'Kifo Kilimuita Kijoti' - Hammer Q | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

'Kifo Kilimuita Kijoti' - Hammer Q

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Mar 30, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Mar 30, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  'TULIPANGA na Issa Kijoti kwamba ashuke njiani kisha anifuate Makambako ili turudi Songea kwa kazi nyingine binafsi, lakini alipofika Morogoro alisita. Hakujua kama kifo kilikuwa kinamuita', Hayo ni maneno yake mwimbaji mahiri Hammer Q.
  "TULIPANGA na Issa Kijoti kwamba ashuke njiani kisha anafuate Makambako ili turudi Songea kwa kazi nyingine binafsi, lakini alipofika Morogoro alisita, Hakujua kama kifo kilikuwa kinamuita", Hayo ni maneno yake mwimbaji mahiri wa kundi la muziki wa taarabu la Five Stars, Hussein Mohamed 'Hammer Q' alipokuwa anazungumzia vifo vya wanamuziki 13 wa kundi hilo waliofariki dunia kwa ajali ya gari Mikumi Morogoro.

  Hammer Q anasema kuwa yeye alikua ni miongoni mwa wanamuziki waliokuwemo kwenye ziara ya kundi hilo mjini Songea, lakini alishuka Makambako ili arudi tena Songea kwa ajili ya kufanya shoo binafsi.

  "Unajua katika ziara ile mimi na Kijoti tulipata tenda ya kufanya maonyesho Songea. Tulikubaliana vizuri kwamba tutakapofika Makambako tushuke na kurudi Songea. Lakini marehemu alisita na kuendelea na safari na kupata ajali eneo la mikumi kilomita chache kufika Morogoro. Nadhani siku zake zilifika, kama zisingefika haya yote yasingetokea," alisema Hammer Q.

  Mwimbaji huyo anasema kuwa taarifa za vifo vya wanamuziki wenzake alizipata kesho yake, kwani simu yake alikuwa nayo marehemu Kijoti.

  "Kwa kuwa tulikuwa na mpango wa kurudi Songea, simu yangu alikuwa nayo yeye. Nilipiga simu yake haikupatikana, nilipiga simu yangu haikupatikana, kwa hiyo nilidhani huenda zimeisha chaji. Nilipata habari kesho yake, kwa kweli roho iliniuma sana," alisema msanii huyo.

  http://nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsID=5567102&&Cat=7
   
 2. D

  Dopas JF-Expert Member

  #2
  Mar 30, 2011
  Joined: Aug 14, 2010
  Messages: 1,151
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Na wewe Kilimasera una tatizo la jiografia ya Tz, au ni kukosa tu umakini wa habari? Soma kwenye red; ukitokea Songea kwenda Moro unapitia Dodoma? Inawezekana ukifika Iringa ukapitia Mtera kisha Dodoma ikiwa una sababu kubwa. Tunavyofahamu ajali ilitokea eneo la Mikumi sio Dodoma kabla ya kufika Morogoro.

  Asante lakini kwa habari, ila inafaa kuwa na kaumakini fulani
   
 3. JOYCE PAUL

  JOYCE PAUL JF-Expert Member

  #3
  Mar 30, 2011
  Joined: Jan 8, 2010
  Messages: 1,007
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  R.i.p kijoti na wengine.poleni wafiwaa
   
 4. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #4
  Mar 30, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  hahaaaaa mzee ni makosa ya kiuandishi tu nimesharekebisha!!
   
Loading...