Kifo cha WP Johari Shani kimefunua uvunjaji wa Sheria za Utumishi

Hismastersvoice

JF-Expert Member
Jan 26, 2013
18,688
22,273
WP(Woman Police) Johari Shani alijulikana ni mwandishi wa habari wa Uhuru Media, nyuma ya pazia alikuwa mwajiriwa wa jeshi la polisi (Double Agent)!

Taratibu za ajira serikalini unapoajiriwa na chombo binafsi unalazimika kuacha kazi serikalini kwanza isipokuwa tu kama umeazimwa.

Kifo cha WP Johari kimethibitisha uhusiano unaosababisha kulindana kati ya polisi na CCM na kuzaa policcm na ndicho chanzo cha polisi kutumia nguvu kubwa dhidi ya wapinzani.
 
Hivi unajua mpaka pale Ufipa kuna mtu ni askari kanzu pale?

Sent using Jamii Forums mobile app
Hii inanikumbusha wakati ule Chadema walipomzuia mwandishi wa gazeti la Uhuru kuingia kwenye mkutano wa ndani wa chama, kilichotokea ni Chadema kuzongwa kila kona kwanini wamemzuia! Mwenye nyumba anayo haki ya kumkaribisha au kumzuia mgeni.
Vyama vya upinzani viwe makini na waandishi wa habari.
 
Hawakwepeki mbona

Waandishi wa habari huwezi wakwepa ukimkataa huyu yuko mwingine

Dunia nzima iko hivyo CIA wako vyombo vyote vya habari Marekani
 
Nyinyi sasa kila mtu ni mjuaji wa sheria.
Yaani nchi imejaa ma Bush lawyers.

Kila nchi inao mfumo wake wa state intelligence, nyinyi mnapolala na kujamba usiku, hamuelewi kuna watu wanawajibika kuhakikisha nchi iko salama.

Wewe unashangaa mwandishi wa habari kuwa double agent wa serikali.
Hii ni kwa sababu mnao ufinyu wa uelewa kwenye hiyo tasnia.

Utashangaa kama ungeweza kujua kwamba inner circle inafanya kazi kwa weledi mkubwa.

Siku ukijua labda utakaa kimya kabisa....
 
Hii inanikumbusha wakati ule Chadema walipomzuia mwandishi wa gazeti la Uhuru kuingia kwenye mkutano wa ndani wa chama, kilichotokea ni Chadema kuzongwa kila kona kwanini wamemzuia! Mwenye nyumba anayo haki ya kumkaribisha au kumzuia mgeni.
Vyama vya upinzani viwe makini na waandishi wa habari.
Elewa hii
Ndani ya vyama vya upinzani na ndani ya chama tawala kuna mapandikizi wa ujasusi wa kutosha. Tena wengine ni viongozi wakubwa wa vyama hivyo. Na hii ni kwa Dunia yote siyo Tanzania pekee.
 
WP(Woman Police) Johari Shani alijulikana ni mwandishi wa habari wa Uhuru Media, nyuma ya pazia alikuwa mwajiriwa wa jeshi la polisi (Double Agent)!
Taratibu za ajira serikalini unapoajiriwa na chombo binafsi unalazimika kuacha kazi serikalini kwanza isipokuwa tu kama umeazimwa.
Kifo cha WP Johari kimethibitisha uhusiano unaosababisha kulindana kati ya polisi na CCM na kuzaa policcm na ndicho chanzo cha polisi kutumia nguvu kubwa dhidi ya wapinzani.
IMG-20220113-WA0445.jpg
 
Alikuwa mwandishi wa habari wa polisi wa kupeleka habari za polisi Uhuru media kuchapishwa wako kibao wa polisi ambao in waandishi wa kupeleka habari Hata vituo vya TV binafsi nk
Wacha kutetea upumbavu wewe! Kama ni kupeleka habari ndiyo ujitangaze kwamba wewe ni mwandishi wa habari wa chombo hicho? Kwa nini asijitambulishe tu mwandishi wa habari wa jeshi la polisi?
 
WP(Woman Police) Johari Shani alijulikana ni mwandishi wa habari wa Uhuru Media, nyuma ya pazia alikuwa mwajiriwa wa jeshi la polisi (Double Agent)!
Taratibu za ajira serikalini unapoajiriwa na chombo binafsi unalazimika kuacha kazi serikalini kwanza isipokuwa tu kama umeazimwa.
Kifo cha WP Johari kimethibitisha uhusiano unaosababisha kulindana kati ya polisi na CCM na kuzaa policcm na ndicho chanzo cha polisi kutumia nguvu kubwa dhidi ya wapinzani.
Hapo ndiyo nazidi kuamini kuwa ipo siku ambayo ipo karibu sana kuiona ccm ikipotea katika ulimwengu wa siasa.

Haya matukio hayaji bila nguvu ya Mungu.
Mungu anazidi kuwaumbua wabaya wa ustawi wa wananchi wa Tanzania.
 
hii huwa ni kawaida sana, nilishashuhudia askari jeshi wawili ni walimu tena hawavai gwanda wanavaa kiraia tu kama walimu wengine,

halaf ukae ukijua mapandikizi yapo kila sehem hata CHADEMA wamo wa kutosha
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom