Maandamano yamezidi kushika kasi katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi, siku ya Alhamisi, ambapo magari yalichomwa moto na polisi walifyatua mabomu ya machozi kuwatawanya waandamanaji waliokuwa na hasira kufuatia kifo cha mwanablogu wa kisiasa aliyefariki akiwa mikononi mwa polisi wiki iliyopita, kwa mujibu wa picha za Reuters TV.
Kifo cha Albert Ojwang mwenye umri wa miaka 31, ambaye alikuwa akiandika kuhusu masuala ya kisiasa na kijamii, ni tukio la hivi karibuni kuibua tena mjadala kuhusu vitendo vya vyombo vya usalama nchini humo, ambavyo kwa miaka kadhaa vimekuwa vikishtumiwa kwa mauaji ya kiholela na utekaji nyara wa kulazimishwa.