kimsboy
JF-Expert Member
- Oct 17, 2016
- 9,000
- 17,909
Iran, Uturuki, Russia na India zaitisha kikao Ankara kuipiga teke sarafu ya dola ya Marekani.
Kikao cha "Changamoto na Fursa za Biashara kwa Fedha za Taifa" kilifanyika jana Ijumaa mjini Ankara Uturuki na kushirikisha maafisa na wataalamu kutoka nchi za Iran, Uturuki, Russia na India.
Shirika la habari la IRNA limetangaza habari hiyo na kumnukuu Rasul Khonsari, mtaalamu wa kitengo cha fedha cha Benki Kuuu ya Iran akisema katika kikao hicho kwamba fikra ya kutumia fedha za taifa katika biashara za kimataifa ni dharia mpya inayotekelezeka.
Amesema, hatua ya Marekani ya kuziwekea vikwazo vya kiuchumi Iran, Russia na Uturuki na kuzibana kiuchumi nchi za China, India na Umoja wa Ulaya imepelekea kupata nguvu fikra ya kutumia fedha nyingine za kigeni katika miamala ya kibiashara ya nchi hizo.
Kwa upande wake, Bi Hatice Karahan, mshauri wa Rais wa Uturuki katika masuala ya kiuchumi amesisitiza kuwa, ubunifu wa kutumia fedha za taifa katika mabadilishano ya kibiashara na kwenye uhusiano wa kiuchumi wa nchi zinazostawi itapelekea kupatikana mazingira mazuri huru na ya kudumu ya kibiashara.
Naye Bi Ila Patnaik, mtaalamu wa masuala ya uchumi kutoka India amesema kwenye kikao hicho kuwa nchi yake iko katika juhudi za kutumia sarafu ya taifa katika kufunga mikataba na nchi za kigeni na kwamba hivi sasa inashirikiana kibiashara na nchi sita kwa kutumia sarafu ya taifa.
Kwa upande wake, Marcel Salikhov, mkurugenzi wa taasisi ya uchumi na nishati ya Russia amesema, kutumia fedha za taifa katika biashara na nchi za kigeni kutapunguza kuyumba thamani ya fedha za taifa na kutaleta utulivu zaidi wa kiuchumi katika nchi hizo.