Kichere umeingia Mtego wa Timothy Apiyo

Stuxnet

JF-Expert Member
Feb 12, 2011
10,422
18,056
Timothy Apiyo (RIP) aliyekuwa Chief Secretary wa State House enzi za J K Nyerere aliwahi kufanya makosa Kama haya ya CAG Kicheere.

Watendaji walileta mapendekezo ya kuboresha mafao ya kustaafu. Lakini yeye akayapiga chini enzi hizo yuko ofsini na ni kijana.

Hatimaye kwenye miaka ya mwishini mwa 2010 hivi kabla hajafariki aliwahi kuilalamikia Serikali kwenye ITV juu ya mafao madogo ambayo yanawafanya wastaafu waishi kwa shida na mateso.

Alisahau kabisa kuwa yeye mwenyewe miaka ya 1980s ndiye aliyekataa mapendekezo ya maboresho

Naye Charles Kicheere amesahau kuwa hana miaka 5 atakuwa mstaafu pia.
 
NHIF imekuwa inashindwa kuhudumia wateja wake kutokana na Ufisadi, serikali kukopa hovyo, kukopesha hovyo na wizi wa viongozi wake na sio michango ya wateja wake kuwa kidogo!

Lakini Charles Kicheere amelewa na kiburi cha madaraka anasema wastaafu hawachangii.
 
Kwani wanazokwapua wakiwa ofisini hazitoshi kuishi milele kwa raha mustarehe mpaka asumbuliwe na mafao ya uzeeni?

Kumbuka mafao ni kwaajili ya wenza wa viongozi wenu pia, WOTE WAKIWA HAWACHANGII sumni, wakipewa vinono kwa utumishi wa miaka michache.

Wanaochangia kwa miaka 36, wanapewa 33% tu ya haki yao na kuambiwa mwisho wa monthly pension ni miaka 12 ILHALI wasiochangia ambao wanalipwa mshahara kwa nafasi walizoomba wenyewe, wanalipwa mpaka KUFA.

Mtumishi kaongezewa tsh 23,000 kama nyongeza ya mshahara, IMETANGAZWA KITAIFA, MBUNGE kaongezewa MILIONI 5, hakuna aliyeambiwa! Ajabu, watumishi 500,000 hawana la kufanya...pathetic fools.

Hakuna serikali inaweza ku-replace watumishi 200,000 tu kwa pamoja; wapumbavu 400 Bungeni wanafaida gani ya nyongeza ya 5m monthly, kisha kulipwa 290m kama mafao kila baada ya miaka 5? Na ndio hao waliopitisha 33% kwa mtumishi wa miaka 36!

TUENDELEE TU kuhoji kwenye mitandao, WAO wanakwapua kihalisia!
 
Watu wanalipa bima kama kinga ya majanga yanayoweza kutokea hapo baadaye vinginevyo haina maana na mtu hastahili kulipa.

Sasa CAG Kichele unaposema wastaafu na wenza wao wanafilisi Mfuko wa Bima ya Afya ni kichekesho na inaelekea hujui maana ya BIMA!

Sasa tueleweshe kwa uelewa wako "Bima ni nini?" Hao wazee wamelipa Bima muda wote wakiwa katika ajira zao kwa matumaini kuwa iwafae uzeeni sasa wewe unakuja na ngonjera zako kuwa wanafilisi Mfuko, umetumia kigezo gani?

Mfuko huu usigeuzwe kuwa sehemu ya mapato ya serikali bali kinga ya afya ya wanachama na hasa wazee!

Vinginevyo ni WIZI wa fedha za wanachama!
 
Naona Kichere anataka serikali itutelekeze kabisa ili tufe mapema kuwe na saving kubwa kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii.

Yeye akistaafu analipwa 80% ya mshahara wa CAG aliyeko ofsini pamoja na huduma zingine ikijumuisha matibabu na usafiri.
 
Back
Top Bottom