Kibwana Dachi tuombe radhi Wakatoliki

Kibwana Dachi tuombe radhi Wakatoliki

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
63,029
Reaction score
126,474
Leo Katika Kipindi Chao Cha Morning Magic Kinachorushwa Na Radio Ya Magic FM Akiwa Na Mtangazaji Muongozaji Wao Orest Kawau, Maria Edward Na Salum Mkambala Huyu Mtangazji Mzee Kibwana Dachi Tena Katika Hali Ya Kujiamini Kana Kwamba Yeye Anayajua Mambo Ya Dhehebu La WAKATOLIKI Huku Akiwa Anatoa UFAFANUZI Kwa Kuhusiana Na Moshi Mweupe Na Mweusi Ambao Huwa Unatoka Wakati Makadinali Duniani Wakiwa Katika Mchakato Wa Kumtafuta PAPA.

Yeye KIBWANA DACHI Tena Kwa Mbwembwe Zote Na Akitamka Kabisa Kwa Wenzake Namnukuu ;

" Jamani Hili Halina Ubishi Wala Usiri Na Nasema Ukweli Kuhusiana Na Hili Jambo Ambapo Ni Kwamba Duniani Kote Hakuna Kanisa Ambalo LINAAMINI USHIRIKINA Kushinda Yote Kama La WAKATOLIKI " Mwisho Wa Kumnukuu.

Na Bahati Nzuri Hiyo Kauli Yake Naamini Hata Watu Wa TCRA Watakuwa Wameirekodi.

Nikiwa Kama Mmoja Wa WAKATOLIKI Tena NILIYETUKUKA Kabisa Nawaomba Upesi Na Haraka Sana Mabosi Zake Hawa Watutake Radhi WAKATOLIKI Wote Tanzania


  • Dina Chahali
  • Dativas Mango
  • Nicky Ngonyani
  • Orest Kawau

Kisha Na Yeye Mwenyewe KIBWANA DACHI Kupitia Radio Yake Hiyo Hiyo Anayoifanyia Kazi Ya Magic FM Na Kwa Ukubwa Na Umuhimu Ule Ule ATUOMBE RADHI Sisi WAKATOLIKI Wote Nchini Tanzania Kabla Na Sisi Hatujachafua Hali Ya Hewa Kuanzia Kwa Dini Yake ( Ambayo Tunaijua ), Alichokifanya Mzee Wake Wakati Akiwa Afisa Mwandamizi Wa Jeshi La Polisi, Maisha Yake Binafsi Na Bila Kusahau Na AFYA YAKE Kiujumla.

AMETUDHALILISHA KULIKOTUKUKA SISI WAKATOLIKI WOTE NCHINI TANZANIA Na DUNIANI KWA UJUMLA. Na Najua Humu JF Yupo Na Hata Hao Mabosi Zake Niliowataja Hapo Na Wafayakazi Wenzake Wapo Humu Naomba Wamtaarifu Na ATUTAKE RADHI UPESI Na HARAKA Kabla Watu HATUJAFUNGUKA Na KUFUNGUKA Juu Yake Kwa Tunayoyajua.


====

JAMIIFORUMS
: Tumepokea ujumbe kutoka kwa Kibwana Dachi kuhusiana na hili suala. Ujumbe wenyewe ni huu hapa;


Mimi Kibwana Dachi wa Magic Fm, katika kipindi cha Morning Magic cha leo tarehe 16/07/2015 nakubali kwamba nilifanya kosa la msingi la kuzungumzia jambo linalohusu uchawi na kulihusisha Kanisa Katoliki, kwanza naomba radhi kwa usumbufu niliousababisha kwa watanzania wenzangu hususan wale waamini wa dhehebu hilo, ukweli nilichotaka kusema ni kwamba, Kanisa hilo lina idara maalum ambayo inatafiti uwepo wa uchawi duniani.

Idara hii ipo Vatican na nia yake ni kujua ukweli na si vinginevyo, lakini kutokana na hilo wengi wanahusisha uwepo wa tukio la kuwepo Moshi mweusi au mweupe wakati wa kumchagua PAPA ni tukio linalotokana na "utafiti huo", ukweli kinachosababisha hilo ni maombi ya dhati yanayofanywa na maaskofu na mapadri wakati wa mchakato wa kumpata Papa mpya haina uhusiano na utafiti huo narudia tena.

Hivyo nawaomba radhi wale wote niliowakwaza kwa kuwa najiamini mimi ni mtu makini ila wakati mwingine nafanya makosa ya kibinadamu.
 
Uchawi ni miongoni mwa mambo ya Kishirikina, na nijuavyo mimi dini kubwa duniani zinaamini uwepo wa mambo hayo kwa sababu yameandikwa katika maandiko matakatifu. Sasa wewe ukikataa SI UNAPINGA BIBLIA?
 
Afanye haraka kabla hatujamshughulikia. Sisi wakatoliki hatuamini ushirikina. Aharakishe

Huyu Jamaa Kanifanya Asubuhi Yangu Ibadilike Na Iwe Mbaya Kwani AMENISIKITISHA KULIKOTUKUKA.

Na Kibaya Zaidi Kaongea Hivyo Akijisahau Kuwa Yeye ni Muislamu tena aliyetukuka na sasa yupo katika mwezi mtukufu wa Ramadhan. Nasubiri msamaha wake ndipo akili yangu iweze kukaa sawa. Katutukana kulikotukuka Wakatoliki wote Tanzania na sitaki kuamini kuwa ndugu zetu Waislamu wana maneno kama hayo ya chuki na kashfa dhidi ya Wakatoliki bali ni akili yake tu ndio imemtuma.

Akizidi kukaa kimya nasi tutakunjuka kumhusu yeye na hatofurahi kwani data zake zipo za kutosha tu. Sijawahi kukasirika na kuchukia kama asubuhi ya leo.
 
Hua siyo msemaji sana humu jamvini japo ni mwanajamvi hili. Kiukweli sijapata nafasi ya kusikiliza hii radio kwa leo. Ila kama ni kweli kayasema haya basi atuombe radhi mara moja wakotoliki si tu kwa Tanzania bali kwa ulimwengu wa kikatoliki. Catholic church means 'universal Church'.
 
Hua siyo msemaji sana humu jamvini japo ni mwanajamvi hili. Kiukweli sijapata nafasi ya kusikiliza hii radio kwa leo. Ila kama ni kweli kayasema haya basi atuombe radhi mara moja wakotoliki si tu kwa Tanzania bali kwa ulimwengu wa kikatoliki. Catholic church means 'universal Church'.

Akhasante Mkuu Na Tupo Pamoja.
 
Amesema hivyo??

Basi ingekuwa busara kama Ch10 wangemsimamisha kazi huyo Dachi.

Halafu mkuu wa idara ya huyo Dachi, HR na MD/CEO wao wanapaswa haraka waliombe radhi Kanisa Katoliki kwenye taarifa yao ya habari ya saa moja usiku.

Imani na chuki zake binafsi za kidini asizirushe hewani. Abaki nazo moyoni mwake zimsonge na kumsumbua.
 
Labda elezea kisa kizima ilikuwaje akaongea hivyo na mada ilihusu nini.
Then tutajua kama ni kashfa au ni sentensi katika maelezo ambayo yamekupa shida kuelewa
 
mkuu,tumsifu Yesu Kristu,kwanza kabisa nashangaa kusikia wewe ni mkatoliki kwani katika katoliki hatuna watu wa aina yako.mimi ni mkatoliki damu na napingana na wewe kwa asilimia mia mbili kwa sababu zifuatazo:

1.wakatoliki huwa hatushughuliki na vitu au watu ambao siyo kikwazo katika imani yetu. kwa maneno aliyotamka huyo dachi sijui nani, hayajapunguza wala kuongeza imani yetu. tutaendelea kuwa imara kama kawaida. yaani kwa mkatoliki hayo maneno siyo hata kitu cha kukera. ameongea amemaliza, imani yetu ilikuwepo,ipo na itaendelea kuwepo. Nakushangaa mkatoliki wa aina gani wewe.

2.sisi siyo watu wa visasi. hicho unachotaka kukifanya usipoombwa radhi ni wewe mwenyewe na siyo ukatoliki. kama unataka akuombe radhi nenda ukaombwe mwenyewe kama jentamaizini na siyo kwa mwamvuli wa ukatoliki. na hayo utakayoyafanya usipoombwa radhi uayafanye kama wewe na siyo ukatoliki.

3."mpende jirani yako usimchukie, wapendeni adui zenu waombeeni wanaowaudhi ili mpate kuwa wana wa baba aliyembinguni" nadhani kwa kauli hii nimeeleweka. na kauli hii ndiyo ya ukatoliki.

4.ukweli ni kwamba wakatoliki sisi wenyewe tunajua hatuamini katika ushirikina. kwa hiyo mtu akitusema tofauti hiyo haiondoi imani yetu.kwanini tuhangaike nae? we are not after phyisical things, we are after spiritual gifts. maneno yoyote hayo hayaondoi imani yetu. tuna kawaida ya kusamehe na kuendelea na mambo yetu. kumbuka gwajma alivyomtukana pengo, ulisikia pengo akitaka kuombwa radhi? wewe ni aina gani ya mkatoliki?

mwaisho kabisa sioni misingi yako katika ukatoliki. kama kweli wewe ni mkatoliki basi umetoka kwenye reli, jitambue na ujirudi haraka sana. kama ni kutukanwa huwa tunatukanwa sana, tutabaki kila siku kutoa matamko ya watu kutuomba radhi badala ya kushughulika na mambo ya kiimani zaidi.
 
Kijana, hayakusaidii lolote hayo mambo, hii dunia huwezi kumlazimisha kila mmoja awaze unavyowaza wewe, soo ukitaka kila kitu kiwe katika njia unayotaka wewe basi dunia isingekuwa hivi ilivyo

Mkuu, sijapata kuona Wakatoliki wa ajabu kama huyu mtoa mada na wote wanaomshabikia. Wamejaa chuki pale ambapo wanapaswa wasamehe na kuombea
 
Uchawi ni miongoni mwa mambo ya Kishirikina, na nijuavyo mimi dini kubwa duniani zinaamini uwepo wa mambo hayo kwa sababu yameandikwa katika maandiko matakatifu. Sasa wewe ukikataa SI UNAPINGA BIBLIA?
Kuamini kwamba uchawi upo ni TOFAUTI kabisa na kuamini katika uchawi. Hoja hapa ni kwamba mleta mada amemsikia mtangazaji mmoja akisema kwamba RC wanaamini uchawi. Na kama nia yake ingekuwa kusema 'wanaamini kuwa kuna uchawi', basi ingekuwa wakristu wote au watu wote wanaotumia biblia, lakini yeye amesikika akisema Roman Catholic
 
Kuamini kwamba uchawi upo ni TOFAUTI kabisa na kuamini katika uchawi. Hoja hapa ni kwamba mleta mada amemsikia mtangazaji mmoja akisema kwamba RC wanaamini uchawi. Na kama nia yake ingekuwa kusema 'wanaamini kuwa kuna uchawi', basi ingekuwa wakristu wote au watu wote wanaotumia biblia, lakini yeye amesikika akisema Roman Catholic

Akhsante Mkuu Na NASISITIZA Tena Hakusema Kuwa Wakristo Duniani Wanaamini USHIRIKINA Bali Nimemsikia Mwenyewe Kwa Masikio Yangu Mazima Na Akili Zangu Timamu Mtangazaji Kibwana Dachi Akisema Kuwa Dhehebu La WAKATOLIKI LINAAMINI SANA USHIRIKINA Na Naomba Kama Mimi GENTAMYCINE Nimemsingizia Huyu MTANGAZAJI Basi Naomba ISIFIKE Hata Saa 6 Mchana NILAANIKE au NIPATWE Na JAMBO Baya. Najiamini 100% Kwa NILICHOKIWASILISHA Hapa Kwenu.
 
Kwanza kabisa atupe mifano ya imani ya ushirikina wa kanisa katoliki, usikimbilie kutishia watu, je kama kweli.
 
Back
Top Bottom