Je kila nafsi itaonja mauti?

brevars

Member
Apr 15, 2023
49
71
Wadau, habari ya majukumu bila shaka muwazima wa afya, kama na wale wenye changamoto ya afya, niwaoe pole.

Bila kupoteza muda, twende kwenye mada husika. Hili neno "kila nafsi itaonja mauti," kiuhakika, halijaandikwa kwenye Biblia. Nadhani ni utashi tu wa mwadamu ameamua kutumia hili neno. Sasa turudi kwenye swali letu: Je, ni kweli kila nafsi itaonja mauti?

Kwenye kitabu cha Ufunuo, kinasema parapanda itakapolia, wafu waliolala watafufuliwa kwanza ndipo wataungana na hawa walioko hai kwa wakati huo, ndipo watapaa mawinguni kwenda kumlaki Bwana mawinguni. Sasa, kama tunasema kila nafsi itaonja mauti, na Biblia nayo inasema parapanda itakapolia itakuta kuna binadamu ambao wapo hai watasubiri kwanza wafu wafufuliwe ndipo waungane nao kwenda kumlaki Bwana mawinguni, je, kwanini hiyo kuna baadhi ya watu hawataonja mauti?
 
Hakuna nafsi ya kuonja mauti wala mboga.

Kwasababu nafsi haipo.

Upo wewe na mimi.

Kifo kipo, ni nature na ndio sifa ya kiumbe hai lazima kipitie njia hiyo.

Japo wanasayansi wanaamini kuwa miaka ya mbeleni huko kunaweza kupatikana ufumbuzi wa kurudisha uhai kwa mtu aliyekufa.

Na ndio maana wanajaribu kuhifadhi miili ya watu isiharibike kwa lengo la kuja kuiwekea uhai huko mbeleni itakapopatikana suluhu.
 
IMG_5017.jpg
 
1Wakorintho 15:51 “Angalieni, nawaambia ninyi siri; HATUTALALA SOTE, lakini sote tutabadilika,

52 kwa dakika moja, kufumba na kufumbua, wakati wa parapanda ya mwisho; maana parapanda italia, na wafu watafufuliwa, wasiwe na uharibifu, nasi tutabadilika”.

Hapo 👆 aliposema kwamba hatulala wote bali wote tutabdilika maana yake ni kwamba hatutakufa wote bali wote tutabadilika.
 
Mtoa mada achana na habari zijazo kwanza angalia hata angalia kwanza zilizopita... Kwa mujibu wa biblia Henoko hakufa na Elia pia hakufa. Kwa kuangalia hapo tu unaona huo msemo hauna maana (kwa wakristo). Nadhani waislamu wanaamini hivyo na sisi wakristo tulivyo wepesi wa kudaka vitu hata tusivyovijua tumeiga
 
Wadau, habari ya majukumu bila shaka muwazima wa afya, kama na wale wenye changamoto ya afya, niwaoe pole.

Bila kupoteza muda, twende kwenye mada husika. Hili neno "kila nafsi itaonja mauti," kiuhakika, halijaandikwa kwenye Biblia. Nadhani ni utashi tu wa mwadamu ameamua kutumia hili neno. Sasa turudi kwenye swali letu: Je, ni kweli kila nafsi itaonja mauti?

Kwenye kitabu cha Ufunuo, kinasema parapanda itakapolia, wafu waliolala watafufuliwa kwanza ndipo wataungana na hawa walioko hai kwa wakati huo, ndipo watapaa mawinguni kwenda kumlaki Bwana mawinguni. Sasa, kama tunasema kila nafsi itaonja mauti, na Biblia nayo inasema parapanda itakapolia itakuta kuna binadamu ambao wapo hai watasubiri kwanza wafu wafufuliwe ndipo waungane nao kwenda kumlaki Bwana mawinguni, je, kwanini hiyo kuna baadhi ya watu hawataonja mauti?

Huyo aliyeandika ufunuo unamjua ??
 
Hakuna nafsi ya kuonja mauti wala mboga.

Kwasababu nafsi haipo.

Upo wewe na mimi.

Kifo kipo, ni nature na ndio sifa ya kiumbe hai lazima kipitie njia hiyo.

Japo wanasayansi wanaamini kuwa miaka ya mbeleni huko kunaweza kupatikana ufumbuzi wa kurudisha uhai kwa mtu aliyekufa.

Na ndio maana wanajaribu kuhifadhi miili ya watu isiharibike kwa lengo la kuja kuiwekea uhai huko mbeleni itakapopatikana suluhu.
Kifo ni nature kwamba lazima tupitie kifo bila kujali sababu ya kifo?
 
Mtoa mada achana na habari zijazo kwanza angalia hata angalia kwanza zilizopita... Kwa mujibu wa biblia Henoko hakufa na Elia pia hakufa. Kwa kuangalia hapo tu unaona huo msemo hauna maana (kwa wakristo). Nadhani waislamu wanaamini hivyo na sisi wakristo tulivyo wepesi wa kudaka vitu hata tusivyovijua tumeiga
Hapo mkuu hakuna habari zilizopita bora useme kuna watu hadi sasa hawajafa.
 
Back
Top Bottom