Kibonzo: Kuna kiongozi mfu anaangushiwa takataka

Kuna ukweli, sometimes lugha na hata matendo yaliyokuwa yakifanywa na mheshimiwa yule yalikuwa yana tia hofu na hata kuwa kero kubwa kwa jamii.
Wasiojulikana
Kodi hewa
Kughushiwa mashtaka kubambikwa
Kunyang'anywa mali kwa nguvu
Kuna "waliopotea"
Ukabila(Sukuma Gang)-watu tunaanza kusahau

Lakini vile vile kuna aliyofanya vema
Vituo vya afya
Barabara
Ndege(ingawaje zipo mbovu)
SGR-hata kama haijakamilika
Bwawa la umeme JNHEPP-Stiglaz

Jukumu letu ni kupembua jema na baya lake.
Lakini kula na kunywa(ufisadi) na kutupia takataka kaburini?
 
Mkuu,

Hicho kitu ukichokisema ni muhimu sana.

Jana nilikuwa nafikiria legacy ya Magufuli.

Nikasema hivi, ni vigumu sana kumpata Mtanzania ambaye anaweza kuwa level headed kuhusu Magufuli.

Watu wengi wanaangukia kwenye extremes, ama wanampenda saaaana ama wanamchukia saaana. Ni vigumu kumpata mtu anayeweza kukaa kati akahesabu mazuri na mabaya.

Mimi namlaumu Magufuli mwenyewe kwa haya matatizo, kwa sababu he had all the basics of being successful. Yani Magufuli ilikuwa hata akitaka kufanya kitu kizuri, presentation yake inakuwa na show za kibabe sana mpaka inafuta ule uzuri.

Lakini wabongo ndio walivyopenda hivyo labda.
 
Hao watupa takataka nao wenyewe pia ni takataka tu
 
Hao watupa takataka nao wenyewe pia ni takataka tu
Tanzania huwezi kupata uongozi wa kitaifa bila ya kuwa takataka.

Ile ngazi ya kupanda juu tu imejaa vizingiti vya kukuchafua na kukufanya uwe takataka.

Kwenye chaguzi za ubunge tu utakutana na mambo ya rushwa, uchawa, siasa za udini na ukabila, na ujinga mwingi kama huo.

By time unafikia uwaziri ushafuzu.

By the time unakuwa rais au makamu wa rais, ushakuwa master wa uchafu.

Magufuli hakuweza kuepuka mitego hii, Samia hakuweza.

Uongozi wote umeoza.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…