Indonesia, Malaysia na Thailand watangaza kuachana na dola ya marekani

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
9,000
17,909
Kujiunga Jumuiya ya ASEAN na juhudi za kutumia sarafu za kieneo badala ya dola

Sep 02, 2023 02:43 UTC

[https://media]

Kufuatia kutiwa saini makubaliano ya kifedha kati ya Indonesia, Malaysia na Thailand, sarafu za ndani za nchi hizo sasa zitaanza kutumika katika masoko ya biashara ya Jumuiya ya Kusini Mashariki mwa Asia (ASEAN).

Magavana wa benki kuu za Indonesia, Malaysia na Thailand, wakiwa pambizoni mwa kikao cha Mawaziri wa Fedha wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Kusini Mashariki mwa Asia (ASEAN) huko Jakarta, mji mkuu wa Indonesia, wametia saini makubaliano ya kuanza kutumika rasmi na kivitndo sarafu za nchi zao katika mabadilishano ya kibiashara na hivyo kufutilia mbali matumizi ya dola ya Marekani katika masoko ya kibiashara ya jumuiya hiyo. Indonesia ambayo kwa sasa inashikilia uenyekiti wa zamu wa Jumuiya ya Mataifa ya Kusini Mashariki mwa Asia (ASEAN) imeanzisha mfumo wa ushirikiano wa LCT na nchi wanachama wa ASEAN. Mkataba wa LCT ulitiwa saini kati ya nchi kumi wanachama wa Jumuiya ya Nchi za ASEAN na China, Japan na Korea Kusini, kwa ajili ya kupanua ushirikiano wa kifedha wa kieneo.

Moja ya vifungu muhimu vya mkataba huo ni kukuza matumizi ya sarafu za ndani na kupunguza utegemezi kwa dola ya Marekani. Kuhusiana na hilo, Bima Yadhastara, mkurugenzi wa Kituo cha Mafunzo ya Uchumi na Sheria cha Indonesia ambaye pia ni mtaalam mashuhuri wa masuala ya kiuchumi wa nchi hiyo anaamini kuwa uenyekiti wa kiduru wa Jakarta katika Jumuiya ya Mataifa ya Kusini Mashariki mwa Asia ASEAN mwaka huu wa 2023 ni fursa nzuri ya kukuza matumizi ya fedha za kitaifa katika miamala ya kibiashara, ndani ya mfumo wa makubaliano ya LCT. Kabla ya hapo jumuiya nyingine muhimu kama vile Eurasia, Shirika la Ushirikiano la Shanghai na BRICS zimesisitiza azama yao ya kuondoa dola katika miamala ya kibiashara kieneo.

[https://media]Bendera za nchi wanachama wa ASEAN

Nchi kadhaa za Amerika ya Kusini na Kati pia zimekuwa zikifanya juhudi za kufutilia mbali matumizi ya dola katika miamala yao ya kibiashara. Kupanuliwa ushirikiano na nchi mpya kunatajwa kuwa moja ya mipango muhimu zaidi ya serikali ya Indonesia wakati huu wa uenyekiti wa nchi hiyo katika Jumuiya ya ASEAN. Kwa kuzingatia juhudi maradufu zinazofanywa na nchi tofauti duniani kwa lengo la kuondoa dola ya Marekani katika shughuli za biashara za kieneo, weledi wengi wa mambo wanaamini kwamba kufuatia kusainiwa makubaliano ya hivi karibuni ya kuondoa dola ya Marekani katika mabadilishano ya kibiashara ya kikanda, suala hilo litaimarisha haraka matumizi ya sarafu za kieneo katika mzunguko mpana wa mabadilishano ya biashara ya nchi wanachama wa Jumuiya ya ASEAN.

Wakuu wa nchi 10 wanachama wa Jumuiya ya ASEAN hivi karibuni walizindua mfumo wa malipo ya kielektroniki mpakani kwa kutumia sarafu zao za kieneo. Kwa mujibu wa takwimu zilizochapishwa karibuni na Shirika la Fedha la Kimataifa IMF, kufuatia kupitishwa na nchi nyingi za dunia mipango ya kuondoa dola katika mizunguko ya kifedha, hisa ya dola katika hifadhi za fedha za kigeni ulimwenguni ilipungua kutoka asilimia 71 mwaka 2000 hadi asilimia 58 mwaka uliopita wa 2022. Tafiti zinaonyesha kuwa utekelezaji wa mkakati wa kuondoa dola katika miamala ya kieneo na kimataifa unahitaji mlolongo wa usambazaji fedha kimataifa. Iwapo nchi nyingi zitageukia matumizi ya sarafu za ndani badala ya dola na euro katika biashara zao, bila shaka matokeo chanya ya suala hilo yatazinufaisha nchi wanachama wa jumuiya za kieneo zinazonapinga siasa za kujitanua na za upande mmoja za Marekani, ikiwemo jumuiya ya ASEAN. Machapisho ya takwimu za Shirika la Fedha la Kimataifa pia yanaonyesha kuwa uchumi wa Marekani unakabiliwa na hatari kubwa kutokana na kuondolewa dola katika shughuli za kibiashara za nchi mbalimbali duniani. Ni dhahiri kwamba kuendelea mchakato huo kutasababisha uharibifu wa kimsingi katika uchumi wa Marekani na hivyo kutayarisha mazingira ya kuporomoka uchumi wa nchi hiyo ya kibeberu ulimwenguni.

4bpo4a95a2f9e213p4d_800C450.jpg
 
Kwanin kiongozi?
Me naona mifumo ya kielectroniki ikikaa sawa tu tayari inapoteza ushawishi. Kinachochelewesha ni kijenga hii mifumo
Kama nchi zikiendelea na hizi jitihada zao halafu US akakaa tu bila kuchukua hatua zozote, basi hadi kufika 2050 dollar itakua imeanguka.
Swali ni je, hatachukua hatua yoyote? Au hiyo njia wamayoiendea wengi yeye ameshafika anawasubiri?
 
Itachukua muda sana.
Dollar imekita mizizi sana si rahisi kama wanavyodhani.
Labda nchi zote zianzishe huu mfumo lakini si nchi mbili au tatu.
Mchi mbili Tatu kivipi?bona nchi nyingi TU Sasa zimashaazimia kuachana na Dola na kuanza kufanya biashara kwa pesa zao wenyewe?
Ukiangalia nchi hizo zilzoamua kufanya hivyo ni nchi kubwa duniani na Zina ama uchumi mkubwa ama idadi kubwa ya watu
Mafano china,India, Urusi, Brazil,SA,Soud Arabia,Iran, Argentina,Ethiopia,Malaysia, Indonesia, Thailand,misri, Algeria n.k.
Sasa ukiangalia hizi nchi zina uchumi mkubwa na wimbi bado linaendea kwa Kasi ya Hali ya juu mno.
 
Dola kupoteza ushawishi kabisa sio leo wala kesho.
Sidhani kama lengo la kuachana na Dolla ni kutaka ipoteze ushawishi,Bali lengo la nchi nyingi ni kutaka kujikomboa kutoka utumwa wa Dola kua huru kibiashara,kiuchumi na vitisho vya USA.
Nchi nyingi poa zinapendeala kufanya biashara kwa fedha zao .
Hivyo sidhani lengo ni kuifanya Dola ipoteze ushawishi.
 
Itachukua muda kwa dollar kuanguka kabisa! US bado ni dola lenye nguvu kiuchumi.
Naomba nijadiliane na wewe kidogo na kiungwana kabisa kuhusu hoja Yako hapo juu kuhusu Dolla kuanguaka ama kutokuanguka.
Kwanza kabisa Mimi sio mchumi wala mtaalam wa mambo ya fedha ,ila nitajadiliana na wewe kwa kile nachokifahamu.

Kwanza kabisa lengo Kuu la mataifa mbalimbali kuamua kuachana na Dolla sio kutaka Dola ianguke wala sio kwa sababu ya chuki dhidi ya USA au Dola yenyewe,la hasha.

Bali ni kutokana na sababu nyingi sana, lkn moja Kuu ni kuona USA inafaidika zaidi kuliko nchi zinazoitumia.
Hili sio jambo la ajabu,bali
Katika biashara Kuna tabia hii,yaani Kila mtu huangalia faida zaidi kwa upande wake.

Sababu ya pili ni sabau za kisiasa.

Kwa muda mrefu USA imekua ikiziadhibu nchi zinazotofautiana nayo, kwa kuziwekea vikwazo vya kiuchumi ambapo Dola inahusika pakubwa.

Sasa Iko hivi,na kwa mtazamo wangu naiona Dola inaenda kupoteza ushawishi kwa Kasi kubwa mno ingawa itabaki kua moja ya pesa zenye thamani kubwa kwa sababu Marekani ni nchi yenye uchumi mkubwa.

Kwa miaka mingi Dola imekua ikitumika kama pesa ya kati ya kufanyia malipo katika miamala ya biashara za kimataifa au nchi na nchi.

(Natambua Kuna mikataba ya kifedha iliyowahi kufanyika huko nyuma lkn Mimi sitaielezsa hapa wala siwezi kuielezea ,Bali nitaongea kwa lugha nyepesi.ila kama wewe unaweza kuielezea Haina shida,ni mjadala TU.)

Marekani ilifanikiwa kuipenyeza Dola na kuwa katika Hali iliyopo Sasa.

Mfano wa jinsi Dola ilivyoweza kupata umaarufu.

Unataka kununua mitambo au bidhaa kutoka Malaysia,
mafanyabiashara wa Malaysia anajua bidhaa zake Zina uzwa kiasi Gani kwa pesa ya Malaysia.
Wewe mtanzania unao uwezo wa kununua bidhaa hiyo,lakini huna pesa ya Malaysia.
Kinachotokea ,mfanyabiashara wa Malaysia anakuambia ili kukurahisishia, bidhaa yangu inauzwa kiasi Fulani cha pesa ya. Malaysia ambacho ni sawa na Dola kadhaa za Marekani.

Hivyo nawe unatafuta kiasi hicho Cha Dola ya Marekani badala ya fedha za Malaysia na kwenda kutuma Malaysia kwa ajili ya kuagiza bidhaa hiyo.

Sasa kilichotokea .
Kwa ugumu huo ndipo benki kuu karibu zote za nchi hapa duniani ilibidi ziwe na akiba ya Dola kwa ajili ya kusaidia kufanya malipo kwa biashara za kimataifa au nchi na nchi.

Ilikua rahisi hivyo kwa sababu ni ngumu sana kwa benki kuu kumiliki akiba ya pesa ya Kila nchi.ndipo umaarufu wa Dola ulipotokea.

Sasa kwa Nini nasema Dola itapoteza ushawishi lakin haitaanguka?
Kwa vile nchi nyingi zimeamua kufanya biashara kwa kutumia fedha zao maana yake zitaachana na Dola. Hapa ndio kupoteza ushawishi kwenyewe.
Na ni lazima zitaachana nayo kwa sababu ya kuepuka maumivu ya kiuchumi na kisiasa(vikwazo).

Itakua ni rahisi kuiacha kwa sababu hakuna lazimisho la kisheria kuitumia ama kutoitumia,wala hakuna sheria yoyote inayzilazimisha nchi kutumia Dola Bali,ni utashi wa nchi TU na urahisi wa kufanya malipo kutokana na urahisi wa upatikanaji wa Dola.

Nchi zimeanza kuifanyia kazi Hali hii ya kuwa tegemezi wa Dola ambayo kimsingi hata zikifanya biashara nchi mbili tofauti lkni na Marekani nayo inafaidika bila kutoa jasho

Nchi zinahangaika kuweka njia nzuri za kufanya biashara bila kutumia Dola.
Zikifanikiwa kuweka mifumo Yao vizuri basi huo ndio utakua mwisho wa kufanya biashara kutumia Dola.na ndio mwisho wenyewe wa ushawishi wa Dola.

Hata hivyo hii haimaanishi kua doa itashuka thamni ama itapotea ,hapana Bali itapungua katika mzunguko wa duniani.

Kumbuka itakapofikia nchi ikataka kununua kitu kutoka Marekani,Marekani nayo itaitaka nchi hiyo kulipa kwa dola.na Marekani nayo ukitaka kununua kitu nchi nyingine nayo Marekani italipa kwa pesa ya nchi hiyo.lakini hii haimaanishi kama pesa ya USA itashuka thamni Bali itapoteza ushawishi.kwa sababu Kuna nchi zina pesa yenye thamani kuliko Dola lakni sio maarudu kama dola.

mfano katika mabenki ukienda solo la fedha linaondsha fedha kadhaa ikiwemo paundi ya uingereza,yen,euro n.k Kuna baadhi kithamanani Zina nguvu kuliko Dola,lkn Dola ni maarufu kushinda hizo.

Hivyo huko mbele kwa wimbi hili, Dola inaweza kubaki na thamani yake kama ilivyo paund lkn isiwe maarufu kama ilivyo sasa.


Inawezekana

kumbuka miaka ya nyuma nchi za ulaya hazikua na pesa Yao.
Kila moja ilikua na pesa yake.
Lakini walikuja wakaachana na pesa za nchi mojamoia na kuunda pesa Yao euro,ambayo inapigabkazi Hadi Leo.

Hizi nchi zinazoachana na Dola Leo zinaweza zikaja na mfumo mwingine wa kufanya malipo badala ya Dola.

Kumbuka kutumia Dola sio suala la kisheria na kuachana nayo USA hawezi kuifanya nchi hiyo chochote zaidi ya kununa TU. Hata kama nchi hiyo ni ndogo kama Swaziland.

Kwa maoni yangu naungana na wanaoona Dola inaenda kupoteza ushawishi lkni itabakia kua pesa yenye tahamani kama ilivyo euro pound n.k
 
Back
Top Bottom