Kifo cha Faru Fausta

mbenge

JF-Expert Member
May 15, 2019
4,572
9,808
Faru Fausta akiwa na miaka 57, faru mweusi mwenye jinsia ya kike ameaga dunia siku ya tarehe 27-12-2019 muda mfupi kabla ya kuingia mwaka 2020. Faru huyu maarufu aliyepewa jina hilo, na anayetajwa kuwa alikuwa ni kikongwe zaidi ya faru wote duniani, alitunzwa kwa gharama kubwa na chini ya uangalizi mkubwa wa serikali yetu.

Katika duru na anga za siasa alitajwa sana, ikiwemo na hata bungeni, alijumuishwa pamoja na wenzake Faru John na Faru Ndugai. Kifo cha kimetokea huku habari zake ziki "trend" katika social media mbalimbali na kugusiwa na vyombo vyetu vya siasa. Pamoja na kuwa alikuwa ni sehemu kubwa ya mapato kupitia utalii, lkn wanasiasa wetu wanifunze kuwa na utu zaidi wananchi zaidi ya hayawani hawa wa mituni ambao wanawindwa kwa hali na mali na makundi ya majangili.

Naogopa kutumia neno "buriani" kwa faru huyu, kwa kuwa pamoja na umaarufu wake, bado atabaki kuwa ni hayawani wa mwituni tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom