Kibonde wa Clouds anaharibu

Nyie mnaoleta post kuhusu kibonde mnamkuza bila sababu ni sawa na wasanii wanaojitengenezea kashfa kwenye magazeti ya udaku ili wapate umaarufu na magazeti yanunuliwe sioni sababu ya kumjadili mtu ambaye anaongea upuuzi
 
Mnaojifanya wanaCHDM mtaacha kelele siku si nyingi maana kaz yenu ni kubwabwaja tu dhidi ya serikali nani kawafunza kuwa upinzan maana yake kupinga kila kitu
 
Siyo wana Kusini. Ni watoto wa Mtwara mjini. Waliingia kichwa kichwa kwenye maandamano yenye nia yakupata umaarufu wakisiasa bila kufanya analysis ya matokeo ya agenda yao kwa jamii yenye maono tofauti. Hawakuweza kufanya analysis kujua malipo ya manesi, walimu, mapolisi pamoja na dawa wanazotumia mahospitalini, vitabu shuleni etc pale Mtwara mjini yanatoka wapi. Wangeweza kufanya hilo, wangepata kugundua kuwa pesa hizo kwa kiasi kikubwa hutokana na makato ya Pay as you earn ya watu wanaofanya kazi Tanzania popote pale na zaidi, wale wa Dar. Hilo lingeweza kuwafanya waelewe kuwa rasilimali za nchi hii ni za Watanzania wote na siyo wa eneo zitokako. Ngugu zangu hawa pia wangeweza kujua kuwa kwa vile mkopo wa ujenzi wa bomba hilo umetoka China at a very cheap price, then chances are that the force for them to say NO to the project, may have some western influences, kupitia vyama vilivyoamua kuwatumia. Kama wasomi, we have every reason to say NO to this type of Imperialism. Hayo ni miongoni tu mwa mambo ambayo wakazi wa Mtwara mjini na wale walioletwa kwa malori na vyama vya siasa waliyapuuzia. Besides, tumeambiwa mara kadhaa kuwa hawa ndugu zetu kwa sasa wana-surplus ya umeme by 5MW wakati sisi ndugu zao huku unakatikakatika kila siku, hivi, kuna shida gani kwa wao kutulea ndugu zao sisi ambao nasi ni Watanzania? Je, huu siyo uchoyo? Kama ni kazi, ni Mtanzania yupi anayekatazwa kwenda popote pale Tanzania kutafuta kazi au kusoma na akitaka kuhamishia ule utaalam alioupata kule alikozaliwa? Mimi ni mwenyeji wa Mbinga kule kusini ila naishi Dar na wewe pia inawezekana siyo mzaliwa wa Dar ila unaishi Dar. Jirani yangu hapa naye ni Mmachinga wa Mtwara mjini ila anaishi Dar. Dar ni ya Watanzania wote. Haya yote waliyapuuzia na wakatanguliza sera ya uchoyo blindly.

Mzee wa Bagamoyo ni mambo gani hawa wana kusini waliyapuuza kabla ya kuandamana?
 

kwani sio wapuuzi?!
 
Nakubali kuwa tuna uhuru wa kutoa maoni lakini jambo la kuwaita watu wapuuzi si la kutetea, kibonde kateleza.
Pia, nilichokisikia mimi ni kuwa wana mtwara wanataka kiwanda kijengwe kwao sio kuitumia gas peke yao na kwa maoni yangu wamelenga kupata fursa zitakazoambatana na uwepo wa kiwanda. Mi naona wako sawa, kwanini iwe ni DSM tu? hata miji mingine inahitaji maendeleo na kiwanda ni moja ya hatua za kuyafikia.
 
kwani ni mara ya kwanza kumsikiliza kibonde hasa kwenye issue zenye reaction ya jamii fulani? mi kilawakati kukiwa na watu wanaoriot nimesikia kibonde akiwaita wapuuzi, wajinga, wapumbavu na tena anakandia huyo, mfano madaktari, tanesco, wanafunzi wa vyuo, yeye ni kupindua tu. mzoeeni tu hivyo, mkitaka kumsema, sina uhakika kama anakumbuka kama anaongeaga hivo. hivi ukienda kumuuliza mwendawazimu kwa nini jana umenitukana atakujibu? pengine anaweza akakuongezea tusi kwa kuona kuwa unamchokoza, leave him. kila mtu mwenye madai yeye huwa anachukulia mnaitaabisha serikali ya ccm ambayo ni kipenzi chake, atawatukaneni tu.
 
Wote mlio upande wa Kibonde MLAANIWE na nitaenda kuchukuwa uchawi wa NGENDE niwaroge wote yaan niny pamoja na Kibonde wenu, nitawageuza panya "chamaki nchanga" na nitafanya pati kubwa, nitawaalika wamakonde wote akiwemo Che Nkapa! "tutafaudu"
 
 
Hahaha, Nyani Ngabu, nikikuita mpuuzi utakuwa ok? Umenikumbusha kuna ofisi ilibidi tukubaliane kuwa neno mpuuzi ni offensive na halitatumika kiofisi. Manake tulipata CEO lilikuwa at the tip of her tongue.
Huyo muite Mpuuzi Nyani Ngabu maadamu anakubaliana na hiyo "abusive language". Watu wengine bwana.........................
 

Uko sahihi kabisa NN. Tumechoka kila siku humu jamvini lazima kauli za kibonde zipewe attention....wakati mwingine mnampa mtu umaarufu ambao hana. Nimegundua pia kuwa wengi ni wasikilizaji wa hiyo Redio though kila mmoja anakataa kuwa alishaacha kuisikiliza.....sasa kama hamsikilizi ya kibonde mnayajulia wapi? Kama anawakera si radio zipo nyingi?

Mtu asiyekuwa tayari kusikia maoni ya mtu mwingine ni hatari sana na chanzo cha maafa katika jamii. Si lazima tukubaliane katika kila jambo.
 

kwani kwetu sisi watanzania kuiita jamii fulani ni wapuuzi kwa kipimo cha ufahamu wako sio matusi?
 

Tatizo unajadili kitu ambacho hajakitafakari vizuri. Sioni kama una tofauti na hao waandishi wa tz kama kibonde ambao kila siku wanasubiri huruma ya watawala waweze kukithi haja zao. Wananchi wa mtwara wana hoja ya msingi inayohitaji kujadiliwa na watu wenye mawazo na fikra huru sio kama wewe unayekurupuka. Mnawalisha wananchi wa mtwara maneno wa uongo bila sababu za msingi. Shame on you. Tafuta ukweli na ujadili mada hujui hacha wengine wakupe maneno. Kinachosababisha waandishi kama hawa wa Clouds FM kuact unprofessionally ni kwa sababu ya kutojiamini na kutegemea huruma ya watawala kuliko uwezo wa taaluma yao. Historia imeonesha kwamba waandishi wa habari pamoja na vyombo vyao hushiriki na serikali iliyoko madarakani kugandamiza uhuru wa raia na kuwanyima haki zao kwa kuwaziba midomo. Jikumbushe kilichotokea rwanda wakati genocide. Jikumbushe kesi ya kenya katika mahakama ya the Hughe. Waandishi wa habari na vyombo vyao kama Clouds FM na Startv ni aina vyenye ushirika na watawala kuziba midomo ya raia masikini ili waweze kuendelea kuwatawala kirahisi. Tafakari.
 
Toka Gadner kipindi kimekosa mvuto huwa sisikilizi kabisa bora niskilize choice fm muzik wa kufa mtu
 
Angeegemea CHADEMA mngelia kama mnavyolia humu au ndiyo kwanza mngemwagia misifa kedekede?

We nyani sio lazima utetee kila upuuzi, kibonde ni nani mpak awaite watu wa Mtwara wapuuzi? Uhuru wa kutoa maoni yake anao na ndio hayo yanayotufanya tum judge kama hivyo.
 

Give&Take! Hakuwapa wakamnyima
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…