Kifo ni sehemu ya mpango wa Mungu

Kifo ni sehemu ya mpango wa Mungu

Malaria 2

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2023
Posts
8,478
Reaction score
12,672
Kifo ni sehemu ya mpango wa Mungu

Qur'an inasisitiza kuwa kifo ni mchakato wa kawaida uliopangwa na Mwenyezi Mungu kwa kila kiumbe hai.

"Kila nafsi itaonja mauti..."
(Surah Aal-Imran 3:185)

"Ambaye ameumba mauti na uhai ili kukujaribuni, ni nani katika nyinyi aliye mbora wa vitendo."
(Surah Al-Mulk 67:2)

2. Hakuna anayeweza kuepuka kifo

Hata Mitume na watu wema hawawezi kuuepuka wakati wake ukifika.

"Mahali popote mlipo, mauti yatakufikieni, ijapokuwa mko katika ngome zilizo imara..."
(Surah An-Nisa 4:78)

3. Kifo sio mwisho, bali ni mwanzo wa maisha mengine

Qur'an inaeleza kwamba maisha ya duniani ni ya muda, na baada ya kifo kuna maisha ya Akhera, yaani maisha ya kudumu.

"Na hakika nyumba ya Akhera bila ya shaka ndiyo maisha hasa – laiti wangekuwa wanajua."
(Surah Al-Ankabut 29:64)

4. Malaika wa mauti

Qur'an inamtaja Malaika anayehusika na kuchukua roho za viumbe wakati wa kifo.

"Sema: Malaika wa mauti atakayekufeni, atakufeni; kisha mtarudishwa kwa Mola wenu Mlezi."
(Surah As-Sajda 32:11)

5. Hakuna kuchelewa wala kuharakisha kifo

Kifo hutokea kwa wakati ulioandikwa, hakuna mtu anayeweza kukichelewesha au kukiharakisha.

"...Basi wanapowadia muda wao hawataweza kuchelewa hata saa moja, wala hawatatangulia."
(Surah An-Nahl 16:61)
 
Sasa kwanini mtu akifa tu baada ya robo saa mnakua mshamfukia pengine anakua kazimia kwanini msisubiri kwanza?
Ushawahi kusikia hivyo wapi? Sisi waislam akifa saa 2 asubuhi basi baada ya Alasiri tunaenda kumsitiri na sio kumfukia. Wengine baada ya Adhuhuri tunaenda kumsiri. Hatujazika mtu mzima. Au dini nyengine ndio maana wanakaa siku 3 na maiti kusubiri kufufuka?
 
Aliyeonja Mauti kwa niaba ya Wanadamu ni Yesu Kristo pekee yake!
(Waebrania2:9)
Yeye alikufa mara moja na akafufuka mara moja na hawezi kufa tena milele yote.
Wengine Wote Wakifa hawafufuki tena mpaka siku ya Kiyama wakingoja Hukumu ya Mauti au Uzima wa Milele,(Yohana5:26-29)
Kwa lugha nyepesi kuna tofauti ya Kuonja na Kunywa kabisa.
Vinginevyo kama ulivyosema Hakuna anayeweza Kuchelewesha au Kuharakisha Kifo cha mtu labda Mwenyezi Mungu mwenyewe akiamua atakavyo,uko sahihi.
 
Kifo ni kifo tu hayo mengine ni kujifariji tu
 
Aliyeonja Mauti kwa niaba ya Wanadamu ni Yesu Kristo pekee yake!
(Waebrania2:9)
Yeye alikufa mara moja na akafufuka mara moja na hawezi kufa tena milele yote.
Wengine Wote Wakifa hawafufuki tena mpaka siku ya Kiyama wakingoja Hukumu ya Mauti au Uzima wa Milele,(Yohana5:26-29)
Kwa lugha nyepesi kuna tofauti ya Kuonja na Kunywa kabisa.
Hizo ni imani tu hakuna uthibitisho wowote
 
Ushawahi kusikia hivyo wapi? Sisi waislam akifa saa 2 asubuhi basi baada ya Alasiri tunaenda kumsitiri na sio kumfukia. Wengine baada ya Adhuhuri tunaenda kumsiri. Hatujazika mtu mzima. Au dini nyengine ndio maana wanakaa siku 3 na maiti kusubiri kufufuka?
Hamna nyinyi akianguka saa 2 asubuhi mazishi yanakua saa 3 tena kwa kukurupushana ukichelewa unakuta watu washamfukia mtu na wamekaa juu ya kaburi kulinda asije mtu akaja kufukua, kwaanini mnafanya hivyo? Hamjui km kuna wengine mnawazika wakiwa bado wapo hai?
 
Hizo ni imani tu hakuna uthibitisho wowote
Tunaamini kilichoandikwa kwenye Vitabu vya Mungu.Vitabu vimeweka Ushahidi wa matukio yote yaliyotokea kwenye historia ya mwanadamu,na mpaka leo watu wanakufa.
Yanayotokea mfano wa yale yaliyoandikwa ni uthibitisho wa kile tunachoamini.
 
Tunaamini kilichoandikwa kwenye Vitabu vya Mungu.Vitabu vimeweka Ushahidi wa matukio yote yaliyotokea kwenye historia ya mwanadamu,na mpaka leo wanakufa.
Mungu wenyewe hathibitiki uwepo wake sembuse maneno ya kwenye kitabu?
 
Ushawahi kusikia hivyo wapi? Sisi waislam akifa saa 2 asubuhi basi baada ya Alasiri tunaenda kumsitiri na sio kumfukia. Wengine baada ya Adhuhuri tunaenda kumsiri. Hatujazika mtu mzima. Au dini nyengine ndio maana wanakaa siku 3 na maiti kusubiri kufufuka?
Wewe ukifa saa 4 asubuhi kisha tukikufukia saa 5 asubuhi hio hio yaan limepita saa 1 tu la kukuchimbia kaburi tukakufukie chini utakubari yaan haupewi muda hata wa kupumua utakubari wewe?
 
Back
Top Bottom