Kifimbo cha Malkia wa Uingereza Chatua Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kifimbo cha Malkia wa Uingereza Chatua Tanzania

Discussion in 'Sports' started by MziziMkavu, Jan 3, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jan 3, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,611
  Trophy Points: 280
  Kifimbo cha Malkia wa Uingereza Chatua Tanzania
  [​IMG]
  Rais Kikwete akiwa amekishikilia kifimbo cha malkia wa Uingereza Wednesday, December 30, 2009 2:15 PM
  Kifimbo cha malkia wa Uingereza ambacho kitashindaniwa katika mashindano ya 19 ya nchi za Jumuia ya Madola yatayofanyika nchini India mwakani kimewasili Tanzania. Rais Jakaya Mrisho Kikwete amekipokea kifimbo cha malkia wa Uingereza ( Queen Baton) ambacho kitashindaniwa katika mashindano ya michezo ya 19 ya Jumuia ya Madola yatakayofanyika Delhi nchini India.

  Mashindano hayo yatakayoshirikisha nchi 71 ikiwemo Tanzania yataanza mwezi wa kumi mwakani.

  Akiongea wakati wa hafla ya kukipokea kifimbo hicho ikulu, rais Kikwete alisema kuwa anatarajia kumleta kocha wa riadha wa mbio fupi kutoka Jamaica kwa ajili ya kurudisha heshima ya michezo nchini.

  Wakati wa ziara yake nchini Jamaica mwezi uliopita, Rais Kikwete alipata nafasi ya kuzungumza na mwanaridha Usain Bolt na Asafa Powel na kugundua siri ya mafanikio wanayoyapata ni maandalizi ya muda mrefu na kugunduliwa mapema kwa vipaji.

  Aidha rais Kikwete alisema anashangazwa na michezo kushuka nchini ingawa amefanikiwa kuwaleta makocha wa michezo kama riadha ngumi na judo ambako anatarajia kuona mabadiliko kupitia makocha hao.

  Rais Kikwete pia alielezea kushangazwa kwake na kudorora kwa michezo ingawa ameruhusu michezo mashuleni sambamba na majeshini kulikowaibua wachezaji kama Filbert Bayi, bondia Titus Simba na Kanali Juma Ikangaa.

  “Tanzania ina historia ya kufanya vizuri kwa sababu miaka ya 1970 na kuendelea ilikuwa tishio lakini sasa hivi inashangaza pamoja na kuleta makocha kutoka nje hakuna mafanikio,” alisema rais Kikwete.

  Rais Kikwete alisema ujio wa kifimbo hicho ni changamoto kwa wachezaji wetu kujiandaa vilivyo na kuondokana na sababu kama ilivyo katika soka kwamba mwamuzi aliwahujumu au kocha. GONGA HAPA KWA PICHA ZA HAFLA YA KUWASILI KWA KIFIMBO CHA MALKIA
  http://nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsID=3831902&&Cat=1
   
 2. M

  Mbunge wa CCM JF-Expert Member

  #2
  Jan 3, 2010
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 476
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nakubaliana na mzee mwanakijiji kuwa imebaki kuletewa gagulo la malikia, na si ajabu likapokelewa na mkulu wa kaya!!!!!!!! mi simo!
   
Loading...