Kifo cha MCHINA 1 ni sawa na VIFO VYA WATANZANIA 1000

Upuuzi mtupu wa viongozi wa serikali yetu. Watanzania wangapi wameuawa hapa nchini? Wangapi wameuawa nje ya nchi?
 
Dah hawa eti wawekezaji!! Unafki tu huu inauma hatuna thaman ndani ya nchi yetu!!
 
Idadi ya wachina imeniogopesha. Ukijumlisha na prescence iliyokuwepo naona kweli akili alizokua nazo chief Mangngo wa Morogoro alivyokutana na Carl Peters bado zipo miongoni mwetu. Iwapo tathmini itafanywa ya jinsi wachina walivyowaondoa wenyeji Singapore nakuifanya nchi yao WAKUU Mtatambua kwanini nimeogopa sana leo.
 
Mwe mwe mwe! Maiti zinazozagaa Igunga baada ya uchaguzi mdogo wameshaziongelea au hawana taarifa nazo?? Amemuona mchina tuu rait?
 
Hivi kule china akafa mtanzania itakuwa hivi??????????????????? Aibuuuuuuuuuu nimeshangazwaaaaaaaaa
 
naona mnashangaa tu, sisi wengine hatujui mnachokisema, mchina kapigwa ROBA wapi, mwageni story kabla kutoa mitazamo yenu.
 
Rangi ndugu yangu! rangi nyeupe sijui ina nn kwetu waafrika!

Tukubali ukweli, akili ya mchina mmoja ni sawa na akili ya maprofesa 10,000 wa kitanzania. Kati ya pikipiki 10,000 ni mbili tu zimebuniwa na kutengenezwa na viwanda vya Tz the rest China. Au uwongo?!
 

Kule kwenye migodi ya North Mara wanakufa watu kila iitwapo leo,sijamuona hata mwenyekiti wa mtaa kuhudhuria kwenye misiba hii,tunaposema kuwa kuna tatizo uwa hatuelewi........

hapo umedanganya umma. Ina maana kila siku watu wanauawa? Hizo takwimu umezipatia wapi.
 
Hongera viongozi wangu!

Lazma tuwajali wawekezaji. Nani asiyejua mchango wa wachina ktk nchi yetu.
Kuanzia vifaa vya Electronics hadi majengo.
 
Ndio mtajua mabosi wa nchi hii ni kina nani! Hao mafala na maviwanda yao kwenye eneo la majumba ya watu kuchafulia watu hewa na mazingira waache wafe tu mbwa hao!! Walinzi wao ndio hao hapo kama mlivowaona.

Haiwezekani mbongo akabwe china, watu wenye nyazifa kama hizo zao huko serkali ya china waende kwenye mazishi. Huu ni utumwa wa kileo,yani hizi njaa zetu zitatuua wenyewe..
 
+njaa+umimi+uloho=chamoto tutakiona

Hapana, tuwe wakweli na tuwaambie hawa ndg zetu. Pamoja na kwamba nchi yetu ni yenye amani na utulivu, bado kutakuwepo na uhalifu tu kama zilivyo nchi zote. Ndo maana tuna polisi na magereza pia wafungwa. Mkasa huo umemkuta binadamu mwenzetu na imetugharimu wote bila kujali eneo wala rangi ya mtu. Serikali yetu itachukua hatua kulingana na sheria za nchi kama inavyofanya kwenye uhalifu na mauaji yoyote. Alale mahali pema mama wa kichina. Wote tuseme AMINA.
 
Mnashangaa nini hapa? Hivi katika pikipiki 1,000 zilizopo bara barani leo, ni ngapi ni za kitanzania na ni ngapi ni za kichina? Money matters.
 
Umaskini wetu kama nchi unatuponza sana ni lazima tuwapigie magoti hawa wakubwa,kumbuka ya kuwa mwalimu Nyerere aliwahi kusema ya kwamba adui mkubwa wa binadamu mmojawapo ni umaskini'.Tatizo moja kubwa la umaskini si tu unakosa kujiamini hata kupanga unachotaka ni tatizo

Na umasikini wa MAWAZO au AKILI ni mbaya sana kuliko wooooote!
 
mazishi yamehudhuriwa na waziri wa mambo ya nje benad membe, suleiman kova, salma kikwete NI MAZISHI YA MCHINA ALIYEFARIKI KWA KUPIGWA ROBA lkn watanzania wanatandikwa risasi, wanauwawa kinyama tn na hao wachina, wanakufa kwa kuvamiwa na majambazi sijaona waziri akihuzuria mazishi lbd wafe Watanzania zaid ya 1000, KWA HALI HII SIDHANI!

Ngozi nyeupe inashobokewa kweli na weusi.
Lakini kumbuka ni mwekezaji huyo
 
Back
Top Bottom