Kutoka Fb nawe shiriki hii post,
KIFO CHA GADAFI NI FEDHEHA KWA BARA LA AFRIKA NA KEJERI KWA KIZAZI CHETU, UNITED NATION JITAZAMENI MLIPOJIKWAA
Mimi si mshabiki wa watenda dhambi bali ni mshabiki wa watu wanaojali maslahi ya taifa lao, kama Gadafi alifanya mema kwa maslahi ya Taifa lake, sioni kosa lake, na kama kosa lake ni kugoma kuwapa rutuba mataifa ya nje basi sio kosa na kama kosa ni kukaaa madarakani kwa muda mrefu basi ilitakiwa ashinikizwe kuitisha uchaguzi na kumpindua kupitia matokeo ya uchaguzi.
Lakini sio mtu mweupe aliyetufedhehesha wana wa Afrika bali ni mtu mwenzetu mweusi mwenzetu aliyepewa dhamana na mamlaka katika nchi ya watu weupe na akatupindua Libya, je, Mweupe ana akili sana ameona yeye akimwaga damu atalaaniwa na akaona ni bora amtume mweusi mwenzao akamwage damu au? Mimi sijui na jaribu kutafakari kama tunaweza kusaidiana. Kama Gadafi alikuwa na ugomvi binafsi na familia flani basi wangemalizana wao kwa chuki zao, kuliko kuasiri taifa zima la Libya na wanachi wake. Leo Libya wanamkumbuka Gadafi, yale mema aliyoyafanya sasa hayapo tena, je, huenda walimpindua ilikuweka vibaraka wao? Lakini Gadafi kwangu mimi Yupo hai mbele za Mungu maana ni mmoja ya watu wema katika bara la afrika.
Nchi za magharibi hazina uwezo wa rasilimali bali zinategemea Afrika ndio iwasaidie na kusababisha kuitwa Nchi zinazoendelea kutokana na kupata rasilimali Afrika. Je, kwanini wasituheshimu na wanatufanyia unyama badala ya kutafta mbinu mbadala ya kuepuka kumwaga damu za watu wasio na hatia hasa wananchi. Tusichukiane kisa tumeshindwa kufikia muafaka wa makubaliano ya kimaslahi. Tujifunze kuwa na hekima ya kutatua matatizo, U.N inanafasi kubwa sana ya kubadilisha mfumo mzima wa Kiutawala Dunia nzima lakini yote haya tunatakiwa kupata Katibu Mkuu wa U. N mwenye Hekima na Busara zaidi ya akili zake ili kujenga Dunia nzima katika mfumo safi. Mimi ni Mtanzania niliyeguswa na Kifo cha Rais gadafi lakini sina meno ya kujitokeza hadharani na kusema ukweli wa namna gani tusuluhishe migogoro binafsi na namna gani tulipe kisasi bila kuathiri wengine.
Naitwa DEOGRATIUS KISANDU
Kijakazi Cha roho Mtakatifu.
7 Dec 2016.