Kifanyike kitu gani watu wadumu kwenye ndoa?

Heloo

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
4,391
3,402
Habari zenu!
Nina maswali kidogo..kuhusu ndoa Na mahusiano kwa ujumla.Unakuwa watu wamependana wenyewe wakafunga mpaka ndoa, ama wapo kwenye uhusiano..

Baada ya Muda Ni ugomvi, kusalitiana, huyu ana mteta huyu, siri zinaanza kutolewa, jamani ndugu zangu.Ni nini hasa kinachosababisha ?? Sio wote lakini nashawishika kusema ni Tatizo la Dunia.Mfano.Mfano.Unaweza sema sababu ya pesa( kuna wanaopewa kila kitu but ndoa/ uhusiano unavunjika!

Kuna wanaobembelezwaa na kuenziwaa uhusiano unavunjika( nikawaza au ni maumbile?? Labda unapendana na mtu kwa nje( siku mnalala wote unakuta bwawa au kibamia?? Au siooo? Au Sio bwawa Sio kibamia but wana achana Na wengine kufikishana Mpaka police kwa wajumbe.

Je Hakuna mjadala wowote Ili kujifunza Walau kuponya kizazi Na vizazi vijavyo? Kumbukeni Mapenzi yana nguvu yakitumika vibaya ndo chanzo cha watoto wengi wa mitaani.Je Tufanye nini??
 
"nikiacha kuchepuka,nikiridhika nayeye kwa kila kitu, akiniheshimu akinithamini tukimtanguliza Muumba katika mambo yetu hakuna litakalo tuahinda"


Somebody said......
 
Jando na unyago vilisaidia pia ...lakini kwa sasa elimu ya kidini ndo muhimu kwa pande zote mbili ili kuweka uwiano katika mahusiano..na kutowapa sana wanawake vichwa juu ya mwanvuli wa haki sawa mana hiki kitu upande mwingine kinawapa viburi wanawake wanaanza kujilinganisha na wanaume....na wanaume kutimiza majukumu yao ipasavyo..ie...kuhudumia familia,kumtunza mke,tendo la ndoa na kuwa na misimamo dhahiri juu ya asichokipenda juu ya mwanamke.....ELIMU YA DINI NI MUHIMU KULIKO YOTE( KUMJUA MUNGU)
 
Wanandoa wajifunze kumuhusisha Mungu katika mambo yao... Wengi wanajiendesha kwa akili zao na tamaa zao... Ukimuhusisha Mungu kuanzia kwenye kutafuta mwenza mpaka kwenye ndoa mtahimili changamoto zote...
 
Ndoa ni sawa na kula chakula aina moja kwa maisha yako yote,ndo maana inafikia mahali ukishakinai vijisababu visivyo na maana vinapelekea maugomvi.
 
Tafuta Ukuta Ndani Kwenu Uandike Ndoa Baada Ya Hapo Chukueni SuperGlue Ndoo Nzima Jipakeni Alafu Kajibandike Kwenye Ilo Neno Ndoa. Hakika Mtadumu Milele.
 
Ila vijana inabidi baadhi yao wapewe elimu kabla ya kuamua kuingia katika mahusiano na baadaye ndoa...
Kwasababu mimi naamini kuwa endapo umeridhia kuishi au kuwa katika mahusiano means huyo uliye naye ndiye anayekufaa pekee kati ya wale mamilioni uliyowaona au kuwatumia je, haya masuala ya kutafuta au kuangalia pembeni yanatoka wapi?

chagua vyoote unavyotaka wewe kuchagua ila ikifika kwenye suala la mahusiano

''CHUNGA USIJE JILAUMU/ KUJUTIA MAISHA YAKO YOTE''

mimi yangu ni hayo
Muda mwema kwenu
 
Tangu zamani ndoa haijawahi kuwa rahisi.Uzinzi,usengenyaji,umasikini,vibamia,mabwawa na vyote hivyo vilikuwepo tu. Kinachofanya tofauti kwa sasa ni kumomonyoka kwa maadili tu. Zamani watu walikuwa wanaona aibu,nikiacha mke/mume ni aibu ya ukoo mzima, na hakuna mtu angenielewa kabisa. Lakini sasa ule muunganiko wa ukoo na familia haupo tena. Kila mtu anafanya anavyo jisikia.
 
Vijana wengi wanaofunga ndoa hawako serious wengi wao wanafuata mkumbo tu kuona rafiki zake wameoa au kuolewa naye anataka bila kufikiri mara mbili kuhusu ndoa yenyeweee, wengine wanakuwa na matarajio fulani wakiyakosa ndio yanaanza mengine
 
Habari zenu!
Nina maswali kidogo..kuhusu ndoa Na mahusiano kwa ujumla.Unakuwa watu wamependana wenyewe wakafunga mpaka ndoa, ama wapo kwenye uhusiano..Baada ya Muda Ni ugomvi, kusalitiana, huyu ana mteta huyu, siri zinaanza kutolewa, jamani ndugu zangu.Ni nini hasa kinachosababisha ?? Sio wote lakini nashawishika kusema ni Tatizo la Dunia.Mfano.Mfano.Unaweza sema sababu ya pesa( kuna wanaopewa kila kitu but ndoa/ uhusiano unavunjika! Kuna wanaobembelezwaa na kuenziwaa uhusiano unavunjika( nikawaza au ni maumbile?? Labda unapendana na mtu kwa nje( siku mnalala wote unakuta bwawa au kibamia?? Au siooo? Au Sio bwawa Sio kibamia but wana achana Na wengine kufikishana Mpaka police kwa wajumbe.
Je Hakuna mjadala wowote Ili kujifunza Walau kuponya kizazi Na vizazi vijavyo? Kumbukeni Mapenzi hana nguvu yakitumika vibaya ndo chanzo cha watoto wengi wa mitaani.Je Tufanye nini??
hakuna sababu moja unaweza kuitaja ili kudumisha ndoa ila siri ya ndoa nyingi kudumu licha ya kugombani ni uvumilivu, kusameheana na kuheshiana....basi ni hayo tu.
 
Back
Top Bottom