Kifo cha CCM hichi hapa

Kifo cha CCM hichi hapa

Ritz, US population is over 318 millions na ni Muungano wa 50 STATES.
mleta bado ana hoja.
 
Last edited by a moderator:
kibaka lowasa ndio atawaua ccm.Kuiba anataka na uraisi anataka na ccm haimtaki fisadi gamba gumu lowasa.Mwaka wa Shetani

Tatizo siyo Lowassa,tatizo ni nani anayechagua MWENYEKITI wa CCM,Je ni wajumbe au ni PESA?Kama ni wajumbe sawa lakini kama ni PESA ndiyo inayochagua MWENYEKITI wa CCM basi Lowassa si tatizo hapa,anayechagua MWENYEKITI wa CCM ambaye atasimamishwa kugombea URAIS wa TANZANIA ni MAFISADI..............

Kwa hiyo tatizo ni CC na NEC ya CCM upo kaka?
 
Kamanda mmebadili tena mada? Mwenzio kasema hivi...

Wote walio chukua fomu na kutangaza nia ya kugombea urais niwengi sana na bado wanaongezeka, haijawai kutokea popote duniani ndani ya chama kimoja.

Mimi ndiyo nikamuwekea hiyo orodha.

Hao Wamarekani unaowaongelea, wametangaza tu nia na sıo kwamba wamechukua fomu.Na wenge kwenye orodha wametajwa tu na tetesi za Magazeti.CCM ni wamechukua fomu na wanaenda kwenye kinyanganyiro wote.
 
Ili tuendelee tunahitaji CCM iliyovunjika. Mwelekeo ni huo. Sasa hivi imevunjika kimtazamo (figuratively). Ila baada ya uteuzi itavunjika kihalisia. Huo ndo utakuwa mwanzo wa kuelekea Tanzania imara. CCM ya ujamaa na kujitegemea inachoweza ni kuturudisha nyuma tu na kuliharibu taifa.
 
Du, humu ndani ya JF kweli kuna watu watafiti, wapembuzi na waduduzi. Yaani wameweka list ya wagombea au watangaza nia wa democrats na republican. Kumbe wale wa CCM ni cha motto.

Ukweli ni kuwa pamoja na udhaifu wa CCM katika mambo mengi lakini katika suala la kutoa fursa kwa wote (which can be interpreted to democracy) CCM haina wa kumzidi hapa Tanzania.

Ukiwa wewe ni CUF na ni mfanyakazi wa kawaida (kama ilivyo kwa amos Siyantemi au yule mtu wa Kigoma-waliochukua fomu za urais ndani ya CCM) na ukachukua fomu kushindana na Prof. Lipumba ni lazima utaipatapata na pengine kucharazwa bakora.

Kwa upande wa Chadema muulizeni yailiyompata Zitto alipojaribu kupambana na Dr. Slaa. Wewe ukiwa ndani ya vyama vya upinzani na ukaonyesha upinzani utaipata kama yule kiongozi wa chadema kule temeke.

The fact is vyama vyote vya upinzani nchini mwetu havina internal democracy. Vinazungumzia ufisadi katika nchi lakini vyenyewe vimejaa uozo, upendeleo wa waziwazi na umangimeza. Vimenafanya shughuli na kuongoza kama vile ni ngo.

Kama CUF ina demokrasia ajitokeze mtu na apambane Maalim Seif kule Zanzibar uone kitakachompata. Nchi hii iko hapa ilipo kwa umasikini kwa kuwa hakuna upinzani wenye nguvu.

Hakuna mbadala wa kuingoza nchi hii. Ndio maana CCM wanatamba watakavyo. Yaani katika list ya wale watangaza nia ya urais wa CCM mmoja ndio atakuwa rais wetu.

Hata wapinzani wanajua hivyo na wanasema hivyo. Kwenye majukwaa ya upinzani utasikia huyu ametangaza nia ndani ya CCM hafai kuwa rais na anafaa kuwa jela.

Interpretation and analysis za kauli za upinzani zinaashiria kuwa wapinzani wanafahamu wazi kuwa candidate atakayeteuliwa na CCM ndiye atakuwa rais wetu.

Lipumba hawezi kuwa rais na hata slaa ambaye amepoteza mvuto hawezi kuwa rais.Slaa, after all, hawezi kuteuliwa na UKAWA. Ni aibu kubwa kuwa na vyama vya upinzani kama hivi tulivyo navyo sasa nchini. Unakuta kiongozi wa upinzani kama Lissu, anamtukana father of the nation.

Huwezi kuona katika nchi walizostaarabika wanamtukana mtu aliyeaasisi taifa. Pamoja na mapungufu ya Lenin huwezi kuona Urusi wanamtukana waziwazi mtu huyo aliyeanzisha taifa la Soviet Union.

Slaa anakwenda ziara ya nje anaanza kubwajabwaja ubaya wa Tanzania. Wazungu wanapomshangilia kwa makofi anadhani wanafurahia kumbe wanamuona ni mtu wa ajabu kutoa siri za ndani.

Eti aje hapa mpinzani wa Russia au Marekani au Uingereza aanze kubwajabwaja udhaifu wa nchi yake. This country is in crisis na wapinzani have a role in this mess. Wababaishaji wakubwa.
 
1954

Kwa heshima na taadhima naombeni wakuu mnifahamishe maana na asili ya neno hili "mangimeza". Seriously
 
Last edited by a moderator:
Kwa hali ilivyo ni wazi kabisa kwamba chama cha mapinduzi CCM kinaenda kusambaratika endapo busara hazitatumika,kuna mambo makuu mawili ya kuua chama.

1.Lowassa,yeye ni sababu ya kwanza kufa kwa chama,maana yeye anasema lazima ateuliwe kugombea urais kupitia CCM asipoteuliwa hakubali kwa maana hiyo atahama chama pengine ameshakiandaa ili akagombee urais huko na wakati anahama chama anaondoka na kundi kubwa la wanaccm wanaomuunga mkono.

2.Ufisadi,ndani ya CCM kuna wanachama wamepewa alama kama mafisadi na wanachama wenzao na wote wako kwenye kinyanganyiro cha urais,hivyo basi kama CCM itampitisha mgombe mwenye doa la kifisadi basi kuna kundi kubwa la wanaccm watoondoka CCM kwa madai ya kwamba hawawezi kuunga mkono mafisadi hivyo nao watajiunga na chama chochote ili wamwangushe huyo fisadi.

Kwa maana nyingine CCM mwaka huu lazima iwe tayari kupokea Matokeo ya uchaguzi mkuu kwa namna yoyote yatakavyokuwa.
 
Lililopo ni kusanyiko la masalia ya ccm, yenyewe iliondoka na mchonga meno.
 
Na nyie na Lilowassa lenu, wacha CCM isamabalatike kwani nini?
 
Hata hivo mabadiliko haya ya kisiasa yanapoendelea kutokea watanzania tuendelee na umoja wetu wa kidini,na kijamii tusikubali kugawanywa na hawa wanasiasa,japo kila nikiangalia umasikini wa wananchi wengi unaotokana uongozi mbovu unaotokana mfumo mbovu naumia kwa kweli.
 
Mwambieni chama hakifanyi maamuzi kwa kuogopa vitisha vya mtu, chama kinafanya maamuzi kwa kufuata vigezo 13 tulivyojiwekea baasi, no alternative, no shortcut
 
Lowasa siku akitoka ccm ndio mwisho wake kisiasa. Hao watu anaodai ni wafuasi wataendelea kuwa wafuasi ndani ya ccm na si kwingineko. Atashangaa siku anaondoka atakuwa peke yake na pengine wafuasi kiduchu. yangu macho.
 
Hivi lowassa ni nani hadi aitishie nchi kishamba hivyo?...
 
Ccm ilashakufa ktambo sana! Hv sasa tuna andaa jeneza na shimo mwezi oktoba ili tuizike kabisa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom