Kwangu tatizo sio mchago wa 10,000, shida inakuja hiyo michango itaboresha sekta ya elimu? au ni miradi mingine kwa ajili ya wakurugenzi kutumia kwa ajili ya kisiasa?
Michango mingi inatolewa mfano BRN Speed kila mtoto anatakiwa atoe sh 500 kila siku kwa ajili ya mitihani na 1000 kila jumamosi haina faida yoyote kwani mtoto kwenye pepa amepata ila ukimwambia alirudie swali hawezi!
Na wakilwa kwenye majukwaa wanasema elimu ni bure,, hili jambo ni la kisiasa zaidi kuonyesha mmejenga maabara?
Sasa niwaulize maabara ni jengo au ni vifaa??
Wanunue vifaa kwanza sio kutujengea majengo ambayo hayatakuwa na faida yoyote kwani watasema vifaa hakuna