Kifo (mauti) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kifo (mauti)

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Mar 15, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Mar 15, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  Watu wako wamelala hali wako hai na huwa macho baada tu ya kufa. kujielekeza kwa mabaki ya matamanio ya mtu ndiko kujiuwa haraka. Ufe kabla ya kifo kukuijia. Mauti inaidhihaki tamaa..

  Mauti ni kutenganisha toka kitakachoisha na kuelekea kule pasipokwisha.
  . Kuikumbuka mauti kila mara kutampunguzia mtu tamaa za duniani.
  Wale watembeao juu ya ardhi siku moja watazikwamo.
  . Tamaa hukuongoza katika njia ya upotofu.. Wakati hatuna matumaini huwa hatuhuzuniki..

  Kufadhaika huwa pamoja na tamaa.
  Kinachoipatia madhara na hasara dini ni tamaa. Waroho ni watumwa wa matilabayao..
  Kutokuwa na mategemeo kunaituliza na kuipumzisha roho.
  Uroho huuangamiza uadilifu. Ubinadamu ni wa aina mbili; wale wenye matamanio matupu na

  wale watakao kuja kuwa wasioridhika.
  . Tamaa huingamiza hadhi ya mtu bila ya kuongezeka kwa bahati yake.

  Hata kama wakiwa uchi na wenye njaa, hao walioridhika huwa ni wenye furaha.
  . Kuridhika ni hazina isiyo na kifani.. Kuridhika ni hadhi na heshima isiyodidimia milele. Mwenye kuridhika tu ndiye aishiee kwa amani na usalama.
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Mar 15, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Source?

  Mkuu, ujumbe wako unaongea ukweli mno!...
  Nimetishika sana!
   
 3. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #3
  Mar 15, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  Jiepushe na Tamaa za dunia mkumbuke Aliye kuumba uache Maasi.
   
 4. Shark

  Shark JF-Expert Member

  #4
  Mar 15, 2012
  Joined: Jan 25, 2010
  Messages: 20,140
  Likes Received: 7,394
  Trophy Points: 280
  Kaka unanitisha,
   
 5. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #5
  Mar 15, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  Kuogopa mauti!
  Watu wengi wana mtazamo wa kutishia kuhusu mauti, na kwa hivo, si wengi wasiohofia kufa. Lakini, watu tofauti hupata athari tofauti kutokana na hofu hii. Wengine huona wataweza kuikimbia hofu hii kwa kukusanya mali mengi, kwani mali huwafanya wasiogope sana uhakika wa mauti.
  Wengine nao huona kuwa mauti yanatishia kwani wengi wanayafkiria kuwa yana maumivu. Kwa hivyo, hawa hujiambia kuwa mauti hayana maumivu, na mwanadamu hahisi lolote baada ya kufa kwake.
  Wengine nao huhepa hii hofu kwa kutofkiria wa kuzingatia mauti, na kuwanasihi wengine pia wasitafakari kuhusu mauti, ili wasiogope mauti.
  Uzoefu unaonyesha kuwa njia zote hizi hazisaidii kuondoa hofu ya mauti.


  Kwanini watu wanaogopa mauti?
  1. Kupenda maisha ya dunia ni sababu kubwa ya kuogopa mauti, haswa kwa yule ambaye lengo lake lote ni huu ulimwengu. Mtu akam huyu huogopa mauti kwani huona kama mauti itamuondolea raha na anasa zote anazozijua.
  Mtu anafaa azingatie: je, kama ulimwengu wa baada ya mauti ni bora na wa kupendeza na kufurahisha kuliko dunia hii, lengo lake litakuwa kufikia dunia ile nyingine, na hatohofia kupoteza raha za dunia hii.
  2. Kutojua uhakika wa mauti ni sababu nyingine ya hii hofu ya mauti. Hajui kuwa mauti ni mapito tu, au mlango wa kumpeleka kutoka dunia hii kuingia dunia nyingine, na hudhani kuwa mauti ni mwisho wa yote. Mtu akifikira hivi bila shaka atakuwa na hofu kuhusu mauti, na kuona mauti kama jambo la kutisha.
  3. Hofu ya kujibu kuhusu aliyoyafanya katika hii dunia pia humfanya mtu ambae hakumtii Mungu, lakini anaamini kuwa kuna akhera, au dunia nyingine baada ya mauti, kuogopa mauti.
  Tumeangalia kuhusu uhakika wa kifo hapa. Katika makala yajayo, tutazidi kuangalia uhakika wa jambo hili.
   
 6. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #6
  Mar 15, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 18,037
  Likes Received: 750
  Trophy Points: 280
  Kweli tupu.
   
Loading...