerezani.

Meshina anasema kwamba mara baada ya kupata taarifa za kukamatwa mwanaye alikwenda polisi na kukuta mtoto amesha pelekwa mahakama ya wilaya ya Bunda.

“Nilipofika mahakamani sikumkuta mwanangu alikuwa amekwishahukumiwa miaka mitatu bila hata kupatiwa muda wa kujitetea...nilipojaribu kutafuta uwezekano wa kuachiwa nikaambiwa kwamba mtoto ameshapelekwa gereza la Tabora B, wilayani Serengeti,” anasema mzee huyo.

Akijibu malalamiko hayo msemaji wa Grumet Reserve Fund, Shaaban Madanga, alisema malalamiko hayo si mapya kwani yamekuwepo siku nyingi.

Askari wa kampuni hiyo hawawezi kulalamikiwa kutoka na kitendo cha kufungwa wanafunzi hao, kwani wao wanakamata wanaokiuka sheria za hifadhi na mahakama ndiyo inayohukumu.

“Wananchi wenyewe wanajua kwamba ni kosa la sheria za uhifadhi kusogelea maeneo hayo, lakini wanafanya makusudi halafu wanalalamika,” anasema Madanga.

Source: Mtanzania Daima.


MY TAKE:Je hakuna uwezekano wa kuwasaidia hawa vijana na wazazi wao wanaoteseka?
 
Labda hao wanao jitia kutetea haki za binadamu (watoto), wameona kuwa hakuna dili wala ulaji hapo.
 
Last edited:
Labda hao wanao jitia kutetea haki za binadamu (watoto), wameona kuwa hakuna dili au ulaji.
Kwani kwenye msaada kunahitaji ulaji?. Kwani hao wanaotetea haki za binadamu na za watoto hawana mafungu ya pesa maalum?.
 
Kwani kwenye msaada kunahitaji ulaji?. Kwani hao wanaotetea haki za binadamu na za watoto hawana mafungu ya pesa maalum?.
Kilicho pelekea mpaka mtoto wa miaka 13 kufungwa miaka3 kwa kosa la kunywesha ndama wake, na uku hao wanao jiita watetezi wa haki za watoto wanaangalia bila ya kufanya lolote la maana ni kitu gani?
Au mpaka waletewe Fund toka nje ya nchi!?
 
Kama habari hii ni ya kweli basi ndiyo kasi mpya na ari mpya hiyo. How comes Waziri ana ataarifa ili hali DC hajui lolote? Its sickening hata kusoma habari yenyewe. Huyo hakimu na askari magereza iweje wawasweke watoto katika gereza la watu wazima? How comes? Mwandishi anasema Ukoloni umeisha! kwa hilo hao wananchi bado wako katika makucha ya ukoloni. N ahao viongozi waliojaza hiyo mikataba walikuwa na njaa au walikatiwa kitu kidogo? Je is possible ku review mkataba huo?
 
Haya ni madhara ya kuuza nchi yetu, urithi wetu na mali zetu kwa wageni. Leo hii Mtanzania anakuwa mtumwa ndani ya nchi yake. Hayo ni machache yanayotokea ndani ya Tanzania kuhusu unyanyasaji wa raia. Karibu kila shirika ama kampuni iliyonunuliwa na wageni kuna malalamiko ya unyanyasaji.

Tulimwondoa mkoloni Tanzania miaka mingi iliyopita na tulishangilia kwa mbwembwe na vigelegele vingi sana, lakini leo hii sisi wenyewe tunamwita mkoloni tuliyemfukuza aje tena kututawala.

Watanzania tusikubali utumwa huu kwani Watanzania si mabwege tena.
 
Ninashangaa sana hapa JF kukitokea habari ya vyama vya siasa watu watachangia sana lakini habari kama hizi watu wako kimya hawataki hata kuchangia au kwa kuwa aliyeileta hii habari sio ............? kwa nini watu wanabagua habari za kuchangia humu.
 
Haya ni madhara ya kuuza nchi yetu, urithi wetu na mali zetu kwa wageni. Leo hii Mtanzania anakuwa mtumwa ndani ya nchi yake. Hayo ni machache yanayotokea ndani ya Tanzania kuhusu unyanyasaji wa raia. Karibu kila shirika ama kampuni iliyonunuliwa na wageni kuna malalamiko ya unyanyasaji.

Tulimwondoa mkoloni Tanzania miaka mingi iliyopita na tulishangilia kwa mbwembwe na vigelegele vingi sana, lakini leo hii sisi wenyewe tunamwita mkoloni tuliyemfukuza aje tena kututawala.

Watanzania tusikubali utumwa huu kwani Watanzania si mabwege tena.
Usishangae kwa hili kutokea kwani serikali yetu kwa kukaa kimya ndio kawaida yao kama ya mgodi wa North mara watu wameongea na viongozi wa dini wametembelea na kutoa maoni kwa serikali hakuna kilichotokea itakuwaje hili la kijijini na mwekezaji?
 
Za mwizi arobaini. One day hali itakuwa mbaya na mwisho KOSOVO. Maana wananchi watkandamizwa wee mwisho wataamua kuondolea uvivu manyanyaso. ikifikia wakati huo serikali itaanza kutumia mabavu na nguvu. Ndiyo mwisho wa hadithi ya amani na utulivu wa ukondoo!!!!!!
 
Za mwizi arobaini. One day hali itakuwa mbaya na mwisho KOSOVO. Maana wananchi watkandamizwa wee mwisho wataamua kuondolea uvivu manyanyaso. ikifikia wakati huo serikali itaanza kutumia mabavu na nguvu. Ndiyo mwisho wa hadithi ya amani na utulivu wa ukondoo!!!!!!
hasa vijijini ambako watu wanesahaulika kama vile hakuna binadamu.
 
Ninashangaa sana hapa JF kukitokea habari ya vyama vya siasa watu watachangia sana lakini habari kama hizi watu wako kimya hawataki hata kuchangia au kwa kuwa aliyeileta hii habari sio ............? kwa nini watu wanabagua habari za kuchangia humu.
Pole Degauche, this is JF...!
 
Ni wakati muafaka kama hali itaendelea hivyo basi jadi ianza kutumika. just kuanza kuwagecha. Jamaa wa mara si nasikia hawana mchesomcheso. au watumie tradition ya wazanaki(wawatungue na mishale ya sumu) wakilambwa waliobakia wachache watakimbia!!!! kama wezi wanachinjwa live kamateni hao asakri chinja mmoja au wawili hivi. hawatakama tena mtu hapo.
 
Kwa kweli mm inaniuma sana......mawakili walio karibu pse....nendeni mkaookoe jahazi JF (wadau wengi) nina imani tuko tayari kuchangia gharama za mawakili....ili hao watoto watolewe jamani ni aibu kwa mahakama na jamii nzima hasa watetezi wa haki......nipo tayari kabisa kuchangia mawakili.....
 
Tatizo si kuchangia mawakili. hiyo ni end result. Si wataendelea na kukamata na hakim huyo kichwa kibovu hata haulizi umri ataendelea kuwafunga nasi tutaendelea kuchanga kwa ajili ya wakili. vicious circle. Wauza Ardhi ya wananchi should stop na mikataba iliyosainiwa isitishwe mara moja. sasa waliondani tuwatoe. Mwisho wa ugomvi.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom