GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 63,575
- 127,912
Mimi Kibwana Dachi wa Magic Fm, katika kipindi cha Morning Magic cha leo tarehe 16/07/2015 nakubali kwamba nilifanya kosa la msingi la kuzungumzia jambo linalohusu uchawi na kulihusisha Kanisa Katoliki, kwanza naomba radhi kwa usumbufu niliousababisha kwa watanzania wenzangu hususan wale waamini wa dhehebu hilo, ukweli nilichotaka kusema ni kwamba, Kanisa hilo lina idara maalum ambayo inatafiti uwepo wa uchawi duniani.
Idara hii ipo Vatican na nia yake ni kujua ukweli na si vinginevyo, lakini kutokana na hilo wengi wanahusisha uwepo wa tukio la kuwepo Moshi mweusi au mweupe wakati wa kumchagua PAPA ni tukio linalotokana na "utafiti huo", ukweli kinachosababisha hilo ni maombi ya dhati yanayofanywa na maaskofu na mapadri wakati wa mchakato wa kumpata Papa mpya haina uhusiano na utafiti huo narudia tena.
Hivyo nawaomba radhi wale wote niliowakwaza kwa kuwa najiamini mimi ni mtu makini ila wakati mwingine nafanya makosa ya kibinadamu.
Afanye haraka kabla hatujamshughulikia. Sisi wakatoliki hatuamini ushirikina. Aharakishe
Hua siyo msemaji sana humu jamvini japo ni mwanajamvi hili. Kiukweli sijapata nafasi ya kusikiliza hii radio kwa leo. Ila kama ni kweli kayasema haya basi atuombe radhi mara moja wakotoliki si tu kwa Tanzania bali kwa ulimwengu wa kikatoliki. Catholic church means 'universal Church'.
Kijana, hayakusaidii lolote hayo mambo, hii dunia huwezi kumlazimisha kila mmoja awaze unavyowaza wewe, soo ukitaka kila kitu kiwe katika njia unayotaka wewe basi dunia isingekuwa hivi ilivyo
Afanye haraka kabla hatujamshughulikia. Sisi wakatoliki hatuamini ushirikina. Aharakishe
Kuamini kwamba uchawi upo ni TOFAUTI kabisa na kuamini katika uchawi. Hoja hapa ni kwamba mleta mada amemsikia mtangazaji mmoja akisema kwamba RC wanaamini uchawi. Na kama nia yake ingekuwa kusema 'wanaamini kuwa kuna uchawi', basi ingekuwa wakristu wote au watu wote wanaotumia biblia, lakini yeye amesikika akisema Roman CatholicUchawi ni miongoni mwa mambo ya Kishirikina, na nijuavyo mimi dini kubwa duniani zinaamini uwepo wa mambo hayo kwa sababu yameandikwa katika maandiko matakatifu. Sasa wewe ukikataa SI UNAPINGA BIBLIA?
Kuamini kwamba uchawi upo ni TOFAUTI kabisa na kuamini katika uchawi. Hoja hapa ni kwamba mleta mada amemsikia mtangazaji mmoja akisema kwamba RC wanaamini uchawi. Na kama nia yake ingekuwa kusema 'wanaamini kuwa kuna uchawi', basi ingekuwa wakristu wote au watu wote wanaotumia biblia, lakini yeye amesikika akisema Roman Catholic