Kifo cha ridhaa na kifo cha lazima

Kifo cha ridhaa na kifo cha lazima

mkuu nimekuelewa sana, ukiua kwa kunuia (umekatili maisha ya mtu) ikifika kipindi cha ukomo wa maisha yake kikweli basi mambo yatakuchachia

ivi bro ujawahi kuwa mkubwa wa wanga kweli
 
Tuendelee na mada zetu za ulimwengu wa roho katika upana na ukubwa wake... Habari za vifo vya lazima na vifo vya hiari

Hapa tofautisha na mustakabali (fate) hapa ni tamati ya kukoma kuwa... Kukoma kuwepo... End of existence... Kikomo cha ugiligili kani... Uvutano uliofikia ukomo

Twende kwa mifano rahisi.... Maisha ya nzi baada ya kuzaliwa ni wiki moja... Yaani siku saba ama masaa 168 na kwa dakika ni 10080... Huu muda ukitimia nzi lazima adondoke afe bila hata ya kugusa na chochote... Hiki ndio kikomo cha kuwa.. Ama kuwepo... Hiki kinaitwa kifo cha ridhaa

Nzi huyu huyu akifa kwa njia yoyote ile akifa kabla ya siku saba kutimia anakuwa amekufa kifo cha lazima ambapo kiroho atakufa kamili siku zake saba zikitimia.... Hapo ndio penye utimilifu wa hatima yake...! Sio mustakabali....
Kina kiumbe hai kina life span yake kulingana na udogo ama ukubwa wake.... Kikifa kwa lazima, bado kitakuja kufa kamili hata kama mwili wake ulishaoza na kugeuka samadi ya manyua

Ndugu yangu unayeenda kutafuta tiba mbadala ya matatizo yanayokukabili epuka kwa namna yoyote uwezavyo kutoa roho ya kiumbe hai chochote kwa ajili ya uzima na utatuzi wa matatizo yako.. Makinika kwakuwa huo ni mwanzo wa kuingia kwenye maagano yasiyokoma

Unaweza kufanikiwa sasa kwakuwa kile kiumbe roho yake ingali hai... Lakini itakapofika muda kamili wa roho kutengana na roho kwa ridhaa nawe mambo yako yataanzia kuharibikia hapo....

Ukiwa na kumbukumbu utawahi kwa mtaalam na bila kukwambia ukweli atakwambia kuwa wabaya wako wameanza kukutafuta tena hivyo unahitaji kafara kubwa zaidi...

Makinika na ogopa kabisa kitu kinachoitwa damu.. Shughuli inayohusika na kumwaga damu.. Ule ni uhai ulioondoshwa kwa lazima itafika mahali utaondoka kwa ridhaa na ndio hapo dunia inapogeuka chini juu
Mshana njoo PM mara moja
Dk 3 tu
 
Mshana kila siku naota nipo School wakati nimemaliza long time. What does it mean bro?
 
Mshana kila siku naota nipo School wakati nimemaliza long time. What does it mean bro?
hahah juzi pj wa clouds kalalamika pia anasema yy huwa anaota amefeli mtihani wa form six wakati alishamaliza shule miaka mingi, hop anafanana na wew
 
Back
Top Bottom