Kidonda sugu kwenye ankle

Kisusi Mohammed

JF-Expert Member
Aug 10, 2009
563
468
Habari za majukumu wakuu, mi nimekuwa na tatizo la kidonda kilichosababishwa na ajali ya pkpk tokea mwezi wa 11 mwaka 2009, nimeshatumia tiba za kila aina mpaka skin grafting nilishafanyiwa lkn cjapona! Naombeni msaada wa dawa za kutumia ili kidonda kipone maana kimekuwepo kwa miaka 2 sasa! Ntashukuru kwa msaada wenu!
 
Jamani wana Jf doctor mbona mpo kimya kuhusu hili suala langu!? Naombeni msaada wenu jamani, nina hali mbaya sn!
 
ASALI DAWA YA VIDONDA
Tangu enzi na enzi, asali imekuwa ikitumiwa na mababu zetu kama chanzo cha nishati ya mwili, lakini pia katika utafiti wa hivi karibuni, imegundulika kuwa asali ina ewezo mkubwa sana wa kuponya vidonda vya aina mbalimbali kutokana na viambata vyake kuwa na uwezo wa kukausha maji haraka kwenye kidonda.

Aidha, virubisho vingine vilivyomo kwenye asali vina faida kubwa kwa wana michezo kwani huongeza nguvu na wana michezo wengi wamekuwa wakitumia vyakula vitokanavyo na asali au vyenye mchanganyiko wa asali na wameona mafanikio makubwa.

Pakaa Asali Safi ya nyuki kwenye kidonda chako kutwa mara 2 asubuhi na usiku tumia mpaka hicho kidonda kipone. Au Tumia hii Dawa unapoamka Asubuhi ukikojoa mkojo wako jipake kwenye kidonda kwa muda wa siku 21 utapona inshallah. Na jambo muhimu nenda hospitali kapime Damu na mkojo huenda una maradhi ya kisukari ndio maana ahicho kidonda huwa hakiponi pole sana. tumia unipe FeedBack P.h.D. MziziMkavu
 
Pamoja na kutumia asali lazima usafishwe kidonda hosptal kwa kutumia gauze sterile,na kisha unaweka asali baada ya kusafishwa na kifungwe kwani ukikiacha wazi inzi na wadudu wengine watatua kwenye kidodnda na kuacha wadudu wengine kufanya kidonda kisipone.

Pia ukumbuke kuwa skin graft haiwezi kushika kwenye kidonda ambacho si kisafi sana,pia wakati kikifunguliwa baada ya grafti watalaam wengine wa afya hujariburibu kusafisha kwenye grafti kama vidonda vingine matokeo yake ngozi hiyo huanza kuachia mwishowe kidonda hurudi tena.

Kinachotakiwa ni kupangusa tu kwenye grafti mpaka inashika,nilishaona watu wana vidonda vya muda mrefu lakini walipona solong as huna kisukari, HIV kwani kupona kwa vidonda inakuwa ngumu kwao japo wapo hupona pia.
 
Back
Top Bottom