Huyu ni mmoja wa viongozi wa kuu wa nchi hii anayesema haya tena kanisani. Kwa nini hakujiuliza ni nini kilicho mfikisha hapo khadaffi? Anasemaje kuhusu wale waliouwawa na khadaffi tena kwa kuwalinganisha na panya, mende n.k, ilikuwa sawa kwake?
Anasemaje kuhusu uongozi na viongozi wa nchi hii wanaofanya ya kufanana na khadaffi, mbona hakukemea? hakuomba hekima ya Mungu akiwa kanisani kuwa aongee nini? Bibilia ina tukataza tusiue na hiyo hiyo inasema anayeua kwa upanga atauwawa kwa upanga, analiongelea je hilo kuhusu yaliyo mpata Khadaffi, wanawe na wapambe wake?
Yeye upambe wake unamwambia vipi akijilinganisha na wapambe wa Khadaffi? Watapona?