Kibuti kimeback fire... Nacheka kama vile mazuri

Sio lazima nichangie content ila shida ipo hapo kwenye lugha uliposema "alikucheat" kwamba amwpata bwana wa kumuoa kimsingi mtu ambae umeachana nae hawezi kukucheat bali anakudanganya i.e" Lie" maana cheating inatumika kwa mtu ambae mna uhusiano nae..ila sababu hii lugha ilikuja na ndege na ikaondoka na ndege upo sahihi kwa kiasi fulani...
Hahah st marys

Sent using Uncesored Device
 
Kuna vile amekuona mwepesi.mimi nakushauri uachane naye kabisa ila kama una roho ya chuma mtumie kuichapa kwa sana

Wa sukumaland
 
Huu uzi nimeusoma vizuri mpaka mwisho. Mimi, kuna wakati huwa naumia sana kuona mwanamke akimwaga machozi, so sad!

Kuendana na uzi wako bwana KIUNGOMCHEZESHAJI, sometimes kwenye haya mapenzi tatizo sio kunyea kambi tu. Chukulia kuwa kila mwanadamu ni mkosaji, na wewe usijipe moyo kuamini kwamba huyo manzi labda bado anakupenda sana, anakumbuka zile style zako za chuma mchicha, sijui biashara imebuma, sijui nini... Hapana bwana, hakuna cha biashara imebuma, wala mapenzi!

Anachokifanya huyo manzi kwako ndicho anachowafanyia wanaume wengine huko alipotoka, hata kwako hakuna jipya hapo ni kama mnatengeneza movie tu! Kama aliweza kukuacha, baadae akarudi kwa udhaifu wako ukaamua kula matapishi basi elewa tu kwamba kila njia yenye kwenda ipo pia ya kurudi kasoro ile ya kukielekea kifo, hukifa hurudi. Lakini njia zingine zote zinamarejeo... Huyo Manzi ana haki ya kurudi kwako wewe Mlamatapishi, ndio sababu ya kilio chake.
 
Kuna misemo mingi sana ambayo wahenga walituachia, laiti tungeifanyia kazi maisha yangekuwa poa kabisa aisee. Ila binadamu wengine wana masikio yaliyozibwa pamba, macho yana upofu na mwishowe ni ajali ya maisha. Mfano,
  1. Usinyee kambi.
  2. Usitukane wakunga na uzazi ungalipo
  3. Usitukane mamba kabla hujavuka mto.
Sasa kuna bidada ananisumbua sana, na mimi nimeamua liwalo na liwe. Tulianza mahaba yetu miaka ya 2013 mpaka 2014. Tukaachana 2015 kwa sababu zilizo nje ya uwezo wa kila mmoja wetu. Tukaja kuonana tena 2017. Hapo kati tulipokuwa mbali mbali mwenzangu akanijulisha kuwa kapata bwana wa kumuoa, off course alinicheat kuwa ameolewa, kumbe walikamatana tu wakaanza kuishi kinyumba. Walivyoanza walikutana na jamaa kwenye basi wakiwa safarini, wakafahamiana, wakapeana namba mambo yakanoga. Jamaa ni mfanyabiashara na ana pochi nene usiombe. Mara paap, jamaa akaja kumpangishia nyumba Dar. Bidada akajifungua mtoto wa kiume 2016. Kipindi hicho binti alikuwa na nyodo kweli hata tukiwasiliana dharau si dharau basi ananijibu kama hanijui vile.

Mwaka 2017 mwishoni hivi, nikaona bidada anaanza mawasiliano na mimi mpaka nikawa nashtuka kulikoni? Kumbe buana alikuja kugundua jamaa ana familia, mke na watoto wanne mambo yakawa fayaaaaaaaaaa. Pakawa hapakaliki wala hapatoshi. Kama haikutosha akaja kugundua jamaa anadate na wanawake wengine wawili, mmoja ni askari polisi. Jeuri ya hela buana, acha tuu. wakatifuana sana mpaka binti akaondoka kwa hasira akaenda kupanga chumba mtaani ili mradi aachane na jamaa. Kipindi hiki ndo alikuja kurudisha majeshi kwangu. akanieleza yote yaliyomsibu mpaka kuamua kuachana na huyo mwanaume. Nikasema poa ila tukacheki afya kwanza, haikuwa tatizo mambo yakawa poa. Ila moyoni mwangu nilijua sitakiwi kuingia mazima mazima kwa single mothers hawaeleweki, pia status yake na huyo aliyezaa naye kumwamini maelezo yake siyo kirahisi kivile, may be wanaweza kurudiana nitajuaje. kwa hiyo niliamua kumpenda kwa akili zaidi kuliko moyo.

Mwishoni mwa mwaka jana 2018, December akaniambia anaacha kazi ya kufundisha maana shule aliyokuwa anafanyia kazi hawalipi mishahara kwa wakati na tena ni midogo sana. Akasema baba yake atampa mtaji wa milioni 7 akafanye biashara, basi akawa ananioma mawazo biashara gani nzuri afanye

Wakati hayo yakiendelea nikalogwa na nani sijui nikaishika simu yake, nikakuta anadate na mwanaume mwingine yaani mambo moto moto. Kitendo cha mimi kuhoji huyu ni nani ikawa kosa, akawa mbogo usipime. Nikasema ok, yaishe. Mapenzi yakapungua kidogo. Baba yake alivyopokea penshen january mwishoni, huyu mrembo akafanya mambo yake kimya kimya, akakata mawasiliano na mimi. Akahama pale alipokuwa anaishi, akaenda kufungua kibanda cha m pesa, tigo pesa na kuuza maji na soda sehemu nyingine. Nikimpigia simu hapokei, nikituma sms hajibu, mara moja moja akijibu anatuma sms fupi sana "achana na mimi" Nikasema poa.

Sasa Juzi kati nikashangaa anaanza tena kunitafuta tena kwa staha adabu na heshima, anatuma sms za mahaba uuuuh. Nikaona isiwe tabu, nikawa nascreenshot zile chats zake za kuniambia tuachane, namtumia. alafu nakula kimya. Hivi majuzi alinitafuta sana nikapokea, daaah tuliongea, akanibembeleza, akaniomba msamaha mpaka alilia sana Nilimwambia nimekusamehe ila najua uko vizuri huhitaji tena msaada wangu maana una pesa zako, alafu una mtu wako mimi sina thamani yoyote tena. If you make me a spare tyre, i make you an emerdency door. Hiyo sms ilimuuma sana, akapiga tena simu alilia weeeeee, nikamjibu in short, nimekusamehe, relax, and goodbye. Nikakata simu.
Juzi ijumaa akanibembeleza sana aje kwangu leo nikamwambia sawa karibu, akaniambia hana nauli nimpromise nitampa nauli ya kuja na kurudi nikasema poa. Sasa leo asubuhi sijapokea simu yake nilijua tu ataniambia niko njiani nakuja. Baadaye kidogo akanitumia sms "niko getini" nikamwambia nimesafiri kwenda bagamoyo nitarudi usiku. Ukweli niko getoni kwangu nakula bata. Pale getini niliwaelekeza walinzi kuwa huyu mtu asije akaingia humu ndani, mwambieni kiungomchezeshaji amesafiri, alitoka na gari asubihi na alikuwa amebeba sanduku.

Kilichofuata nilitumiwa sms ya matusi ya aina yake.
Nikawacheki walinzi baadaye wakaniambia wewe mwanaume mkatili sana. Mtoto wa watu anaupigia simu hata hupokei zaidi ya mara kumi. Mpaka ameshindwa kujizua mpaka amelia machozi hadharani amekukosea nini? Nikawajibu siyo kazi yenu.

Hili liwe fundisho kwa wadada, unapoondoka usinyee kambi. Mimi mpaka sasa hivi nashindwa kuelewa tatizo ni nini, biashara inabuma au ni mapenzi tu anakosa mashine, mi sielewi na sitaki kujua.
Baada ya kusoma mistari yako mirefu nimekuelewa kijana, kiufupi huyo demu anakudharau, kakuona boya au poyoyo. Kila akiharibu kule anapopenda anarudi kwako kuondoa stress.

Jitambue na ubadilike, acha kulea ujinga itasaidia maishani, haiwezekani demu umeanza nae, anaenda kuzalishwa halafu anarudi tena kwako, ushamba gani huu!!!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom