Kidela: Hadithi Fupi

Muddyb

Member
Oct 21, 2010
39
30
STORI ZA KUPIGA RAMLI!
Mtunzi: Muddyb Mwanaharakati
Mawasiliano: 0713538427

ANGALIZO: Atakayekwazika, naomba ani-inbox. I will have the post deleted immediately!
Kingine si kama stori ndivyo hali halisi ilivyokuwa. La hasha. Ni katika harakati za kusogeza siku zetu za kuishi tu.

Tuendelee. Kesi sitaki!

Kaka wawili wameketi kibarazani kwao maeneo ya Kariakoo wakitayafakari ya dunia yanavyoendelea. Mmoja alionekana kutopea mawazoni kupitia kiasi.
Hali ambayo iliamsha maswali mengi kichwani mwa mdogomtu.
"Ka' mbona ka' vile umevurugwa?" Aliuliza mdogomtu. Kakamtu akageuka kumtazama mdogo wake. Akatikisa kichwa kuoneshwa kusikitishwa na hicho alichokuwa akikiwaza.
"Dunia tu, mdogo wangu."
"Dunia imefanyaje?"
"Dunia si mbaya!"
"Mbona sikuelewi sasa?"
"Huwezi kunielewa, mdogo wangu!"
"Ila?"
"Walimwengu wabaya!"
Mdogomtu hakutaka tena kuuliza maswali mfululizo. Walikuwa wameketi mbalimbali kidogo. Akajitoa pale alipo na kusogelea karibu kakaye.
"Haya, naomba anza upya kabisa. Huo ubaya wa dunia na watu wake," alisema mdogomtu. Kakamtu akacheka. Cheko la kulazimisha. Machoni alionesha kuumizwa sana na hilo jambo.
"Kwani una kazi gani sasa hivi?" Kakamtu aliuliza.
"Kazi gani kiaje sasa?" Mdogomtu alijibu.
"Ya muziki. Ratiba zako zikoje?" Kakamtu aliuliza tena.
"Si ngumu sana. Vipi unataka tufanye ngoma pamoja?" Mdogomtu aliuliza.
"Ndiyo. Iwe kioo cha niliyotendewa," kakamtu alijibu. Lakini jibu lake lilikuwa nusu kwa mujibu wa akili ya mdogomtu.
"Kuna ubaya gani ukiniambia huyo aliyekutendea? Ni kipi hasa cha kufuta nafsi hata kupelekea mishipa ya shingo ukitoke?" Mdogomtu aliuliza. Kaka akashusha pumzi kubwa mno—mithili ya mtu aliyekuwa anakimbizwa.
"Sawa. Nitakueleza!" Alisema kakamtu.
"Unamkumbuka yule mtoto domo kutoka ufalani kule sijui Tandale sijui Manzese—mi' sijui kwao. Unamkumbuka?" Kakamtu alieleza. Dogo akamgeukia uzuri mdogo wake. "Ndiyo namkumbuka. Kafanyaje?" Dogo aliuliza.
"Ina maana hujasikia kilichotokea huko barobaro au nd'o kusudi zako tena?" Kaka alisema.
"Nimes'kia, lakini hukufunguka mwenyewe. Hivyo si vibaya ukinieleza kila kitu," alisema mdogomtu.
Kaka akatafakari kiasi, kisha akainua kichwa na kumtazama mdogo wake pasi kupepesa macho. "Yule mtoto ni mshenzi!" Kaka alisema.
"Kwanini?"
"Sama yangu mimi, asingekuwa maarufu. Leo hii ananiponda na kusema mi' mwanamuziki wa kitambo sijulikani kama anavyojulikana yeye? Kwamba atahakikisha sisikiki katika uwanja wa muziki? KWELI? 'Akati anatumia studio yangu kurekodi nyimbo zake zote?" Kakamtu alisema akilia. Chozi fupi lilimdondoka.
Mdogomtu akamtuliza kakaye.
"Sasa umeamuaje?" Mdogo mtu aliuliza. "Nimemfukuza studio. Asije tena na wala si sehemu ya barobaro," alijibu kaka. "Aah, kumbe!" Dogo alichagiza.
"Yeah!" Kaka alijibu.
"Hiyo ngoma ilihusu nini ulotaka kufanya nami?" Dogo aliuliza.
"Kuhusu wanadamu na dunia!" Kaka alijibu.
"Ebu nipe mstari mmoja kidogo," dogo alisema. Kaka akacheka. Shavu zikatoa dimpozi ka' ndimu changa.
"Nimepata kuandika kipande tu," kaka alijibu. "Hicho-hicho kipande em nipe kwanza," dogo aliongeza.
"Muogope Mungu, domo! Dunia mapito, domo!" Kaka alianza kuimba. Mdogo akacheka. "Unacheka nini sasa. Mpuuzi nini wewe?" Kaka alifoka. "Sio hivyo, kaka. Sasa hiyo domo itaonekana kabisa unamlenga nani.... hahahahaha," dogo alisema huku akiangua kicheko.
"Unataka jina gani sasa?" Kakamtu alisema.
"Mmmmh, labda Kidumu? Kibaka? Au Kiduku, sijui Kidela?" Tusitaje moja-kwa-moja mifano ya watu watajua tumewalenga wao," mdogomtu alisema. Kaka akaonekana kutafakari juu ya hilo.
"Kweli kabisa. Naona Kidela limekaa sawa zaidi," alijibu kaka. "Basi Kidela," mdogomtu naye alikubaliana na wazo hilo. "Bado ndani, tuweke maneno. Umesema ulimtendea wema halafu kakufanya vibaya bila kukushukuru sio?" Alisema mdogomtu. "Ndiyo. Na matusi juu!" Kaka mtu alisema.
Dogo akaenda ndani. Akarudi na kijitabu kidogo cha kuchukulia taarifa muhimu. Kijitabu cha kuenea kiganjani tu. "Naomba utangulizi uwe, 'Muogope Mungu, Kidela! Dunia mapito! Kidela, mbele kuchungu, Kidela! We chunga sanaa!" Mdogo mtu alisema. Akamtazama kakaye. "Unaionaje hiyo?" Aliongeza mdogomtu.
"Hiyo iko bomba sana. Em hiyo tuifanye kama kiitikio badala ya intro. Unasemaje?" Kakamtu alisema. Dogo akaitikia kwa kichwa.
"Enhee, endelea," kaka alisema.
"Ngoja kwanza. Nimepata wazo... sikia hii."
'Tenda wema uwende zako, usingoje malipo,
Hii dunia sio yako oooh!"

Alisema mdogomtu. Kaka mtu akazidi kufurahi. "Tuongeze neno, 'Kidela!" Alisema kakamtu. "Sawa. Imezidi kupendeza," alisema mdogomtu. Dogo akaendelea.

"Kuishi nawe miaka yote, sisi kama ndugu zako. Ukaiabisha nafsi yakoo ooh, Kidela!" Dogo alisema akatulia. Akamtazama kakaye. Kaka akampa ishara ya aendelee kuandika.

"Binadam haonekani mwema mpaka wemaa, wayasemeee memaa." Dogo akaongeza; "Kutulipa yakoo memaaa uliosemaaaa kwetu si memaaa," dogo alimaliza. Akajipa hongera mwenyewe. Kakamtu akacheka sana. "Nd'o umemaliza hapo?" Kakamtu aliuliza. "Bado, ngoja niongeze mistari. "Kutusemaa kila koona unayookwenda sisi si wemaaaa. Kuishii nawe miakaa yootee tulichovuna nawe ulivunaa hii. Dunia si mbayaa. Kidela. Walimwengu ndio wabaya. Kidela!" Akahitimisha. Wakagongeana tano.

Furaha imemwagika mioyoni mwao. Hapana kwa kweli. "Bado ya kufungia hapo. Em weka ya kufungia kwanza," kakamtu alisema. "Sawa," dogo aliitikia. "Hii Dunia si mbaya. Kidela. Binadam Wabayaaaaaaa," aliimba kwa sauti kubwa hata wale watu waliokuwa wakipita walishangaa.

Wakacheka tena kujipongeza. "Zamu yako sasa!" Dogo alisema. "Ngoja nioneshe ujuzi wangu sasa kama mi' kwenye gemu tangu 2004 enzi hizo "Nalia" kabla ya kufuga "Njiwa" na kesi ya Macmuga kwenda Afrika Kusini. Oh nisisahau kama nimewahi kuwadithia 'Hadithi," alisema kakamtu.

Dogo akawa anamtazama kwa majivuno na mbwembwe tele. Dude wamelipatia kwa ajili ya domo kutokuwa na shukrani. Kaka akaanza. "Jeuri ya nini, sote tuko chini ya juaaaa. Ubabe wa nini, hata we' pia umezaliwa. Ungejiza mwenyewe, apo sure," alisema kaka kisha akatulia. Alionekana kuwaza mstari wa pili.

"Vipi tena, unawaza visa vyake nini?" Dogo aliuliza. "Ndiyo," kaka alijibu. "Kumbuka kile kibaya zaidi!" Dogo alisema. "Kwanza alisema mi' kibamia. Pili eti mfupi sina mvuto. Lakini hiyo nshajibu juu huko katika mistari yangu. Niongeze kipi?" Kaka alisema. Alionekana kugota mwisho kifikra. Dogo akaanza kuwaza na kuwazua.

"Weka mstari wa kukomesha maneno yake." Dogo alijibu. "Kivipi?" Kaka aliuliza. "Yaani, awe na adabu. Kama hawezi kuumba, basi hana uwezo wa kuumbua!" Dogo alisema. "Anhaa!" Kaka mtu aliitikia. "Ndiyo." Dogo alichigaza. Kaka akarudi tena kitabuni. "Sawa, cheki hii," kaka alisema.

"Kijana chungaaa saaanaaa," kaka alisema. Dogo akatikia kwa kichwa kuonesha yuko sawa na mstari huo. "'Afu huyo dogo anaonekana mtu wa kujikweza sana eh?" Dogo alisema. "Ndiyo. Ana majina kibao. Hadi wanyama na mengine yetu hapa kaamua kujiita yeye," kaka alisema kwa ghadhabu. "Basi mwoneshe unyama wako katika mistari na rejea tena suala la kimaumbile," alisema dogo. Kakamtu akacheka kisha akaendelea kuandika.

"Kama we mnyama, mi' mnyama pia. Zaa wako umpangiee sheriaa. Binadam haonekani mwema mpaka weema wayaseme mema. Kutulipa yako memaa uliofanya kwetu si memaaa. Kuishi nawe miaka yote tulichovuna, nawe ulivuna," kakamtu aliimba.
"Hiyo funika bovu! Naona huko aliko domo akilisikia hili atatafuta chimbo la kujisaidia!" Dogo alisema. Kaka akacheka. Wakagongesheana. "Kwanza anavyopenda kutunga mapenzi kila siku—hana lolote umalaya tu," dogo aliongeza. Kaka alikaa kimya tu.

Wakachukua karatasi zao na kuzitunza vyema kabisa. Baada ya wiki, wimbo ulitoka. Wakafanya video na jamaa moja aliyeitwa Maringo Lab na ndani ya video walionesha dhahiri tabia ya domo kwenda kwa waganga, kusema vibaya wenzake, kujiona mjuaji na madhala ya fitina.

MWISHO!
#SamahaniLakini
 

Similar Discussions

1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom