kifo cha Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

kifo cha Tanzania

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kimboka one, Oct 31, 2012.

 1. k

  kimboka one JF-Expert Member

  #1
  Oct 31, 2012
  Joined: Jan 23, 2010
  Messages: 734
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  Ndugu zangu ninajua kichwa cha habari hapo juu kina tisha ama kushangaza ila lengo langu nikuona mbele tunapoelekea,niliwa kuandika hapa jamvini habari yenye kichwa Mhe Raisi wangu,nikibashiri hali ya mambo itakavyo kuwa na kushauri njia sahihi ya kuondokana na matatizo yatakayo ikumba nchi yetu,lakini kwa bahati mbaya mhe najua hakupata nafasi ya kusoma wala wapambe wake kama wapo walisoma hawapendi kumpa habari za kuudhi tofauti kumsifia tu.

  Niliyoyasema yote yametokea tena mfululizo kwa kipindi cha muda mfupi sana. Leo ninasema na watanzania wenzangu ambao ninaimani watasoma na kusikia haya ila si kwamba mimi ni mtabiri hasha! Ila ukiruhusu akili zako kufikiri bila ushabika unaweza kuona yafuatayo:


  1. Nchi yetu inaingia katika sura ya ukabila na udini kwa kasi kubwa.Mimi huwa siamini katika kulalamika ila ninaamini kuona tatizo na kutafuta suluhu.
  Nianze na la UDINI hapa ninaona tatizo si waislamu wa la wakristo au wasiona na dini hasha!. Tatizo ni wanasiasa,wanasiasa wameona kukosa mvuto kwa vyama vyao kutokana na wananchi kupoteza imani na utendaji wao ni hatari kwa matumbo yao na kuona kupitia imani za vyama vyao ni ngumu kupata nchi 2015 ndiyo wakabuni njia hii ya KUWATENGA ILI UWATAWALE na njia peke ikiwa ni kupitia udini,mkakati ukatengenezwa kuwa kwanza ni kupanda hasira kwa waislam waone wanaonewa na kuteswa ili watafute njia ya kujikwamua katika mateso hayo na wakaja na kitu kinaitwa mfumo kristo,kauli mbiu hii wakapewa wasaliti wa uislamu ambayo wamejificha kikamilifu katika kuhubiri uislamu na kujijengea heshima ndani ya waumini wa uislamu. hawa ndiyo wamepewa kazi ya kafanikisha mkakati wa kujenga chuki kati ya waumini hawa.wanasiasa wamelenga kuwa 2015 watanzania wasiulize au kutathimini mtu kwa kigezo cha chama ataokacho ila ANATOKA DINI GANI? Na hapo watafanikiwa.

  kwa kusoma upepo ni waumini wa dini gani? Wanaushiriki mkubwa kwenye siasa na wale watakao onekana ni wengi basi wataletewa mgombea wa uraisi wa dini yao na hapo kampeni zitavuma sana makanisani na misikiti ili kuhakikisha muumini mwenzao anapita.


  2.
  Unaweza kuona pia 2015 maandalizi ya mkakati huo namna viongozi wetu wanavyosimamia maswala ya mgogoro wa dini ili wajioshe kuwa hawausiki na kinachoendelea,tazama hapo mbagala nchi iliamia kule gafla,Zanzibar tumeona sote sisemi eti wasijali, haya mbona si tabia yao kujali mambo?.


  3. Unaweza pia kuona athari na kifo cha watanzania na hapa ndipo ilipo hoja yangu kuu,baada ya watanzania kusambaratisha na wanasiasa na mgombea wao kupita kwa kura nyingi wao wanaamini itakuwa kazi raisi kuwaunganisha tena watanzania.ninawaambia tena leo HAITAKUWA KAZI NYEPESI KUWAUNGANISHA WATANZANIA TENA,kovu hilo litakuwa ni chanzo cha msiba mkubwa wa taifa hili, watakao umia ni watanzania wa kawaidi wao hawatahusika ila sisi ambao sasa tutakosa elimu na huduma nyingine za kijamii kutoka nakile kitakachoelezwa kuwa kila dini iwe na njia zao za kutoa huduma kwa watu wao yaani mkirsto hataruhusuwa kusoma shule ya waislamu kadhalika waislamu hawatapata huduma kwa wakisto.

  4.
  Mwalimu nyerere alisema dhambi ya ubaguzi haishi sehemu moja tu! Tukitoka hapo tutajikita kwenye ukabila kwamba taasisi Fulani ni ya kabila Fulani mfano hata kama haitakuwa rasmi lakini itakuwa hivi TRA ya wachaga,UDSM ya wahaya na Tanroard ni ya wanyakusa huo ni mfano tu.tusiombe tufike hapo. Nisiwachoshe ndugu zangu ombi langu tuwe macho sana na wanasiasa na kamwe tusichukiane,TUVUMILIANE ili dunia pawe mahala salama pa kuishi.hawa wanasisiasa ni watoto wa baba mmoja lengo lao ni moja kupata pesa ndiyo maana wote ni matajiri wapo kulinda mali zao.

  Mimi ninaamini Tanzania ina watu wengi sana wazalendo na wenye moyo ila bado hawajajitokeza kutokana na uwezo wao kuwa mdogo na wale wachache waliochomozwa wanakandamizwa na mfumo TAJIRI wa siasa za Tanzania.

  Tuna haja ya kuondoa mfumo tajiri madarakani maana wametuongoza kwa muda sasa tuweke mfumo wa tabaka wa chini lenye watu wanaofanana na sisi wanaojua mazingira yetu halisi.maana mtu amekulia ulaya huko atajua lini? Matatizo yenu?.

  Wao wameshajiwekea mfumo wao wa ulaji ndiyo maana ukitanganza unataka uenyekiti tu! Wanakuchukia maana unaaribu ulaji wao. Tuamke tuisadie Tanzania yetu na tulinde raslimali zetu na tuwapime wanasiasa kwa matendo yao si kwa maneno yake,wengi ni walaghai wa maneno tu.
   
 2. Nazjaz

  Nazjaz JF-Expert Member

  #2
  Oct 31, 2012
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 5,345
  Likes Received: 1,131
  Trophy Points: 280
  CCM ndo INALIANGAMIZA TAIFA LETU
   
 3. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #3
  Oct 31, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Unastuka leo? msome makala za Mohamed Said, tafuta hata humu JF "Mohamed Said", upate picha kamili ya neno "udini" lilianzia wapi na nini kilichosemwa kuwa kitakuwa madhara yake.

  Licha ya Mohamed Said kujitahidi sana kuyaandika na kutowa indhari ya yatakayotokea wengi humu walimshutumu kuwa "mdini", sasa kilio cha nini? tatizo linajulikana na dawa yake inajulikana.
   
 4. k

  kimboka one JF-Expert Member

  #4
  Oct 31, 2012
  Joined: Jan 23, 2010
  Messages: 734
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  zombe tupe dawa
   
 5. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #5
  Oct 31, 2012
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Tatizo lililopo ni watu wachache walifikiri wanaweza kuficha Historia bila kufahamu kuwa itawa hukumu.

  Na waswahili wanasema '' mficha maradhwi, kifo kitamuumbua".

  Kinachotakiwa ni KUHISHIMIANA kwa dini hizo na SI KUVUMILIANA.

  Poleni sana
   
Loading...