Bujibuji Simba Nyamaume
Platinum Member
- Feb 4, 2009
- 79,036
- 168,670
Jana baada ya kazi nikasogea maeneo fulani ili kuisindikiza jioni na kukwepa foleni za jiji la mafujo.
Nikiwa busy nakunywa huku nikiwaza kwa lugha za kigeni, mara akatokea msichana mlimbwende aliyeumbwa akaumbika.. Ukimwangalia ni kama chotara wa malaika na mwanadamu mweusi. Mtoto ana rangi ya mpodo, akili zikaniganda, nikashindwa hata kuelewa kati ya A na Z kipi huwa kinaanza.
Nikasema sitaki presha, wacha huyu mrembo nimwache na hamsini zake, huenda amekuja kumsubiri mtu wake.
Nikiwa naendelea na unywaji wangu, ghafla sauti nzuri nyororo ikapenya masikioni, samahani kaka Bujibuji naomba uniazime kidadavuzi mpakato chako niangalie kidogo JF.
Nikapigwa na butwaa, nani huyu anayenifahamu kwa jina? Nikamwambia karibu, memba mwenzangu we ni nani kwani?
Malaika akajibu, mi Madame B, dah......
Madame B kaumbika jamani, nikajikuta naaga huku nikiwa nimesahau kabisa habari za kidadavuzi mpakato, akili zisha hama, mapigo ya moyo yamehamia kwenye kidole cha katikati ya bustani ya Eden.
Bujibuji umesahau kidadavuzi mpakato chako......
Nikajikuta naongea bila kujielewa, wee baki nacho tu mi ninavyo vingine nyumbani.
Akili kukaa sawa najikuta niko kitandani, yote yalikuwa ni ndoto tu.

Last edited by a moderator: